RAIS KAGAME KUWASILI NCHINI KESHOKUTWA
Rais
wa Rwanda Paul Kagame anatarajia kuwasili hapa nchini kwa ajili ya ziara ya
kikazi.
Kwa
mjibu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda Mhe.Paul Kagame
anayetarajiwa kuwasili nchini Jumapili ya wiki hii.
Makonda
amesema hayo leo akiwa katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam baada ya kuagana
na Rais Magufuli aliyeelekea visiwani Zanzibar kushiriki sherehe za maadhimisho
ya Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mbali
na hilo Makonda amesema kuwa Rais Paul Kagame atawasili nchini Tanzania siku ya
Jumapili ya tarehe 14 ambapo atakuwa nchini kwa ziara ya siku moja na kufanya
mazungumzo na Rais John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments