MANISPAA YA MPANDA 2016 YAPANGA KUFAULISHA WANAFUNZI KWA 98% KWA SHULE ZA MSINGI
MANISPAA ya Mpanda iliyopo Mkoani
Katavi imepanga kufaulisha wanafunzi wa shule za msingi kwa asilimia 98.
Baadhi ya wanafunzi Shule ya Msingi Nsemulwa Manispaa ya Mpanda wakiwa darasani(PICHA NA.Issack Gerald) |
Hatua hiyo imebainishwa Mkuu wa idara
ya elimu(Afisa Elimu) Manispaa ya Mpanda Bw.Visent Kayombo wakati akieleza
mikakati ya Manispaa kuendelea kufanya vizuri katika matokeo ya mtihani kwa
shule za msingi 36 zilizopo katika Manispaa hiyo.
Amesema kuwa katika matokeo ya
mtihani kwa mwaka 2014 manispaa ya Mpanda ilifaulisha kwa 90% na asilimia 97%
kwa 2015 Manispaa ya ilishika nafasi nafasi ya kwanza kati ya shule zote nchini
ambapo kwa mwaka huku mwaka 2013 wakati Mpango wa Matokeo Makubwa sasa(BRN)
ilifaulisha kwa asilimia 62%.
Aidha Bw.Kayombo ameiomba serikali ya
Mpanspaa ya Mpanda na Mkoa kwa ujumla kutoa motisha kwa walimu ikiwa ni pamoja
na na Manispaa kutoa mahitaji yote yanayotakiwa kuhakikisha ufaulu unaendelea
kuongezeka na kuendelea kuwa namba moja ukilinganisha na shule zote za Msingi Tanzania.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa
Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda Mh.Willium Philip Mbogo ameiomba Manispaa ya
Mpanda kuzingatia mahitaji yote yatakayokuwa yakihitajika kuendeleza elimu
yenye ufaulu wa hali ya juu.
Hata hivyo akitoa taarifa ya
Manispaa,Mkurugenzi Mpya wa Manispaa ya Mpanda Bw.Michael Fransis Nzyungu
amesema Manispaa ya Mpanda ambayo ni miongoni mwa Halmshauri 5 za Mkoa wa Katavi,ina
jumla ya shule za msingi 36 zikiwemo mbili za binafsi huku shule za sekondari
zikiwa 14 ambapo hata hivyo kati ya idadi hiyo 4 zikiwa za binafsi.
Aidha Bw.Nzyungu amesema kuwa
Manispaa ina vyuo 3,chuo cha ualimu,Chuo cha Ufundi Veta na Chuo Kikuu Huria.
Aidha amesema kuwa Manispaa kwa mwaka
wa 2016,Maspaa ya Mpanda ina jumla ya wanafunzi 34552 waliosajiliwa kwa Shule
za msingi kuanzia chekechekea hadi darasa la saba ambapo wavulana ni wanafunzi17107
na wavulana wanafunzi 17445
Kwa upande wa Sekondari amesema kuwa
Manispaa ina jumla ya wanafunzi 50029 wavulana wakiwa 2197 na wasichana2832 ambapo
hiyo ni idadi inayoanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha sita.
Hata hivyo chanagamoto iliyopo kwa
shule za Mkoa wa Katavi ni Uhaba wa vyumba vya madarasa kwa shule za Mkoa wa
Katavi ambapo Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga
amesema mshikemshike wa ujenzi wa madarasa unatarajia kuanza hivi karibuni
baada ya tatizo la madawati kutatuliwa mkakati wa ujenzi wa madarasa ambapo
kila kijiji au mtaa unatakiwa kufyatua tofari milioni moja.
Mwandishi:Issack Gerald Bathromeo
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Habarika zaidi na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments