DKT.SHEIN ATOA MSAMAHA KWA WANAFUNZI 12 WANAOTUMIKIA CHUO CHA MAFUNZO ZANZIBAR
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ametoa msamaha kwa wanafunzi 12 waliokuwa wakiendelea kutumikia vyuo vya Mafunzo vya Unguja na Pemba ikiwa ni miongoni mwa Sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la
Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk.Abdulhamid Yahaya Mzee amsema Rais
amechukua hatua hiyo kwa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 59 cha Katiba ya
Zanzibar 1984.
Mh.Rais ameamuru kuwa kifungo
kilichobaki cha wanafunzi walionufaika na msamaha huo ambao bado wanaendelea
kutumikia katika vyuo vya Mafunzo vya Unguja na Pemba kuwa kipindi hicho chote
kinafutwa na kwamba wanafunzi hao waachiwe huru kuanzia siku ya jana.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Zanzibar inasherehekea
miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar 12 Januari 2018 na kwa kuwa Mhe.Rais
ameridhika kuwa kuna sababu za kutosha za kutumia uwezo wake huo katika sherehe
hii wanafunzi hao waachiwe huru.
Walionufaika na msamaha huo kwa Unguja ni Abdul-Azizi Abdalla
Mohamed,Omar Abdalla Nuhu,Ali Khamis Mrau, Mussa Ali Vuai,Hassan Seif
Khamis,Nassor Abeid Issa,Jihadi Jalala Jihadi na Edward Jeremia Magaja.
Aidha,wengine walionufaika na msamaha huo kwa upande wa Pemba
ni Sleiman Abdalla Amir,Mtumwa Khamis Kaimu,Said Seif Omar na Masoud Seif
Nassor.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments