MKOA WA KATAVI WABAKIZA MADAWATI 2108 KUMALIZA TATIZO LA MADAWATI SHULENI,MKUU WA MKOA ASEMA KIKOMO CHA TATIZO JULAI 31 MWAKA HUU.
Mkoa wa Katavi umekamilisha madawati 13915 kati ya madawati 15452 yanayotakiwa kukamilisha idadi ya
madawati yatakayokuwa yakikidhi idadi ya wanafunzi kwa shule za msingi ambapo
mpaka sasa uhaba wa madawati kwa Shule za Msingi Mkoani ni madawati 1537.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa
Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga baada ya kupokea msaada wa madawati 146 kutoka kwa mbunge wa viti maalumu
Mkoani Katavi Mh.Anna Lupembe ambapo madawati hayo yaliyotokana na Mamlaka ya
Bandari Tanzania TPA makabidhiano ambayo yamefanyika katika viwanja vya shule
ya Msingi Kashaulili.Sehemu ya madawati 327 yaliyokabidhiwa na wabunge Manispaa ya Mpanda(PICHA NA.Issack Gerald) |
Jenerali Muhuga pia amesema kuwa upungufu
wa madawati kwa shule za sekondari ni madawati 571 ambapo yaliyokwishakutengenezwa ni madawati 1642 huku jumla ya madawati
yanayotakiwa yakiwa madawati 2213.
Katika hatua nyingine Mbunge huyo wa
viti maalumu amechangia bati zenye thamani ya shilingi milioni 2 kwa ajili ya
ujenzi wa madarasa katika shule ya Msingi Nsemulwa iliyopo Manispaa ya Mpanda
yenye zaidi ya wanafunzi 2500
wakiwemo zaidi ya 800 wa darasa
chekechea na darasa la kwanza huku vyumba vya madarasa vikiwa 7 ambapo kwa
uwiano wa wanafunzi waliopo ukilinanisha na walimu waliopo,kila mwalimu
analazimika kufundisha wanafunzi 200.
Kwa upande wake Mbunge wa Mpanda
Mjini Mh.Sebastian Simon Kapufi amechangia madawati 181 ambayo nayo
yamekabidhiwa jana kwa mkuu wa Mkoa ambapo hata hiyo baada ya
kuchaguliwa,mwanzo mwa mwaka huu,kila kata ya Manispaa aliipatia shilingi milioni
moja kwa ajili ya utengenezaji wa madawati.
Aidha pamoja na kuwapongeza wakazi wa
Mkoa wa Katavi kwa kuwa na moyo wa kuchangia maendeleo katika miradi
mbalimbali,mkuu wa Mkoa pia amesema kuwa madawati yote yanatarajia kukamilika
ifikapo Julai 31 mwaka huu.
Mwandishi:Issack Gerald Bathromeo
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Habarika zaidi na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments