Posts

VYUO 163 TANZANIA VYAFUNGIWA UDAHILI

Image
Baraza la Taifa la Elimu na Ufundi (Nacte) limezuia vyuo 163 kudahili wanafunzi katika kozi mbalimbali ngazi ya astashahada na shahada,baada ya kukutwa na upungufu ikiwako kutokuwa na walimu wenye sifa. Akizungumza leo,Machi 23 na waandishi wa habari, Mkuu wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Nacte,DK Annastella Sigwejo amesema walifanya uhakiki kwa vyuo 459,kati ya hivyo 296 ndivyo vimekidhi vigezo vya kutoa elimu kwa kiwango kinachotakiwa. "Kutokana na hali hiyo hivyo ndivyo vinaruhusiwa kudahili wanafunzi kwa ajili ya kozi mbalimbali ngazi ya astashahada na stashahada kwa muhula wa udahili wa Machi na Aprili mwaka huu.” Amesema licha ya kwamba vyuo vilivyosajiliwa viko 580 waliamua kujiridhisha kwa kuvifanyia uhakiki ambapo walifanikiwa kuhakiki vyuo 459. Nacte wanawashauri wanafunzi kuhakikisha wanajiridhisha kuwa wanaomba kujiunga kwenye vyuo vilivyokidhi vigezo. Mkuu wa Kitengo cha Udahili, Twaha Twaha amesema kuwa majina ya vyuo vilivyoruhusiwa kudahili yamewekwa kwen...

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA BILL GATES FOUNDATION

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Bill & Melinda Gates Foundation Bw.Rodger Voorhies.

WAVUVI RUKWA WAIPONGEZA ZAMBIA KUONDOA ZUIO BIASHARA YA SAMAKI

Image
WAVUVI wa samaki katika ziwa Tanganyika wilayani Kalambo mkoani Rukwa wameishukuru serikali ya Zambia kwa kuondoa marufuku ya biashara ya samaki katika nchi hiyo. Marufuku hiyo ilikuwa imewekwa kwa takribani wiki mbili zilizopita kutokana na kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa kipindu pindu nchini humo.

WANAFUNZI WAKUMBWA UGONJWA WA AJABU

Image
WANAFUNZI wa kike katika Shule ya Msingi Kabwe  mwambao mwa Ziwa Tanganyika  wilayani Nkasi mkoani Rukwa,wanaugua ugonjwa wa ajabu unaosababisha wapige kelele hovyo,kutetemeka na kisha kuanguka. Mkuu wa Shule hiyo,Amon Kawana alisema ugonjwa huo ulianza kutokea shuleni hapo tangu mwishoni mwa mwaka jana ambapo mpaka sasa ni wanafunzi wapatao 20 wa kike wameshakumbwa na ugonjwa huo na kusababisha taharuki  shuleni hapo.

RAIS MAGUFULI AFYANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA ULINZI WA ISRAEL IKULU

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Ulinzi wa Israel Mhe.Avigdor Lieberman Ikulu Jijini Dar es Salaam. Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt.Hussein Ali Mwinyi,Balozi wa Israel hapa nchini Mhe.Noah Gal Gendler,viongozi wakuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Polisi.

WATU WAWILI MIKONONI MWA POLISI KATAVI KWA KUHAMASISHA MAANDAMANO

Image
Na.Issack Gerald-Katavi Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi ACP Damas Nyanda amesema jeshi hilo linawshikilia watu wawili wakituhumiwa kuhamasisha maandamano kwa njia ya Mtandaoni. Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi ACP Damas Nyanda Kamnada Nyanda ametoa kauli wakati akizungumza na mtandao huu Ofisini kwake kuhusu namna ambavyo jeshi hilo limejipanga kudhibiti maandamano hayo. Aidha Kamanda Nyanda ametoa onyo kali kwa watu watakaohamasisha au kuandamana ambapo amesema watakaoandamana watakabiliwa na hatua kali za kisheria. Baadhi ya wananchi Mkoani Katavi wakiwemo Said Rashid Mdemela,Juma Bairon Mwanda,Jonathan John Midende,Paul Makelele na Wenseslaus Obed wamesema maandamano hayo hayana tija kwa watanzania na hawatashiriki kwa sababu ni wakati wa kufanya kazi za maendeleo na kuepuka mkono wa sheria kwa mambo yasiyokuwa na maana. ‘ ’Majina ya watuhumiwa hayakuwekwa wazi kwa sababu za kiuchunguzi na upelelezi utakapokamilika wanatarajiwa kufikishwa mahakamani ...

SERIKALI YATOA TAHADHARI UGONJWA HATARI WA DENGUE

Image
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu amewashauri wananchi kwenda vituo vya tiba haraka mara baada ya kugundua kuwa wana dalili za ugonjwa wa dengue. Mhe.Ummy Mwalimu Hayo ameyasema wakati alipotoa tamko juu ya kuingia kwa ugonjwa wa dengue hapa nchini mara baada ya kufunga Mkutano wa 65 wa Jumuiya ya Mawaziri wa Afya wa Nchi za Afrika Mashariki,Kati na Kusini ECSA leo jijini Dar es salaam. “Kuna dalili za Ugonjwa Dengue zikiwemo homa ya ghafla,kuumwa kichwa hususan sehemu za macho, maumivu ya viungo na uchovu.Dalili hizi huanza kujitokeza kati ya siku 3 hadi 14 tangu mtu alipoambukizwa virusi vya homa ya Dengue hivyo.Wizara inashauri wananchi wasiwe na hofu,bali mara tu wanapoona dalili za ugonjwa waende katika vituo vya tiba"amesema Waziri Ummy. Aidha Waziri Ummy amesema wakati mwingine dalili za ugonjwa huo zinaweza kufanana sana na dalili za malaria hivyo wananchi wanaaswa kwamba,wakipata homa wahakikishe wanapima ili kugundua k...