Posts

JUMAMOSI KUU

Image
Jumamosi kuu  ni  siku  ya  Juma kuu  inayoadhimisha hasa  pumziko  la  mwili  wa  Yesu Kristo   kaburini  kabla ya  kufufuka  kwa  utukufu   usiku  wa kuamkia  Jumapili  ya  Pasaka . Tarehe  yake inabadilikabadilika kila  mwaka  na hata mwaka uleule ni tofauti katika  madhehebu  ya  Ukristo , hasa yanayofuata  mapokeo  ya  mashariki  na yale yanayofuata mapokeo ya  magharibi . Siku hiyo  Misa  na  sakramenti  mbalimbali haziadhimishwi kwa kuwa  wafuasi  wa  Yesu  wanatulia  kimya  wakitafakari matukio ya  Ijumaa kuu  na kujiandaa washangilie  ufufuko wake kuanzia  kesha  la Pasaka hadi  Jumapili  ya  Pentekoste  siku  50  baadaye. Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

MKUU WA WILAYA AIBULIWA NA SHULE KUITA WAGANGA KUTOKA KONGO

Image
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Said Mohamed Mtanda ametolea ufafanuzi suala la shule ya Msingi Kabwe kuita waganga wa kienyeji kutoka Kongo ili kutatua tatizo la kishirikina linaloikabili shule hiyo.` Mtanda amesema ni kweli alipokea simu kutoka kwa Mkuu wa shule hiyo kumuelezea matatizo yao hapo shuleni na lengo walilofikia serikali ya kijiji ili kutatua tatizo hilo ambalo limekuwa likijitokeza mara kwa mara. Licha ya hayo,mkuu wa wilaya hiyo amesema yeye kama kiongozi wa serikali ni kulichukua tatizo hilo kitaalam kwa kupeleka madaktari ambao watatafuta njia sahihi ya kutibu wanafunzi hao na sio kuruhusu mambo ya kishirikina ingawa hawezi kuwakataza wazee wa kijiji hicho kwani anaheshimu mila zao. Wanafunzi wa kike wa shule ya msingi Kabwe iliyopo Wilayani Nkasi mkoani Rukwa wanakabiliwa na tatizo la kiafya la kuanguka,kuzimia na kupiga kelele jambo ambalo wakazi wa eneo hilo wanahisi linatokana na ushirikina na kuamua kutafuta waganga wa kienyeji ili kutafuta ufumbuzi. Chanzo:ea...

ASKOFU NYAISONGA ATAKA WAKRISTO WATENDE MEMA

Image
Mhashamu Baba Askofu Gervas Nyaisonga Katika maadhimisho ya siku ya Ijumaa kuu kwa wakristo,Askofu wa Jimbo Katoliki la Mpanda Mkoani Katavi   Mhashamu Baba Askofu Gervas Nyaisonga amewataka waumini wa kikristo kuendelea kutenda kutenda mema kama walivyofanya katika kipindi cha mfungu wa Kwaresma. Askofu Nyaisonga ametoa wito huo leo katika adhimisho misa takatifu ya Ijumaa kuu katika ibada ambayo imefanyika katika Kanisa kuu la Bikira Maria Emakulata Jimbo la Mpanda. Kwa upande wao waumini wa kanisa hilo wamesema kipindi cha Kwaresma ni kipindi cha kutafakari wema ambao mungu ameuonesha kwao na hivyo kutakiwa kutenda hivyo hivyo kwa wenye uhitaji. Ijumaa Kuu ni siku maalumu ya mwaka ambayo wafuasi wengi wa Yesu Kristo wanaadhimisha kifo chake msalabani ambacho kilitokea nje ya kuta za mji wa Yerusalemu siku ya Ijumaa ambapo inatanguliwa na Alhamisi Kuu. Sikukuu ya pasaka kwa mwaka 2018 inatarajiwa kuadhimishwa Aprili mosi mwaka huu. Ijumaa kuu kitaifa imeadhimish...

IJUMAA KUU

Image
Ijumaa Kuu  ni  siku  maalumu ya  mwaka  ambayo  wafuasi  wengi wa  Yesu Kristo  wanaadhimisha  kifo  chake  msalabani  ambacho kilitokea nje ya kuta za  mji  wa  Yerusalemu  siku ya  Ijumaa . Kadiri ya  Injili  ya  Mtume Yohane ,kesho yake ilikuwa  Sabato  na pia  Pasaka ,jambo lisilotokea kwa kawaida. Kwa sababu hiyo  wataalamu  mbalimbali wanakadiria ilikuwa tarehe  7 Aprili   30 . Ijumaa kuu ni sehemu ya  Juma Kuu  linaloanza kwa adhimisho la  Yesu  kuingia mji huo akishangiliwa kama  mfalme wa Wayahudi  (yaani  Masiya  au  Kristo ).Adhimisho hilo linafanyika mwanzoni mwa  wiki , yaani  Jumapili ya matawi . Ijumaa kuu ni pia sehemu ya  siku tatu kuu za Pasaka  zinazoadhimisha mateso na  kifo chake  ( Ijumaa ), kulala  kaburini  ( Jumamosi ), na hatim...

MKOANI KATAVI AMUUA MKEWE NA KUZIKA MWILI WAKE

Image
Jeshi   la   Polisi mkoani Katavi   linamshikilia mkazi   wa   Kijiji   cha   Songambele   Kata ya   Sibwesa   Tarafa ya   Karema Wilaya ya   Tanganyika   jina   lake   limehifadhiwa(45) kwa   tuhuma za kumuua mke   wake(31) kwa sababu ya wivu wa kimapenzi na   kisha mzika huku   mtoto wake mwenye   umri wa miaka tisa akishuhudia tukio. Kamanda wa   Jeshi la   Polisi wa   mkoa   wa   Katavi    Damas    Nyanda     alisema tukio   la kupatikana   kwa   mwili   wa   marehemu   huyo lilitokea juzi majira ya saa 6;00 mchana   katika Kijiji   hicho. Alisema   marehemu aliuawa   na   mumewe huyo siku ya   januari 15   kwa   kupigwa na   mumewe   kwa   kutumia silaha   zajadi ambazo ni fimbo na   mpini   wa    jembe baada ...

WATOTO WA KANISA KATOLIKI WATOA MSAADA KWA WAGONJWA HOSPITALI YA MANISPAA YA MPANDA

Image
Katika kuadhimisha Alhamisi kuu kuelekea sikukuu ya pasaka,Watoto wa shirika la mtoto yesu kutoka jumuiya mtakatifu Filomena kigango cha Kawajense Majengo Mapya jimbo katoliki la Mpanda Mkoani Katavi,wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wagonjwa waliopo katika Hospitali ya Manispaa ya Mpanda. Wakizungumza kwa niaba ya watoto wenzao Sesilia John Enock na Samweli wamesema wameamua kutoa msaada kwa wagonjwa wenye uhitaji ikiwa ni kuadhimisha Alhamisi kuu katika kuelekea sikukuu ya pasaka. Jimbo Katoliki la Mpanda Katavi(PICHA NA.Issack Gerald) Kwa upande wake Katekista Joseph Paul Kansato ambaye pia ni mwalimu wa parokia ya kanisa kuu jimbo la Mpanda amesema watoto hao wametoa misaada mbalimbali ikiwemo sabuni, mafuta na sukari kama ishara ya upendo walionao kwa watu wenye shida mbalimbali. Kwa upande wao baadhi ya wagonjwa wakiwemo Mussa Paul na Magreth Peter Ndekeja wametoa shukrani zao kwa watoto hao waliotoa msaada huo huku wakiomba jamii kuiga mfano uliooneshwa na wato...

IGP SIRRO AWAHAKIKISHIA USALAMA WATANZANIA WOTE KIPINDI CHA PASAKA

Image
Amesema Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro matukio  makubwa ya uhalifu wa kutumia Silaha yamepungua kwa kiasi kikubwa hapa nchini. IGP Sirro ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na vyombo vya habari ili kutoa salaamu za pasaka kwa watanzania ambapo amewashukuru Wananchi kwa ushirikiano wanaoendelea kuutoa kwa Jeshi la Polisi  jambo ambalo limesaidia kupunguza uhalifu kwa kiasi kikubwa hapa nchini.  Aidha amesema jitihada za kukabiliana na makosa ya usalama barabarani zinaendelea ili  kupunguza ajali zinazosababisha vifo na majeruhi kwa raia. Katika hatua nyingine amesema jeshi la Polisi katika mikoa yote linawahakikishia wananchi kuwa limejipanga kikamilifu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuhakikisha kuwa sikukuu hii inasherekewa kwa amani na utulivu na hakuna vitendo vyovyote vya uhalifu vitakavyofanyika na vitakapojitokeza vitadhibitiwa kwa haraka. Ulinzi utaimarishwa kwenye maeneo yote yakiwemo maeneo ya kuabudia,fukwe,...