WAKURUGENZI WATATU WATUMBULIWA WAWILI WA KIGOMA
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amewasimamisha kazi wakurugenzi wawili kati
ya watatu wa Halmashauri za Pangani na Kigoma baada ya kupata hati chafu katika
matokeo ya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka
2016/17.
Ripoti hiyo iliyowasilishwa leo Machi
27, 2018 inaonyesha halmashauri 166
kupata hati safi,16 hati zenye shaka na halmashauri tatu kupata hati
chafu.
Halmashauri zilizopata hati chafu ni
Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji na Halmashauri ya Kigoma na Pangani.
Waziri Jafo amesema baada ya
kuwasimamisha,amemwagiza katibu mkuu wa wizara hiyo kuunda timu ya watalaamu
kuchunguza hati hizo na kutoa matokeo ndani ya wiki tatu.
Amesema wakurugenzi waliohusika
katika hati chafu ni Daud Mlahagwa (Pangani),aliyekuwa Mkurugenzi wa Kigoma
Ujiji, Judethadeus Mboya ambaye amestaafu kwa sasa na Mkurugenzi wa halmashauri
ya Kigoma Hanji Godigodi na Damian Chambasi wa Pangani.
Amesema taarifa itakayopatikana
itabainisha kiwango cha uchafu huo na Serikali itachukua hatua nyingine za
kisheria kadri uchunguzi utakavyoelekeza.
Aidha amewataka wakurugenzi katika
halmashauri zilizofanya vizuri katika ukaguzi huo,waendelee kutekeleza na
majukumu yao na kutoa majibu ya hoja zote zilizobainishwa na ripoti ya CAG.
Amesema Serikali imeanza kufanya
vizuri katika ukaguzi huo baada ya kufikia asilimia 90 na matumaini yaliyopo ni
kuondokana na taarifa ya hati chafu ili kuhakikisha fedha za Serikali
zinatumika kwa maendeleo ya wananchi.
Habari kamili ni WWW.P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments