Posts

HIACE YAUA MWALIMU WA SEKONDARI KATAVI

Image
Mwalimu wa shule ya sekondari ya St.Mary’s iliyopo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Hipoliti Julius Milambo amefariki dunia papo hapo baada ya kogongwa na gari aina ya hiace. (Hiyo picha haina mahusiano na habari hii) Kwa mjibu wa mashuhuda,ajali hiyo ilitokea jana majira ya jioni ambapo marehemu aligongwa katika eneo la Mpanda Hotel na gari lililokuwa likitoka kata ya Kakese ambapo aligongwa wakati akivuka barabara. Aidha wametaja gari ambalo lilimgonga mwalimu huyo kuwa ni Hiace Kwa upande wake Mganga mkuu wa Hospitali ya Manispaa ya Mpanda Dkt.Theopister Elisha akizungumza na Mpanda Radio Ofisini kwake amesema hajapata ripoti ya kifo cha mwalimu huyo. Hata hivyo kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Katavi ACP Damas Nyanda alipotafutwa kuelezea tukio hilo amedai kuwa yupo msibani. Wakati huo huo waendeshaji wa vyombo vya moto wameshauri kuwekwa matuta katika barabara inayotoka Mpanda – Kigoma   ili kupunguza ajala za mara kwa mara ambazo zimekuwa zikitokea. Habari k...

WANANCHI WALALAMIKIA UONEVU KATAVI

Wananchi wa kitongoji cha Itogolo katika kijiji cha Kampuni   kata ya misunkumilo Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wameilalamikia serikali kuwakamata,kuwatoza faini na kuwalazimisha kuvuna mazao yao kabla ya kukomaa. Wananchi hao wakiwemo Agnes John,Charles Pius na Peter Luamula wametoa malalamiko hayo katika mkutano wa hadhara wa kijiji cha Kampuni ambapo ulikuwa ukifanyika katika kitongoji hicho lengo likiwa ni kutoa nafasi kwa wananachi kueleza kero zao. Wamesema wamekuwa wakikamatwa ovyo na mgambo kisha kupelekwa mahabusu na kulipishwa faini wakati hakuna elimu ya kutambua mita sitini kutoka chanzo cha maji ya mto Mpanda iliyotolewa. Kwa upande wao wajumbe wa kamati ya watumia maji bonde la mto Mpanda Mahela Mahanda na Daudi Sumuni wamekanusha kuwaamrisha wananchi kuvuna mazao yao kabla ya kukomaa lakini wamekubali kuwakamata na kuwatoza faini kabla ya kutoa elimu kwa wananchi hao. Mwenyekiti wa kijiji cha Kampuni Bw.James Simoni amesema mpaka sasa wat...

WAKURUGENZI WATATU WATUMBULIWA WAWILI WA KIGOMA

Image
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo   amewasimamisha kazi wakurugenzi wawili kati ya watatu wa Halmashauri za Pangani na Kigoma baada ya kupata hati chafu katika matokeo ya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2016/17. Ripoti hiyo iliyowasilishwa leo Machi 27, 2018 inaonyesha halmashauri 166   kupata hati safi,16 hati zenye shaka na halmashauri tatu kupata hati chafu. Umauzi huo unafanyika ikiwa ni dakika chache baada ya Rais John Magufuli kutoa agizo hilo. Halmashauri zilizopata hati chafu ni Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji na Halmashauri ya Kigoma na Pangani. Waziri Jafo amesema baada ya kuwasimamisha,amemwagiza katibu mkuu wa wizara hiyo kuunda timu ya watalaamu kuchunguza hati hizo na kutoa matokeo ndani ya wiki tatu. Amesema wakurugenzi waliohusika katika hati chafu ni Daud Mlahagwa (Pangani),aliyekuwa Mkurugenzi wa Kigoma Ujiji, Judethadeus Mboya ambaye amestaafu kwa...

MKUU WA SHULE AJINYONGA OFISINI KWAKE AKIMTAJA MKURUGENZI

Image
MKUU wa Shule ya Sekondari Kakonko wilayani Kakonko mkoani Kigoma,Peter Rubonya amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kamba ofisini kwake mapema leo asubuhi. Akielezea tukio hilo,Mwalim wa zamu wa shule hiyo Isaac Japhet amesema yeye alifika shuleni hapo saa 12:30 asubuhi ili kuwafundisha wanafunzi wa kidato cha nne masomo ya ziada baada ya kufunga shule wiki iliyopita na baada ya kufika aligundua kuwa hana chaki ambapo mkuu huyo wa shule alimpatia chaki mlinzi ili awape wananfunzi. Amesema baada ya muda,Mratibu elimu kata pamoja na mmoja wa wazazi walifika ofisini hapo wakiwa na shida na mkuu wa shule na baada ya kuelezwa yupo ndani ofisini lakini baada ya kugonga mlango hawakuweza kujibiwa na ndipo wakaamua kufungua mlango na kukuta mwili wa marehemu ukining’inia dalini. Mwalim Isaac amesema Mwalimu aliyejinyonga alikuwa akifundisha masomo ya Kemia na Fizikia shuleni hapo hawakuwahi kusikia mgogoro wowote wa kifamilia au kijamii na mkewe ambaye ni mkufunzi katika Chuo Kiku...

UYOGA WAUA MWINGINE KATAVI

Image
Mtu mwingine mkazi wa kijiji cha Sitalike wilayani Mpanda Mkoani Katavi amefariki dunia akiwa hospitali ya Manispaa ya Mpanda akipatiwa matibabu na hivyo kufikisha idadi ya watu watatu waliofariki kutokana na kula uyoga unaosadikiwa kuwa na sumu. Mwenyekiti wa kijiji cha Sitalike Bw.Christopher   Anjero amemtaja mwanamke aliyefariki leo kuwa ni Mariana Gerald Sanane ambaye ni Mama wa marehemu wawili waliofariki siku ya jana. Waliofariki jana kutokana na kula uyoga huo ni Frenki Mayaga   ambaye alifariki akipatiwa huduma ya kwanza katika kijiji cha Stalike huku   Erizabeth George ambaye alikimbizwa hospitali ya Manispaa ya Mpanda akiaga dunia baada ya kufikishwa katika mlango wa Daktari. Mganga wa zamu wa hospitali ya Manispaa ya Mpanda ambaye alitakiwa kueleza zaidi kuhusu suala hilo amekana kuzungumza kwa madai ya kutokuwa msemaji kwa sasa. Kisa hicho   ambacho kimeacha simanzi kwa jamii kutokana na vifo vya watu watatu wa familia moja kinatajwa kuwa ni k...

RAIS MAGUFULI APOKEA NA KUZINDUA MAGARI 181 YA MSD,MIKOA MIPYA YATAJWA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Magufuli amesema serikali inaendelea kupanga   mikakati yake kuhakikisha inakarabati na kujenga vituo na Hospitali zinazotoa huduma za afya nchini ikiwemo mikoa mipya ya Katavi,Songwe,Geita,Simiyu na Njombe. Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo katika hafla fupi ya ugawaji wa magari 181 ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwa ajili ya kusambaza dawa maeneo mbalimbali nchini,uzinduzi ambao umefanyika eneo la Keko jijini Dar es Salaam. Aidha Rais Magufuli mbali na kuwashukuru Global Fund kwa msaada wa magari 181 yasiyokuwa na   masharti amesema yatarahisisha huduma mbalimbali katika maeneo ya Tanzania katika sekta ya afya. Awali Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya dawa Nchini MSD Laurean Rugambwa Bwanakunu,amesema magari ya bohari ya dawa MSD sasa yatakuwa 213 kutoka magari 32 yaliyokuwepo ambapo magari hayo ya Land Cruiser 104,Malori 77 ambayo kwa ujumla yamegarimu shilingi Bilioni 20.75. Kwa upande wake Leindan Moris mwakailishi wa Gl...

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

Image
Jokate Mwegelo Jokate Mwegelo Amezaliwa Jokate Urban Mwegelo 20 Machi   1987   (umri 31) 20 Machi   1987   (umri 31) Utaifa MTanzania Mhitimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ( Shahada ya Sayansi ya Siasa ) Kazi yake Mwigizaji, mjasiriamali, mtangazaji, mwimbaji Miaka ya kazi 2006-hadi sasa Jokate Mwegelo  ni  mwigizaji  wa  filamu  na mjasiriamali kutoka nchini  Tanzania . Jokate vilevile ni mtangazaji na mwimbaji. Huyu ni  Afisa Mtendaji Mkuu  wa kampuni ya  Kidoti Company .Mwaka wa 2011,alishinda tuzo ya  Zanzibar International Film Festival  akiwa kama mwigizaji bora filamu wa kike.Mwaka wa 2017,Mwegelo aliingizwa katika jarida la Forbes katika  Forbes 30 Under 30  kutoka Afrika. MAISHA YA AWALI NA ELIMU. Mwegelo alizaliwa mnamo tarehe 20 Machi,1987 huko mjini  Washington D.C ambapo wakat...