Posts

MWENYEKITI JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA ABWAGA MANYANGA

Image
Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF) Bw.Theophil Makunga amejiuzulu nafasi hiyo. Taarifa ya kujizulu kwa Bw.Makungu imetolewa leo katika vyombo vya habari na Jukwaa la   wahariri   Tanzania (TEF) na kueleza kuwa mwenyekiti huyo amejiuzulu tangu jana. Kwa mjibu wa TEF,Bw.Makungu amechukua hatua hiyo kwa kutumia uhuru wake binafsi kama mwanachama hai ambapo mkutano wa dharura umefanyika leo na kuridhia kujiuzulu kwake. Pamoja na jukwaa kusema litakosa busara za Bw.Makungu katika taaluma ya habari pia limemtakia kila la heri katika majukumu yake mengine. Habari zaidi ni P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

TANZANIA YATAKIWA KUUNGA MKONO MGOGORO WA URUSI NA UINGEREZA

Image
Serikali ya Uingereza imeitaka Tanzania na Jumuiya ya Kimataifa kuiunga mkono katika kupinga kitendo cha Urusi kutumia sumu aina ya novichok katika jaribio la kumuua jasusi wa Kirusi Sergei Skripal na binti yake Yulia. Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana, Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke alisema nchi yake haitavumilia majaribio yoyote ya mauaji ya watu wasio na hatia ndani ya ardhi yake. Cooke alisisitiza kuwa ni wazi Urusi ilihusika katika jaribio hilo na walipewa nafasi ya kueleza kwa nini waliamua kutumia sumu hiyo ndani ya Uingereza licha ya kwamba matumizi ya kemikali kama silaha ni kinyume cha sheria za kimataifa. Hata hivyo,alisema mpaka sasa hawajatoa maelezo kuhusu suala hilo. Alipoulizwa kuhusu msimamo wa Tanzania kuhusu suala hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje,Dk Susan Kolimba alisema hawezi kulizungumzia kwa sasa ambapo hata Waziri wa Mambo ya Nje,Dk Augustine Mahiga hakupatikana ili kuzungumzia suala hilo . Mpaka sasa Uingereza ...

SERIKALI YAKANUSHA SUKARI YA ZANZIBAR KUZUIWA KUUZWATANZANIA BARA

Image
Serikali imekanusha taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba imekizuia Kiwanda cha Sukari Zanzibar,ZSFL kuuza Sukari yake Tanzania Bara. Msemaji Mkuu wa Serikali Dk.Hassan Abbas Akizungumza jana jijini Arusha,Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Dk.Hassan Abbas amesema, kiwanda hicho kinapaswa kukidhi soko la Zanzibar la tani elfu 10 badala ya kulalamika kimezuiwa kuuza Sukari nje. Dk.Abbas amesema mahitaji ya kawaida Zanzibar ya sukari ni Tani elfu 17 mpaka elfu 20 kwa mwaka lakini kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha tani elfu 10 japo kwa sasa uzalishaji umeshuka hadi tani elfu 8 hivyo kufanya Zanzibar kuwa na upungufu wa tani elfu 9 hadi elfu 12. Mapema wiki hii,Kaimu Mkurugenzi Mkuu Kiwanda hicho cha Sukari Zanzibar,Bi. Fatma Salum Ali,alisema kiwanda hicho kinapata hasara ya zaidi ya shilingi laki tatu kwa kila tani moja ya Sukari inayozalishwa kutokana na kushindwa kupata kibali cha kuuza Sukari Tanzania Bara...

WALIMU 16 WAFUTWA KAZINI

Image
JUMLA ya walimu 16 wamefukuzwa kazi wilayani Nkasi mkoani Rukwa kwa kipindi cha miaka mitatu na wengine 11 wamepewa onyo kali baada ya kubainika wametenda makosa mbalimbali. Hatua hiyo imethibitishwa jana na Katibu wa tume ya utumishi wa walimu TSC wilayani humo  Richard Katyega mbele ya kamishina wa tume ya Utumishi wa walimu Taifa,Samwel Koroso ambapo alisema  kuwa katika kipindi hicho  walipokea mashauri 23 na kupelekea walimu 16 kufukuzwa kazi,11 kupewa onyo kali na wengine 5 waliondolewa kazini baada ya kubainika kuwa na vyeti bandia. Alisema katika mwaka wa fedha wa 2016,2017 na 2018  tume hiyo imesikiliza mashauri hayo na kuyatolea maamuzi ambapo ilifikia maamuzi hayo baada ya kusikiliza mashauri hayo na pasipo kumuonea mwalimu hata mmoja na kutenda haki kwa mujibu wa sheria. Katyega alisema tume hiyo sambamba na kuchukua maamuzi hayo pia imekua ikiwahamasisha walimu kufuata maadili ya ualimu kwa uhakika ili wasiweze kukumbana na adhabu mbal...

MWENYEKITI WA BAJAJI MANISPAA YA MPANDA ANG’ATUKA

Image
Mwenyekiti wa Chama cha madereva pikipiki za tairi tatu maarufu bajaji halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Bw.Rashid Rashid ametangaza kujiuzuru nafasi hiyo. Katika taarifa yake ambayo ameitoa leo Bw.Rashid amesema, miongoni mwa sababu za kujiuzulu kwake ni pamoja na kukosa ushirikiano kutoka kwa madereva wenzake,ukosefu wa ushirikiano kwa kamati yake na kutotekelezwa kwa mipango mbalimbali wanayoipanga kama chama. Aidha amesema changamoto iliyopo kwa sasa ni mgawanyiko wa wamiliki bajaji upande wa watumishi wa serikali kutozingatia kanuni na taratibu za umiliki wa chombo hicho cha usafiri. Kwa upande wa wamiliki binafsi na madereva wao amesema wamekuwa wakikumbwa na mikasa ya kupelekwa kituo cha polisi pamoja na kulipishwa faini mara kwa mara bila utaratibu. Hata hivyo Bw.Rashid amekanusha kula njama na Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu Sumtra kuwatoza madereva bajaji mpaka kiasi cha shilingi 40,000 kwa ajili ya kujinufaisha. Mapema mwaka h...

IFAHAMU TUMBAKU ASILI YAKE,ATHARI KIAFYA,KILIMO MPAKA UVUNAJI NA NCHI ZINAZOONGOZA KILIMO DUNIANI

Image
Tumbaku  (pia  tumbako ) ni majani ( minoga ) makavu ya  mtumbaku  ambayo yanatumiwa na binadamu kwa kuvuta kama sigara,kutafuniwa mdomoni au tumbaku ya kunusa. Tumbaku huwa ndani yake kemikali ya  nikotini  ambayo mwili unazoea haraka sana na kuifanya vigumu kwa wavuta tumbaku kuachana na desturi hii. 1. Asili ya tumbaku 2. Kazi ya nikotini ndani ya tumbaku 3. Hatari za kiafya 4. Kilimo 5. Baada ya mavuno Asili ya tumbaku Asili ya tumbaku ni Amerika ambako  Maindio  wenyeji waliitumia kama dawa ya kidini pia ya burudani. Tangu  Kolumbus  Wahispania walipeleka mtumbaku hadi Ulaya ambako uliangaliwa mwanzoni kama mmea wa kiganga. Matumizi hasa kwa njia ya kuvuta na kutafuna yalienea haraka katika Ulaya na kwa njia ya mabaharia Wareno katika pande zote za dunia. KAZI YA NIKOTINI NDANI YA TUMBAKU Tumbaku inavutiwa hasa kwa sababu nikotini ambayo ni dawa ndani yake inaathiri ubongo na neva ya binadamu na kupungu...

RAIS MAGUFULI AZINDUA KIWANDA CHA SIGARA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Magufuli leo amezindua kiwanda cha kutengeneza sigara cha Philips Morris International kilichopo mkoani Morogoro. Rais Magufuli ametembelea kiwanda hicho na kushuhudia namna sigara zinavyotengenezwa kuanzia katika hatua ya kwanza mpaka sigara inapokamilika kwa matumizi au kwa ajili ya kuuzwa.