MH.MKAPA AIBUKIA SEKTA YA ELIMU ATAKA MJADALA KITAIFA
Rais
Mstaafu wa awamu ya tatu Mh.Benjamini William Mkapa ametaka kuitishwa mjadala
wa kitaifa wa kujadili hali ya elimu nchini kufuatia shule za serikali
kuendelea kufanya vibaya katika matokeo ya mitihani ya kitaifa.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mh.Benjamini William |
Mkapa
ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma amesema hayo mkoani Dodoma wakati
wa tukio la kumuingiza kazini Makamu Mkuu mpya wa chuo kikuu hicho cha Dodoma
Profesa Egid Mubofu.
Katika
tukio hilo wamemuaga Makamu Mkuu wa chuo hicho aliyemaliza muda wake Profesa
Idrisa Kikula.
Mhe.Mkapa amesema mjadala
huo unatakiwa kuhusisha makundi yote ya jamii bila kujali kama ni ya sekta
binafsi au ya umma sambamba na watu wa kawaida siyo wasomi pekee ambapo kupitia
njia hiyo anaamini suluhu ya kudumu itapatikana.
Habari zaidi ni
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments