MKUU WA MKOA WA KATAVI KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU UANZISHWAJI BENKI YA WANANCHI.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali
Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga leo
anataraji kukutana na kuzungumza na vyombo vy ahabari ili kueleza mikakati ya
uanzishwaji wa benki ya Wananchi Mkoani Katavi.
Ofisi za mkuu wa Mkoa(PICHA NA.Issack Gerald |
Taarifa ya Mkuu wa Mkoa ambayo
imetolewa na Katibu wa Mkuu wa Mkoa,inaeleza kuwa kikao hicho kinataraji
kufanyika majira ya saa tano Asubuhi.
Wiki iliyopita wakati akipanga
kuzungumza na waandisahi wa habari,alisema kuwa benki hii malengo yake ni
kumwinua kiuchumi mwanakatavi sanjari na kuongeza mapato ya mkoa kwa kuwa benki
hii itatumiwa na wanakaziu wa mkoa wa katavi.
Mpaka kufikia wiki iliyopita,Mkuu wa
Mkoa alisema kuwa kuna kiasi cha shilingi bilioni 3.2 za kuanzia kama salio
katika akaunti ambapo pia na jengo itakapokuwa benki hiyo limekwishapatikana.
Hata hivyo taarifa rasmi inatarajiwa
baada ya mkuu wa mkoa kuzungumza na waandishi wa habari.
Mwandishi:Issack Gerald Bathromeo
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Habarika zaidi na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments