Posts

ANC CHAZIDISHA SHINIKIZO DHIDI YA ZUMA MGUU SAWA KATIKA MKUTANO WA KESHO

Image
Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC kimeitisha mkutano wa viongozi wake wa juu utakaofanyika kesho huku kukiwa na taarifa kwamba mkutano huo ni kwa ajili ya kujadili shinikizo la kumtaka rais Jacob Zuma kuachia madaraka. Rais Jacob Zuma atakiwa kujiuzuru Hata hivyo kauli ya chama cha ANC iliyotolewa kuhusiana na mkutano huo imesema,wanakutana kujadili ubadilishanaji madaraka kutoka Rais Zuma kama mwenyekiti wa zamani na sasa Cyril Ramaphosa ambaye ni kiongozi mpya wa chama hicho. Siku ya jumatatu viongozi wandamizi wa chama hicho walilazimika kuwa na mkutano wa dharula mjini Johannesburg kujadili hatima ya rais Zuma. Kwa upande wake rais Zuma ameshikilia msimamo wake kutokubaliana na shinikizo la kumtaka aachie madaraka. Mwezi Disemba mwaka jana Ramaphosa alimrithi rais Zuma katika nafasi ya juu ya kukiongoza chama hicho kikongwe barani Afrika. Nafasi ya urais ya Zuma imekuwa ikiandamwa na kashfa za rushwa, ambapo katika miaka ya hivi karibuni al...

RAIS MAGUFULI ATAKA VIONGOZI WA DINI KUJIEPUSHA NA MIGOGORO

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka viongozi wa dini mbalimbali nchini kuhakikisha wanajiepusha na migogoro mbalimbali ambayo imekuwa ikiharibu sifa na heshima ya taasisi hizo za dini.   Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo wakati alipohudhuria hafla ya kumweka wakfu na kumsimika Mchungaji Jackson Sosthenes Jackson kuwa Askofu wa tano wa Kanisa la Anglikana Dayosis ya Dar es Salaam. Kwa upande mwingine,Dkt.Magufuli amedai endapo mahali kwenye uponyaji wa mwili ukisikia kumeanza matatizo basi unapaswa kutazama jinsi taifa unaloliongoza roho zake zitakavyopotea. Misa ya kumsimika Askofu mteule Sosthenes imefanyika leo ikiongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania, Jacob Chimeledya. Mbali na Rais Magufuli aliyekuwa mgeni rasmi wengine waliohudhuria ni mke wa Rais Maguli mama Janeth Mafuli,Rais mstaafu Benjamin Mkapa. Wengine ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,Jenerali Venance Mabeyo,Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba,Waziri wa ...

MAGUFULI AWATUNUKU MAOFISA 197 WA JWTZ

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli amewatunuku kamisheni maofisa wanafunzi 197 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Sherehe hizo zimefanyika leo katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam ambapo maofisa hao wapya ni wa Tanzania na kutoka nchi marafiki waliopata mafunzo katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli mkoani Arusha. Katia tukio hilo ambalo limepambwa na magwaride kutoka kwa Wanajeshi hao,limehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Kitaifa ambapo miongoni mwa waliotunukiwa kamisheni hizo wanawake ni 28 na waliobaki wakiwa ni wanaume. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

RAIS MAGUFULI AMSAIDIA MLEMAVU BAJAJI

Image
Rais waJamhuriya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli ametekeleza ahadi yake ya kumsaidia Bajaj Mlemavu wa viungo Bw.Yusuf Abdulrahaman Ndemanga. Bw.Ndemanga amekabidhiwa Bajaji hiyo na Katibu wa Rais Bw.Ngusa Samike,Ikulu Jijini Dar es Salaam leo Februari 02. Mhe.Rais Magufuli alikutanana Bw.Ndemanga tarehe 25 Agosti,2017 katika sehemu ya abiria wakati akisubiri kupanda kivuko cha MV Magogoni kuelekea Kigamboni Jijini Dar es Salaam. Mara baada ya kukutana na Mhe.Rais Magufuli,Bw. Ndemanga alimuomba msaada wakupatiwa Bajaj ili imsadie kupata kipato. Akikabidhi msaada huo Bw.Ngusa Samike amemtaka Bw. Ndemanga kuitumia Bajaj hiyo vizuri na kujiongezea kipato kitakacho msaidia yeye na familia yake. Kwa upande wake Bw.Ndemanga aliyeongozana na Mkewe Bi.Hawa Mohamed amemshukuru Mhe.Rais Magufuli kwa msaada huo na ameahidi kuwa ataitumia Bajaj hiyo vizuri kuzalisha kipato kwa ajili ya familia yake. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

RAIS MAGUFULI KUWATUNUKU KAMISHENI MAAFISA WAPYA WA JWTZ

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli kesho anatarajia kuwatunuku kamisheni maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Kwa mjibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais I kulu Gerson Msigwa kamisheni hizo atazitunuku katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam. Watakaotunukiwa kamisheni ni maafisa wapya wa Tanzania na kutoka nchi marafiki waliopata mafunzo katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha. Tukio hilo linatarajia kurushwa moja kwa moja na vyombo vya habari hapa nchini kuanzia saa 3:00 asubuhi. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

TUNDU LISSU NAYE AMLILIA MZEE KINGUNGE

Image
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema),Tundu Lissu amezungumzia kifo cha Kingunge Ngombale Mwiru akisema historia itamkumbuka. Akizungumza leo Februari 2, 2018  ameanza kwa kusema “namtakia mapumziko mema.” Amesema Mzee Kingunge alikuwa miongoni mwa wazee wenye historia kubwa na alionyesha ujasiri mkubwa wa kuhama chama chake cha CCM bila kuhofia kuhudhuriwa kutokana na mazingira yalivyokuwa. Kingunge aliyekuwa kada wa CCM mwenye kadi namba nane,Oktoba 4,2015 alitangaza kukihama chama hicho na kusema hatojiunga na chama chochote lakini mara kadhaa alionekana akipanda majukwaa ya upinzani kumnadi aliyekuwa mgombea urais wa Chadema/Ukawa, Edward Lowassa kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25,2015. Tundu Lissu ambaye ni Rais  wa chama cha wanasheria nchini TLS anapatiwa matibabu nchini ubelgiji baada ya kushambuliwa kwa risasi mwaka uliopita. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA MZUNGUKO WA PILI KUANZA KESHO

Image
Ligi kuu soka Tanzania Bara inatarajia kuendelea tena hapo kesho kwa mzunguko wa pili kupigwa katika viwanja mbali mbali. Singida United inayoshika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi ikiwa na alama 27 nyuma ya mabingwa watetezi Yanga SC wenye pointi 28 inajipanga kuingia katika mzunguko wa pili hapo kesho siku ya Jumamosi kwa kuivaa Mwadui FC majira ya saa nane mchana katika uwanja wa Namfua. Michezo mingine itakayo pigwa hapo kesho ni Azam FC waliyo nafasi ya pili kwa kujikusanyia alama 30 katika duru la kwanza itakuwa nyumbani dhidi ya Ndanda FC mechi itakayopigwa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam. Lipuli FC ya Iringa itakuwa na kibarua kizito nyumbani kwake itakapocheza dhidi ya Yanga SC iliyo maliza mzunguko wa kwanza kwa kuwa na pointi 28 ikiwa nafasi ya tatu mtanange utakaopigwa dimba la Samora, wakati Stand United ikiivaa Mtibwa Sugar uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga. Tanzania Prisons iliyo na alama 21 ikiwa nafasi ya 6 katika msimamo wa ligi wata wakar...