BALAZA LA MADIWANI LAOMBA SHERIA ZA ZIMAMOTO KUPITIWA UPYA,MBUNGE VITI MAALUMU PAMOJA NA MAMBO MENGINE KULISEMA BUNGENI.
Na.Issack Gerald Bathromeo-Katavi
BARAZA la madiwani la Halmashauri ya
Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi limeliomba jeshi la zimamoto na uokoaji Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi kupitia upya
sheria inayomtaka mwananchi kuchangia kiasi kikubwa cha fedha ukilinganisha na
uwezo wa mwananchi kumudu gharama hizo kwa mwaka.
Wataalamu mbalimbali katika Manispaa ya Mpanda wakishiriki kikao cha mwaka cha Baraza la madiwani Manispaa ya Mpanda(PICHA NA.Issack Gerald) |
Ombi hilo limetolewa na madiwani wapatao
22 wanaounda baraza hilo kupitia mkutano mkuu wa kufunga mwaka wa fedha
2015/2016 mkutano ambao umefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya
Mpanda.
Aidha Baraza limebaini kuwa mwananchi
huchangia kuanzia shilingi laki moja na nusu(150,000/=) kwa ajili ya gharama za
kujikinga na majanga ya moto huku kiwango hicho kikitajwa kuwa kikubwa huku
wananchi wakionekana kutokuwa na elimu ya kutosha ya kujikinga na majanga ya
moto.
Mara kwa mara wakazi wa Manispaa ya
Mpanda wamekuwa wakilalamika kutozwa kiasi kikubwa cha pesa huku jeshi la Zimamoto
na uokoaji wakilalamikiwa kuchelewa wakati wa majanga ya moto
Kwa upande wake mbunge wa viti maalumu(CCM)
Mkoani Katavi Mh.Anna Lupembe amesema kupitia vikao vya bunge vinavyotarajia kuanza
mwezi Septemba mwaka huu, atawasilisha ombi hilo la Halmashauri kutaka wananchi
wapunguziwe gharama za uchangiaji ziamoto ili kupunguza mzigo mkubwa kwa
mwananchi wa maisha ya kawaida.
Mbunge viti maalumu mkoani Katavi Mh.Anna Lupembe akichangia hojakatika kikao cha mwaka cha Baraza la madiwani Manispaa ya Mpanda(PICHA NA.Issack Gerald) |
Hata hivyo Mstahiki Meya wa Manispaa
ya Mpanda Mh.Willium Mbogo amesema kuwa hata Halsmashauri haina ufahamu wa
kutosha wa namna Zimamoto na Uokoaji wanavyoendesha shughuli zao na kutoza
kiwango hicho cha pesa katika Manispaa.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa sasa
lipo chini ya Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi baada y akuondolewa katika
mamlaka ya Halmshauri miaka ya hivi karibuni.
Katika hatua nyingine Mh.Lupembe amesema
suala la upimaji wa uzito wa mazao ataliwasilisha bungeni ili kupata ufafanuzi
na utatuzi wa vipimo halisi ikiwa mazao yanatakiwa kupimwa kwa kilogramu 75 au
100 kwa kuwa baadhi ya wananchi wamekuwa wakiendelea kudidimia katika umaskini
kutokana na kuuza katika vipimo vinavyowakanganya nje ya matumizi ya rumbesa.
Hatu ya kujadiliwa kwa vipimo halisi
vya mazo imefanyika ikiwa ni baada ya wakulima kulalamika kunyanyaswa katika
upimaji wa mazao.
Hata hivyo ajenda nyingine ambazo zimejadiliwa ni zile zinazohusu sekta ya maji,umeme.afya,elimu,maambara na suala la madawati
Hata hivyo ajenda nyingine ambazo zimejadiliwa ni zile zinazohusu sekta ya maji,umeme.afya,elimu,maambara na suala la madawati
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments