MKOA WA KATAVI KUANZISHA BENKI YA WANANCHI
Na.Issack Gerald Bathromeo-Katavi
Mkoa wa Katavi umepanga kuanzisha
benki ya wananchi kwa ajili kurahisisha na kuharakisha maendeleo ya wakazi wa Mkoa
wa Katavi.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake (hawapo pichani) kuhusu uanzishwaji wa benki ya wananchi(PICHA NA.Issack Gerald) |
Mwenyekiti wa kamati ya Waratibu wa Benki ya wananchi Mkoa wa Katavi |
Akizungumza na Waandishi wa habari
Ofisini kwake,Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga
amesema kuwa benki hiyo inatarajia kuanza kazi yake ifikapo Mwezi Aprili 2017.
Amesema kuwa katika mkutano
unaotarajia kufanyika Kesho Julai 27 na kushirikisha wadau mbalimbali,amewataka
wananchi kujitokeza kutumia fursa ya uwepo wa benki hiyo kijkwamua kiuchumi.
Aidha Jenerali Muhuga amesema katika
kuanzisha benki kunahitajika kiasi cha shilingi Bilioni 3 kwa ajili ya usajili,jengo
na kianzio katika akaunti.
Kwa upande wake Mhandisi Awariywa
Nnko Mwenyekiti wa kamati ya Waratibu Benki ya Wananchi mkoani Katavi ambaye
pia ndiye Katibu tawala Msaidizi kitengo cha Uchumi na Uzalishaji kutoka Ofisi
ya Mkoa wa Katavi amesema miongoni mwa wadau ambao wamealikwa kushiriki katika
kikao cha kesho ili kuchangia fedha za uanzishwaji wa benki hiyo ni pamoja na
mameneja wa Benki Mkoani Katavi,mameneja wa vyama vya ushirika mkoani
Katavi,viongozi wa dini,vyama vya siasa,Chama kikuu cha Ushirika LATCU na
waandishi wa habari.
Mkoa wa Katavi unaanzisha Benki ya wananchi kwa kushirikiana na Jumuiya
Ya Benki za Wananchi Tanzania-Community Banks Association of Tanzania (COBAT)
huku lengo zaidi likiwa ni kupata uelewa pamoja na utaratibu kuhusu manufaa ya
kuwa na benki ya wananchi katika Mkoa wa
Katavi.
Mpaka sasa jumla ya Mikoa 8 ya
Tanzania imekwishaanzisha benki ukiwemo mkoa wa Kilimanjaro na Kagera.
Jumla ya wadau wapatao 400
wanatarajia kushiriki katika Mkutano huo.
Msimamizi mkuu wa benki ya wananchi Mkoani Katavi ni waziri mkuu mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne Mh.Mizengo Kayanza Peter Pinda
Msimamizi mkuu wa benki ya wananchi Mkoani Katavi ni waziri mkuu mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne Mh.Mizengo Kayanza Peter Pinda
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments