Posts

TANZANIA KUWA NA WATU 58 MILIONI IFIKAPO MWISHONI MWA 2018

Image
Tanzania inatarajiwa kufikisha idadi ya watu milioni 58 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu ikiwa ni ongezeko la juu ikilinganishwa na idadi ya awali ya watu milioni 46 iliyoripotiwa mwaka 2010. Kwa mujibu wa Idara ya Jamii na Mambo ya Uchumi ya Shirika la Umoja wa Mataifa (UN),makadirio hayo ni sawa na kila kilomita moja ya mraba kuna wakazi 67 tofauti na makadirio ya mwaka 2010 ya watu 52. Inasema kila sekunde 14,mtoto mmoja anazaliwa nchini huku mtoto mmoja akifariki dunia kila baada ya sekunde moja.

KADA MKONGWE WA CHADEMA AFARIKI DUNIA

Image
Mwanasiasa mkongwe na kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tambwe Hizza amefariki dunia asubuhi ya kuamkia leo (Alhamis ) akiwa nyumbani kwake kwa ugonjwa wa pumu. Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene amethibitisha kifo hicho akisema Hiza amefariki leo asubuhi nyumbani kwake Mbagala akiwa amelala. Hiza amefariki kipindi ambacho alikuwa katika timu ya kampeni za kumnadi mgombea wa ubunge wa Chama hicho katika Jimbo la Kinondoni, Salumu Mwalimu na jana jioni alipanda jukwaani kumnadi. Mwaka 2015,Hiza alitangaza kujiunga na Chadema wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu akitokea CCM ambako aliwahi kuhudumu kama mkuu wa kitengo cha propaganda wa chama hicho tawala.

SERIKALI KUTATUA KERO YA MAJI VIJIJI VYA JIMBO LA KAVUU

Image
Wizara ya maliasili na utalii inatarajia kutatua kero ya maji kwa wakazi wa kata ya Itobanilo na vijiji vyake katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Mkoani Katavi,ili kuondoa mgogoro kati ya askari wa wanayama pori na wananchi wanaotegemea maji ya mto Kavuu uliopo hifadhi ya taifa ya wanyama ya Katavi. Kauli hiyo imetolewa na Naibu waziri wa zira hiyo Mh.Josephat Hasunga,wakati akijibu swali la   Mbunge wa Jimbo la Kavuu Mh.Pudensiana Kikwembe aliyetaka kujua kauli ya serikali kuhusu askari wa wanyama pori wanaowanyanyasa wananchi wanaopata huduma ya maji katika mto Kavuu. Akijibu swali hilo,Mh.Hasunga amesema wizara kwa kushirikiana na mbunge pamoja na wananchi watajadili kwa pamoja ili kutatua kero ya maji ambapo kwa sasa wananchi wanahatarisha afya zao kwa kuchota maji katika hifadhi na kukiuka sheria za nchi.

TANESCO SUMBAWANGA YAPOKEA JENERETA YA KUZALISHA UMEME

Image
KITUO cha kufua umeme mkoani Rukwa kimepata jenereta  ya kufua umeme yenye uwezo  wakuzalisha Megawati 10. Akizungumzia ujio wa jenereta hiyo,Meneja wa TANESCO Mkoani Rukwa Bw.Herini Muhina,amesema hali ya uzalishaji umeme itakuwa hivyo bora zaidi na kufanya upatikanaji wa umeme katika wilaya za Sumbawanga Kalambo,Nkasi kuwa bora zaidi pia katika maeneo ya Laela.

JAJI MKUU WA KENYA AILAUMU SERIKALI YAKE KUKIUKA KATIBA NA SHERIA ZA NCHI

Image
Jaji mkuu wa Kenya,David Maraga ameilaumu serikali ya nchi hiyo kwa kufanya maamuzi kinyume cha sheria na katiba ya kenya katika kukabiliana na upinzani. Jaji mkuu wa Kenya,David Maraga Tamko hilo limekuja mara tu baada ya kiongozi mmoja wa upinzani wakili Miguna Miguna kufukuziwa nchini Canada,baada ya kuzuiliwa na polisi kwa siku tano hata baada ya mahakama kutoa amri kwamba aachiliwe kwa dhamana . Katika maelezo yake jaji David Maraga,amesema malalamiko yaliyopelewekwa mahakamani yalikuwa wazi,na yalikuwa majukumu ya mahakama kufanya maamuzi kwa kuwa ndio chombo pekee cha kutetea haki kwa kila mmoja pamoja na serikali yenyewe. Jaji huyo ametoa tamko hilo la kuionya serikali kwa kushindwa kutii sheria kutokana na kitendo cha serikali ya kenya kuonekana kudharau maamuzi ya mahakama. Kwa mjibu wa madai ya serikali ya Kenya ni Kwamba Miguna Miguna alishakana uraia wa Kenya na kuchukua uraia wa Canada ambapo kata hivyo kwa mjibu wa katiba ya Kenya raia wan chi hiyo anaruhu...

HABARI PICHA KUTOKA BUNGENI DODOMA FEBRUARI 7,2018

Image
Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akisisitiza kuhusu mikakati ya Serikali kutekeleza dhana ya ujenzi wa Uchumi wa Viwanda. Naibu Waziri, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Anjelina Mabula akisisistiza umuhimu wa Halmashauri kutenga maeneo ambayo yatatumiwa na Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) kujenga nyumba za gharama nafuu zitakazouzwa kwa wananchi na watumishi wa Halamshauri husika. Mbunge wa Urambo Mashariki Mhe. Magreth Sita akiuliza Swali Bungeni kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kutatua migogoro ya Ardhi ikiwemo kubatilisha matumizi ya mashamba ambayo hayajaendelezwa. Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Dkt. Aderladus Kilangi akisisitiza jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Kamati hiyo kwa...

SERIKALI KUENDELEA KUWEKA ALAMA YA MIPAKA YA HIFADHI NA MAKAZI

Image
Serikali imesema itaendelea kuweka alama za mipaka ya hifadhi mbalimbali hapa nchini pamoja na kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa mistu ili kuepusha migogoro ya ardhi. Kauli hiyo imetolewa leo bungeni Dodoma na Naibu waziri wa Maliasili na utalii Josephati Hasunga wakati akijibu swali la Mbunge wa Urambo Mkoani Tabora Magreth Simwanza Sitta aliyekuwa akihoji kuhusu mpango wa serikali kumaliza mgogoro wa mpaka kati ya msitu wa North Ugalla na wanaozunguka msitu huo. Akijibu swali la nyongeza la Mh.Sitta pamoja na mambo mengine Mh.Hasunga amesema mara baada ya mkutano wa bunge wataalamu watapanga ratiba ili kufika kwa mara nying8ine Mkoani Tabora ili kutafuta ufumbuzi wa migogoro ya mipaka iliyopo kati ya wananchi na hifadhi. Kwa mjibu wa Mh.Hasunga Misitu ya hifadhi ya Norh Ugalla ina ushoroba wa wanayama ambao mara nyingi husafriri mpaka Hifadhi ya taifa ya Wanyama ya Katavi. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED