HIACE YAUA MWALIMU WA SEKONDARI KATAVI
Mwalimu wa shule ya sekondari ya
St.Mary’s iliyopo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Hipoliti Julius Milambo
amefariki dunia papo hapo baada ya kogongwa na gari aina ya hiace.
Kwa mjibu wa mashuhuda,ajali hiyo
ilitokea jana majira ya jioni ambapo marehemu aligongwa katika eneo la Mpanda
Hotel na gari lililokuwa likitoka kata ya Kakese ambapo aligongwa wakati
akivuka barabara.
(Hiyo picha haina mahusiano na habari hii) |
Aidha wametaja gari ambalo lilimgonga
mwalimu huyo kuwa ni Hiace
Kwa upande wake Mganga mkuu wa
Hospitali ya Manispaa ya Mpanda Dkt.Theopister Elisha akizungumza na Mpanda
Radio Ofisini kwake amesema hajapata ripoti ya kifo cha mwalimu huyo.
Hata hivyo kamanda wa jeshi la polisi
Mkoani Katavi ACP Damas Nyanda alipotafutwa kuelezea tukio hilo amedai kuwa
yupo msibani.
Wakati huo huo waendeshaji wa vyombo
vya moto wameshauri kuwekwa matuta katika barabara inayotoka Mpanda – Kigoma ili kupunguza ajala za mara kwa mara ambazo
zimekuwa zikitokea.
Comments