MBUNGE VITI MAALUMU MPANDA AMWAGA MSAADA WA FEDHA NA BAISKEL KWA WANAWAKE
Wanawake wajasiliamali wakiwa katika mkutano na mbunge viti maalumu Mh.Anna Lupembe(PICHA NA.Issack Gerald) |
Mbunge viti maalumu akizungumza na wanawake wajasiliamali katika viwanja vya shule ya Msingi Kashato(PICHA NA.Issack Gerald) |
MBUNGE wa Wakati huo huo Mh.Anna Lupembe
amekabidhi Shilingi milioni 4 kwa vikundi 40 kati ya 80 vya wanawake alivyoviunda na kuvipatia elimu ya
ujasiliamali Aprili mwaka huu.
Fedha hiyo ameikabidhi kwa wanawake
hao katika mkutano ambao ameufanya akiwa na wanawake hao katika viwanja vya
shule ya Msingi Kashato Mpanda Mjini.
Amesema kuwa vikundi vingine 40
ambavyo havijapatiwa fedha hiyo ili kuanzisha miradi ameahidi kuwapatia fedha
hiyo mwezi Septemba mwaka huu.
Katika vikundi hivyo kila kikundi
kimepatiwa shilingi laki moja.
Katika hatua nyingine Mbunge huyo amekabidhi
baiskeli tatu kwa wanawake wenye ulemavu mmoja akitokea Manispaa ya Mpanda na
wawili Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo.
Aidha mbunge huyo ameahidi kuendelea
kuwasaidia wanawake wajasiliamali watakaokuwa wameonesha kuzitumia vizuri fedha
wanazopatiwa ili kuanzishia miradi ya maendeleo.
Hata hivyo amewataka wanawake kuwa
wamoja kwa kupendana na kusaidiana katik ashida mbalimbali na kuacha malumbano
yasiyokuwa na tija kwao.
Nao baadhi ya wanawake waliopatiwa fedha
hiyo wamempaongeza mbunge wao kwa kuendelea kutekeleza ahadi alizozitoa wakati
wa kampeni za uchaguzi mwaka 2015.
Mpaka sasa kuna vikundi vinmgi vya
wajasiliamali Mkoani Katavi ambavyo vimekwisha patiwa elimu ya ujasiliamali
ambapo kinachosuburiwa na namna ya kusaidiwa ili kupunguza ugumu wa maisha.
Mwandishi:Issack Gerald Bathromeo
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Habarika zaidi na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments