MANISPAA YA MPANDA KUNUNUA GARI JIPYA LA KUZOA TAKA NDANI YA MWEZI JANUARI MWAKA 2018
Na.Issack Gerald
Halamshauri ya Manispaa
ya Mpanda Mkoani Katavi imesema inatarajia kununua gari jipya la kuzoa taka
kabla ya mwezi Januari mwaka huu kukamilika.
Kauli hiyo imetolewa na
Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo Michael Nzyungu ambapo amesema gari hilo
lenye ujazo wa tani 16 litagharimu kiasi cha shilingi milioni 160.
Aidha Nzyungu amesema
halmashauri inaendelea kukarabati magari ya kuzoa taka yaliyopo huku ikiendelea
kusubiri gari lingine aliloliahidi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipofanya ziara
mkoani Katavi mwaka uliopita.
Hatua ya ununuzi wa gari
jipya ni kufuatia kukithiri kwa taka katika maeneo mbalimbali ya Manispaa hali
inayosababisha wakazi kulalamika huku wakihofia mlipuko wa magonjwa kama
kipindupindu.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments