Posts

MKOANI KATAVI AMUUA MKEWE NA KUZIKA MWILI WAKE

Image
Jeshi   la   Polisi mkoani Katavi   linamshikilia mkazi   wa   Kijiji   cha   Songambele   Kata ya   Sibwesa   Tarafa ya   Karema Wilaya ya   Tanganyika   jina   lake   limehifadhiwa(45) kwa   tuhuma za kumuua mke   wake(31) kwa sababu ya wivu wa kimapenzi na   kisha mzika huku   mtoto wake mwenye   umri wa miaka tisa akishuhudia tukio. Kamanda wa   Jeshi la   Polisi wa   mkoa   wa   Katavi    Damas    Nyanda     alisema tukio   la kupatikana   kwa   mwili   wa   marehemu   huyo lilitokea juzi majira ya saa 6;00 mchana   katika Kijiji   hicho. Alisema   marehemu aliuawa   na   mumewe huyo siku ya   januari 15   kwa   kupigwa na   mumewe   kwa   kutumia silaha   zajadi ambazo ni fimbo na   mpini   wa    jembe baada ...

WATOTO WA KANISA KATOLIKI WATOA MSAADA KWA WAGONJWA HOSPITALI YA MANISPAA YA MPANDA

Image
Katika kuadhimisha Alhamisi kuu kuelekea sikukuu ya pasaka,Watoto wa shirika la mtoto yesu kutoka jumuiya mtakatifu Filomena kigango cha Kawajense Majengo Mapya jimbo katoliki la Mpanda Mkoani Katavi,wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wagonjwa waliopo katika Hospitali ya Manispaa ya Mpanda. Wakizungumza kwa niaba ya watoto wenzao Sesilia John Enock na Samweli wamesema wameamua kutoa msaada kwa wagonjwa wenye uhitaji ikiwa ni kuadhimisha Alhamisi kuu katika kuelekea sikukuu ya pasaka. Jimbo Katoliki la Mpanda Katavi(PICHA NA.Issack Gerald) Kwa upande wake Katekista Joseph Paul Kansato ambaye pia ni mwalimu wa parokia ya kanisa kuu jimbo la Mpanda amesema watoto hao wametoa misaada mbalimbali ikiwemo sabuni, mafuta na sukari kama ishara ya upendo walionao kwa watu wenye shida mbalimbali. Kwa upande wao baadhi ya wagonjwa wakiwemo Mussa Paul na Magreth Peter Ndekeja wametoa shukrani zao kwa watoto hao waliotoa msaada huo huku wakiomba jamii kuiga mfano uliooneshwa na wato...

IGP SIRRO AWAHAKIKISHIA USALAMA WATANZANIA WOTE KIPINDI CHA PASAKA

Image
Amesema Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro matukio  makubwa ya uhalifu wa kutumia Silaha yamepungua kwa kiasi kikubwa hapa nchini. IGP Sirro ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na vyombo vya habari ili kutoa salaamu za pasaka kwa watanzania ambapo amewashukuru Wananchi kwa ushirikiano wanaoendelea kuutoa kwa Jeshi la Polisi  jambo ambalo limesaidia kupunguza uhalifu kwa kiasi kikubwa hapa nchini.  Aidha amesema jitihada za kukabiliana na makosa ya usalama barabarani zinaendelea ili  kupunguza ajali zinazosababisha vifo na majeruhi kwa raia. Katika hatua nyingine amesema jeshi la Polisi katika mikoa yote linawahakikishia wananchi kuwa limejipanga kikamilifu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuhakikisha kuwa sikukuu hii inasherekewa kwa amani na utulivu na hakuna vitendo vyovyote vya uhalifu vitakavyofanyika na vitakapojitokeza vitadhibitiwa kwa haraka. Ulinzi utaimarishwa kwenye maeneo yote yakiwemo maeneo ya kuabudia,fukwe,...

DKT.SHEIN AWAAPISHA MAKATIBU WAKUU

Image
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,leo amewaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni kushika nyadhifa mbalimbali katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Viongozi walioapishwa na Rais Dk.Shein katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar ni Fatma Gharib Bilal ambaye ameapishwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee, Wanawake na Watoto na Abdalla Hassan Mitawi ambaye ameapishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais. Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd,Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid,Jaji Mkuu wa Zanzibar   Omar Othman Makungu,Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said pamoja na Mawaziri. Viongozi wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih,Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji,Mkuu wa   Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud,Washauri wa Rais wa Zanzibar pamoja na viongoz...

RIPOTI YA DAKTARI KUHUSU WALIOKUFA KWA SUMU YA UYOGA KATAVI HII HAPA

Image
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Dkt. Theopister Elisa amesema uchunguzi wa kitabibu unaonesha mwanamke Mariana Gerald Sanane(47) mkazi wa kijiji cha Sitalike Wilayani Mpanda aliyefariki duniani baada ya kula uyoga unaotajwa kuwa na sumu aliathiriwa katika ini. Dkt.Theopister Elisa ameeleza hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari kueleza walichokibanini kwa mwanamke huyo baada ya kufariki kwa kula uyoga ambao unadaiwa kuchumwa kutoka zizi la ng’ombe baada ya uyoga huo kumwagiwa dawa ya kupulizia ng’ombe. Aidha Dkt.Elisa amesema waathiriwa wa sumu hiyo walicheleweshwa kufikishwa katika vituo vya huduma za afya hali iliyosababisha mathara makubwa kujitokeza mwilini mpaka kusababisha mauti baada ya idi kuathirika. Machi 25 mwaka huu Frenki Mayaga na Erizabeth George wakazi kijiji cha Sitalike wakiwa wa familia moja,walifariki dunia baada ya kula uyoga huo wenye sumu na hivyo kufikisha idadi ya watu watatu waliofariki dunia wote wakitoka katik...

HIACE YAUA MWALIMU WA SEKONDARI KATAVI

Image
Mwalimu wa shule ya sekondari ya St.Mary’s iliyopo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Hipoliti Julius Milambo amefariki dunia papo hapo baada ya kogongwa na gari aina ya hiace. (Hiyo picha haina mahusiano na habari hii) Kwa mjibu wa mashuhuda,ajali hiyo ilitokea jana majira ya jioni ambapo marehemu aligongwa katika eneo la Mpanda Hotel na gari lililokuwa likitoka kata ya Kakese ambapo aligongwa wakati akivuka barabara. Aidha wametaja gari ambalo lilimgonga mwalimu huyo kuwa ni Hiace Kwa upande wake Mganga mkuu wa Hospitali ya Manispaa ya Mpanda Dkt.Theopister Elisha akizungumza na Mpanda Radio Ofisini kwake amesema hajapata ripoti ya kifo cha mwalimu huyo. Hata hivyo kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Katavi ACP Damas Nyanda alipotafutwa kuelezea tukio hilo amedai kuwa yupo msibani. Wakati huo huo waendeshaji wa vyombo vya moto wameshauri kuwekwa matuta katika barabara inayotoka Mpanda – Kigoma   ili kupunguza ajala za mara kwa mara ambazo zimekuwa zikitokea. Habari k...

WANANCHI WALALAMIKIA UONEVU KATAVI

Wananchi wa kitongoji cha Itogolo katika kijiji cha Kampuni   kata ya misunkumilo Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wameilalamikia serikali kuwakamata,kuwatoza faini na kuwalazimisha kuvuna mazao yao kabla ya kukomaa. Wananchi hao wakiwemo Agnes John,Charles Pius na Peter Luamula wametoa malalamiko hayo katika mkutano wa hadhara wa kijiji cha Kampuni ambapo ulikuwa ukifanyika katika kitongoji hicho lengo likiwa ni kutoa nafasi kwa wananachi kueleza kero zao. Wamesema wamekuwa wakikamatwa ovyo na mgambo kisha kupelekwa mahabusu na kulipishwa faini wakati hakuna elimu ya kutambua mita sitini kutoka chanzo cha maji ya mto Mpanda iliyotolewa. Kwa upande wao wajumbe wa kamati ya watumia maji bonde la mto Mpanda Mahela Mahanda na Daudi Sumuni wamekanusha kuwaamrisha wananchi kuvuna mazao yao kabla ya kukomaa lakini wamekubali kuwakamata na kuwatoza faini kabla ya kutoa elimu kwa wananchi hao. Mwenyekiti wa kijiji cha Kampuni Bw.James Simoni amesema mpaka sasa wat...