TRA YATUMBUA WAFANYAKAZI WAWILI
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewasimamisha kazi watumishi wake wawili mkoani Lindi,kwa kile kilichodaiwa kwenda kinyume na kanuni na miongozo ya kazi inavyowaelekeza na kutumia lugha isiyo rafiki na wateja wao {wafanyabiashara}.
Uamuzi huo,umechukuliwa na Kamishina kodi ya Mapato za ndani
nchini,Elijah Mwandumbya,wakati wa kikao cha pamoja kati yake na
wafanyabiashara wa mkoa huo kilichofanyika Manispaa ya Lindi baada ya
kusikiliza malalamiko mbalimbali kutoka kwa wafanyabiashara hao.
Mwandumbya amesema Taifa wamekuwa wakipata taarifa kwamba hakuna
mahusiano mazuri kati watumishi hao na wafanyabiashara,hali iliyohustua uongozi
na kumtuma Kamishina huyo kufika mkoani humo kupata maelezo ya kina.
Kamishina huyo
wa kodi za ndani amesema {TRA} inapitia kipindi ambacho kinahitaji kuwapatia
huduma bora wateja wao ili waweze kumsaidia Rais wa nchi katika utekelezaji
wake wa maendeleo kwa kuhakikisha wanazingatia Sheria,kanuni,taratibu na miongozo,kuhakikisha
wanatoa huduma iliyo bora kwa walipa kodi.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments