Posts

MKUU WA SHULE AJINYONGA OFISINI KWAKE AKIMTAJA MKURUGENZI

Image
MKUU wa Shule ya Sekondari Kakonko wilayani Kakonko mkoani Kigoma,Peter Rubonya amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kamba ofisini kwake mapema leo asubuhi. Akielezea tukio hilo,Mwalim wa zamu wa shule hiyo Isaac Japhet amesema yeye alifika shuleni hapo saa 12:30 asubuhi ili kuwafundisha wanafunzi wa kidato cha nne masomo ya ziada baada ya kufunga shule wiki iliyopita na baada ya kufika aligundua kuwa hana chaki ambapo mkuu huyo wa shule alimpatia chaki mlinzi ili awape wananfunzi. Amesema baada ya muda,Mratibu elimu kata pamoja na mmoja wa wazazi walifika ofisini hapo wakiwa na shida na mkuu wa shule na baada ya kuelezwa yupo ndani ofisini lakini baada ya kugonga mlango hawakuweza kujibiwa na ndipo wakaamua kufungua mlango na kukuta mwili wa marehemu ukining’inia dalini. Mwalim Isaac amesema Mwalimu aliyejinyonga alikuwa akifundisha masomo ya Kemia na Fizikia shuleni hapo hawakuwahi kusikia mgogoro wowote wa kifamilia au kijamii na mkewe ambaye ni mkufunzi katika Chuo Kiku...

UYOGA WAUA MWINGINE KATAVI

Image
Mtu mwingine mkazi wa kijiji cha Sitalike wilayani Mpanda Mkoani Katavi amefariki dunia akiwa hospitali ya Manispaa ya Mpanda akipatiwa matibabu na hivyo kufikisha idadi ya watu watatu waliofariki kutokana na kula uyoga unaosadikiwa kuwa na sumu. Mwenyekiti wa kijiji cha Sitalike Bw.Christopher   Anjero amemtaja mwanamke aliyefariki leo kuwa ni Mariana Gerald Sanane ambaye ni Mama wa marehemu wawili waliofariki siku ya jana. Waliofariki jana kutokana na kula uyoga huo ni Frenki Mayaga   ambaye alifariki akipatiwa huduma ya kwanza katika kijiji cha Stalike huku   Erizabeth George ambaye alikimbizwa hospitali ya Manispaa ya Mpanda akiaga dunia baada ya kufikishwa katika mlango wa Daktari. Mganga wa zamu wa hospitali ya Manispaa ya Mpanda ambaye alitakiwa kueleza zaidi kuhusu suala hilo amekana kuzungumza kwa madai ya kutokuwa msemaji kwa sasa. Kisa hicho   ambacho kimeacha simanzi kwa jamii kutokana na vifo vya watu watatu wa familia moja kinatajwa kuwa ni k...

RAIS MAGUFULI APOKEA NA KUZINDUA MAGARI 181 YA MSD,MIKOA MIPYA YATAJWA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Magufuli amesema serikali inaendelea kupanga   mikakati yake kuhakikisha inakarabati na kujenga vituo na Hospitali zinazotoa huduma za afya nchini ikiwemo mikoa mipya ya Katavi,Songwe,Geita,Simiyu na Njombe. Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo katika hafla fupi ya ugawaji wa magari 181 ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwa ajili ya kusambaza dawa maeneo mbalimbali nchini,uzinduzi ambao umefanyika eneo la Keko jijini Dar es Salaam. Aidha Rais Magufuli mbali na kuwashukuru Global Fund kwa msaada wa magari 181 yasiyokuwa na   masharti amesema yatarahisisha huduma mbalimbali katika maeneo ya Tanzania katika sekta ya afya. Awali Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya dawa Nchini MSD Laurean Rugambwa Bwanakunu,amesema magari ya bohari ya dawa MSD sasa yatakuwa 213 kutoka magari 32 yaliyokuwepo ambapo magari hayo ya Land Cruiser 104,Malori 77 ambayo kwa ujumla yamegarimu shilingi Bilioni 20.75. Kwa upande wake Leindan Moris mwakailishi wa Gl...

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

Image
Jokate Mwegelo Jokate Mwegelo Amezaliwa Jokate Urban Mwegelo 20 Machi   1987   (umri 31) 20 Machi   1987   (umri 31) Utaifa MTanzania Mhitimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ( Shahada ya Sayansi ya Siasa ) Kazi yake Mwigizaji, mjasiriamali, mtangazaji, mwimbaji Miaka ya kazi 2006-hadi sasa Jokate Mwegelo  ni  mwigizaji  wa  filamu  na mjasiriamali kutoka nchini  Tanzania . Jokate vilevile ni mtangazaji na mwimbaji. Huyu ni  Afisa Mtendaji Mkuu  wa kampuni ya  Kidoti Company .Mwaka wa 2011,alishinda tuzo ya  Zanzibar International Film Festival  akiwa kama mwigizaji bora filamu wa kike.Mwaka wa 2017,Mwegelo aliingizwa katika jarida la Forbes katika  Forbes 30 Under 30  kutoka Afrika. MAISHA YA AWALI NA ELIMU. Mwegelo alizaliwa mnamo tarehe 20 Machi,1987 huko mjini  Washington D.C ambapo wakat...

JOKATE ATUMBULIWA UVCCM

Image
Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa CCM iliyokutana kwa dharura mchana huu chini ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Kheir Denis Jemes imetengua uteuzi wa Kaimu Katibu wa Hamasa na Chipukizi UVCCM Taifa Jokate  U. Mwengelo kuanzia leo. Taarifa hiyo iliyotolewa kupitia mtandao wa twitter wa UVCCM imesema kuwa Jokate Mwegelo ametenguliwa katika nafasi hiyo ambapo amehudumu katika nafasi hiyo kwa takribani miezi 11 toka amelipoteuliwa April 2017.  Kikao hicho kilichomtengua Jokate kiliendeshwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Ndg.  Kheri Denis James (MCC) katika ukumbi wa secretariet  White house Mjini Dodoma lakini bado hawajaweka wazi sababu zilizopelekea kutengua uteuzi wa Jokate Mwegelo.  Jokate Mwegelo Amezaliwa Jokate Urban Mwegelo 20 Machi   1987   (umri 31) Utaifa MTanzania Mhitimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ( Shahada ya Sayan...

RAIS MAGUFULI KUPOKEA MAGARI 181 YA KUSAMBAZIA DAWA NCHINI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kupokea magari 181 yatakayokuwa yakitumika kusambaza madawa vijijini na mjini. Kwa mjibu wa taarifa ya Msemaji Mkuu wa Serikali,Dkt. Hassan Abbas Rais Magufuli ndiye atakuwa mgeni rasmi na kuzindua magari hayo 181. Magari hayo yapo chini ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na yataongeza ufanisi katika kufikisha huduma katika maeneo yaliyokuwa hayafikiwi. Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

UYOGA WAUA WAWILI KATAVI NA WENGINE MAHUTUTI

Image
Watu wawili ambao wametambulika kwa majina Frenki Mayaga na Erizabeth George wakazi wa kijiji cha   Stalike wilayani Mpanda mkoani Katavi,wafamefariki dunia baada ya kula uyoga unaotajwa kuwa na Sumu. Mwenyekiti wa Kijiji hicho Christopher   Anjero amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo leo ambapo amesema mbali na marehemu hao,watu wengine watatu wako mahututi na wanaendelea na matibabu katika hospitali ya wilaya ya Mpanda. Bi.Monica George ambaye ni miongoni mwa ndugu wa marehemu amesema walikwenda porini kutafuta uyoga ambapo baada ya kupika na kula ndiyo wakapatwa na mauti hayo. Aidha George Anjero Mrisho amesema alipokea taarifa za kifo cha kijana wake Frenki Mayaga akiwa shambani. Hata hivyo Mganga wa zamu wa hospitali ya Manispaa ya Mpanda hakuupatikana ili kujua taratibu za kitabibu zinazoendelea kwa sababu hakuwepo kituoni. Kwa mjibu wa mwenyekiti wa kijiji cha Sitalike Bw. Christopher   Anjero hilo ni tukio la kwanza katika kipindi cha miaka 10 iliyopit...