Posts

TRA YATUMBUA WAFANYAKAZI WAWILI

Image
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewasimamisha kazi watumishi wake wawili mkoani Lindi,kwa kile kilichodaiwa kwenda kinyume na kanuni na miongozo ya kazi inavyowaelekeza na kutumia lugha isiyo rafiki na wateja wao {wafanyabiashara}. Uamuzi huo,umechukuliwa na Kamishina kodi ya Mapato za ndani nchini,Elijah Mwandumbya,wakati wa kikao cha pamoja kati yake na wafanyabiashara wa mkoa huo kilichofanyika Manispaa ya Lindi baada ya kusikiliza malalamiko mbalimbali kutoka kwa wafanyabiashara hao. Mwandumbya amesema Taifa wamekuwa wakipata taarifa kwamba hakuna mahusiano mazuri kati watumishi hao na wafanyabiashara,hali iliyohustua uongozi na kumtuma Kamishina huyo kufika mkoani humo kupata maelezo ya kina. Kamishina huyo wa kodi za ndani amesema {TRA} inapitia kipindi ambacho kinahitaji kuwapatia huduma bora wateja wao ili waweze kumsaidia Rais wa nchi katika utekelezaji wake wa maendeleo kwa kuhakikisha wanazingatia Sheria,kanuni,taratibu na miongozo,kuhakikisha wanatoa huduma ili...

MH.MKAPA AIBUKIA SEKTA YA ELIMU ATAKA MJADALA KITAIFA

Image
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mh.Benjamini William Mkapa ametaka kuitishwa mjadala wa kitaifa wa kujadili hali ya elimu nchini kufuatia shule za serikali kuendelea kufanya vibaya katika matokeo ya mitihani ya kitaifa. Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mh.Benjamini William  Mkapa ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma amesema hayo mkoani Dodoma wakati wa tukio la kumuingiza kazini Makamu Mkuu mpya wa chuo kikuu hicho cha Dodoma Profesa Egid Mubofu. Katika tukio hilo wamemuaga Makamu Mkuu wa chuo hicho aliyemaliza muda wake Profesa Idrisa Kikula. Mhe.Mkapa amesema mjadala huo unatakiwa kuhusisha makundi yote ya jamii bila kujali kama ni ya sekta binafsi au ya umma sambamba na watu wa kawaida siyo wasomi pekee ambapo kupitia njia hiyo anaamini suluhu ya kudumu itapatikana. Habari zaidi ni P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

MWENYEKITI JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA ABWAGA MANYANGA

Image
Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF) Bw.Theophil Makunga amejiuzulu nafasi hiyo. Taarifa ya kujizulu kwa Bw.Makungu imetolewa leo katika vyombo vya habari na Jukwaa la   wahariri   Tanzania (TEF) na kueleza kuwa mwenyekiti huyo amejiuzulu tangu jana. Kwa mjibu wa TEF,Bw.Makungu amechukua hatua hiyo kwa kutumia uhuru wake binafsi kama mwanachama hai ambapo mkutano wa dharura umefanyika leo na kuridhia kujiuzulu kwake. Pamoja na jukwaa kusema litakosa busara za Bw.Makungu katika taaluma ya habari pia limemtakia kila la heri katika majukumu yake mengine. Habari zaidi ni P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

TANZANIA YATAKIWA KUUNGA MKONO MGOGORO WA URUSI NA UINGEREZA

Image
Serikali ya Uingereza imeitaka Tanzania na Jumuiya ya Kimataifa kuiunga mkono katika kupinga kitendo cha Urusi kutumia sumu aina ya novichok katika jaribio la kumuua jasusi wa Kirusi Sergei Skripal na binti yake Yulia. Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana, Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke alisema nchi yake haitavumilia majaribio yoyote ya mauaji ya watu wasio na hatia ndani ya ardhi yake. Cooke alisisitiza kuwa ni wazi Urusi ilihusika katika jaribio hilo na walipewa nafasi ya kueleza kwa nini waliamua kutumia sumu hiyo ndani ya Uingereza licha ya kwamba matumizi ya kemikali kama silaha ni kinyume cha sheria za kimataifa. Hata hivyo,alisema mpaka sasa hawajatoa maelezo kuhusu suala hilo. Alipoulizwa kuhusu msimamo wa Tanzania kuhusu suala hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje,Dk Susan Kolimba alisema hawezi kulizungumzia kwa sasa ambapo hata Waziri wa Mambo ya Nje,Dk Augustine Mahiga hakupatikana ili kuzungumzia suala hilo . Mpaka sasa Uingereza ...

SERIKALI YAKANUSHA SUKARI YA ZANZIBAR KUZUIWA KUUZWATANZANIA BARA

Image
Serikali imekanusha taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba imekizuia Kiwanda cha Sukari Zanzibar,ZSFL kuuza Sukari yake Tanzania Bara. Msemaji Mkuu wa Serikali Dk.Hassan Abbas Akizungumza jana jijini Arusha,Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Dk.Hassan Abbas amesema, kiwanda hicho kinapaswa kukidhi soko la Zanzibar la tani elfu 10 badala ya kulalamika kimezuiwa kuuza Sukari nje. Dk.Abbas amesema mahitaji ya kawaida Zanzibar ya sukari ni Tani elfu 17 mpaka elfu 20 kwa mwaka lakini kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha tani elfu 10 japo kwa sasa uzalishaji umeshuka hadi tani elfu 8 hivyo kufanya Zanzibar kuwa na upungufu wa tani elfu 9 hadi elfu 12. Mapema wiki hii,Kaimu Mkurugenzi Mkuu Kiwanda hicho cha Sukari Zanzibar,Bi. Fatma Salum Ali,alisema kiwanda hicho kinapata hasara ya zaidi ya shilingi laki tatu kwa kila tani moja ya Sukari inayozalishwa kutokana na kushindwa kupata kibali cha kuuza Sukari Tanzania Bara...

WALIMU 16 WAFUTWA KAZINI

Image
JUMLA ya walimu 16 wamefukuzwa kazi wilayani Nkasi mkoani Rukwa kwa kipindi cha miaka mitatu na wengine 11 wamepewa onyo kali baada ya kubainika wametenda makosa mbalimbali. Hatua hiyo imethibitishwa jana na Katibu wa tume ya utumishi wa walimu TSC wilayani humo  Richard Katyega mbele ya kamishina wa tume ya Utumishi wa walimu Taifa,Samwel Koroso ambapo alisema  kuwa katika kipindi hicho  walipokea mashauri 23 na kupelekea walimu 16 kufukuzwa kazi,11 kupewa onyo kali na wengine 5 waliondolewa kazini baada ya kubainika kuwa na vyeti bandia. Alisema katika mwaka wa fedha wa 2016,2017 na 2018  tume hiyo imesikiliza mashauri hayo na kuyatolea maamuzi ambapo ilifikia maamuzi hayo baada ya kusikiliza mashauri hayo na pasipo kumuonea mwalimu hata mmoja na kutenda haki kwa mujibu wa sheria. Katyega alisema tume hiyo sambamba na kuchukua maamuzi hayo pia imekua ikiwahamasisha walimu kufuata maadili ya ualimu kwa uhakika ili wasiweze kukumbana na adhabu mbal...

MWENYEKITI WA BAJAJI MANISPAA YA MPANDA ANG’ATUKA

Image
Mwenyekiti wa Chama cha madereva pikipiki za tairi tatu maarufu bajaji halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Bw.Rashid Rashid ametangaza kujiuzuru nafasi hiyo. Katika taarifa yake ambayo ameitoa leo Bw.Rashid amesema, miongoni mwa sababu za kujiuzulu kwake ni pamoja na kukosa ushirikiano kutoka kwa madereva wenzake,ukosefu wa ushirikiano kwa kamati yake na kutotekelezwa kwa mipango mbalimbali wanayoipanga kama chama. Aidha amesema changamoto iliyopo kwa sasa ni mgawanyiko wa wamiliki bajaji upande wa watumishi wa serikali kutozingatia kanuni na taratibu za umiliki wa chombo hicho cha usafiri. Kwa upande wa wamiliki binafsi na madereva wao amesema wamekuwa wakikumbwa na mikasa ya kupelekwa kituo cha polisi pamoja na kulipishwa faini mara kwa mara bila utaratibu. Hata hivyo Bw.Rashid amekanusha kula njama na Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu Sumtra kuwatoza madereva bajaji mpaka kiasi cha shilingi 40,000 kwa ajili ya kujinufaisha. Mapema mwaka h...