Posts

MBUNGE CHADEMA MKOANI KATAVI AIBUKA NA HOJA YA KUPATIKANA DIWANI MWINGINE WA KATUMBA

Image
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Katavi kupitia   Chadema Rhoda Kunchela amesema kitendo   cha kata ya Katumba halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi kutokuwa na diwani ni kuchelewesha maendeleo kwa wananchi wa kata hiyo. Hayo yamebainishwa leo na Mbunge huyo na kusema kuwa wananchi wanakosa uwakilishi  na kushauri uchaguzi ufanyike ili apatakane diwani mwingine. Katika hatua nyingine Mh Kunchela  amezungumzia ziara aliyoifanya mwenyekiti wa Bawacha taifa  Halima Mdee amabye pia ni mbunge wa jimbo la kawe na kusema ziara  hiyo imefanyika mkoani katavi ikilenga kuimarisha uhai wa chama hicho. Diwani aliyekuwa akiongoza kata hiyo Mh Seneta Baraka mwezi Novemba mwaka jana alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kupokea rushwa. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

RAIS WA LIBERIA ATIMULIWA

Image
Rais anayemaliza muda wake nchini Liberia,Ellen Johnson Sirleaf,ametimuliwa katika chama chake kwa tuhuma za kutomuunga mkono mgombea wake ili amrithi. Chama chake cha Unity kinamtuhumu Bi.Ellen, kwa kuwahamasisha wananchi kutompigia kura mgombea ambaye alikuwa Makamu wa Rais Joseph Boakai. Aidha,chama hicho kinamtuhumu kwa kukiuka Katiba kwa madai ya kumfanyia kampeni George Weah,ambaye aligombea kupitia chama cha Coalition for Democratic Change na kuibuka mshindi. Bw.Weah ambaye ni mwanasoka nyota wa zamani, anatarajiwa kuapishwa rasmi Januari 22 mwaka huu ikiwa ni mara ya kwanza Liberia kushuhudia mabadiliko ya uongozi kwa njia ya amani tangu mwaka 1944. Chanzo:EATV Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

RAIS WA RWANDA PAUL KAGAME AFANYA ZIARA HAPOA NCHINI,APANGA MIKAKATI YA MAENDELEO NA RAIS MAGUFULI

Image
Rais wa Jamhuri ya Rwanda Mhe.Paul Kagame leo tarehe 14 Januari, 2018 amefanya ziara ya kikazi ya siku moja hapa nchini kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli. Katika Picha Rais Magufuli Kushoto na Kulia ni Rais Kagame Mhe. Rais Kagame amewasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na kupokelewa na mwenyeji wake Mhe.Rais Magufuli na kisha kulakiwa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, na baadaye akaelekea Ikulu ambako pamoja na kufanya mazungumzo ya faragha, viongozi hao wamezungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari. Mhe.Rais Magufuli amesema katika mazungumzo yao wamekubaliana ujenzi wa reli kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) kati ya Isaka nchini Tanzania na Kigali nchini Rwanda yenye urefu wa takribani kilometa 400 uanze mwaka huu (2018), na wamewaagiza Mawaziri wanaohusika na miundombinu kukutana ndani ya kipindi cha wiki mbili kuanza sasa il...

MELI YA MAFUTA ILIYOKUWA IKITEKETEA MOTO IMEZAMA BAHARINI

Image
Meli ya mafuta ambayo imekuwa ikiteketea kusini mwa bahari ya China kwa zaidi ya wiki moja hatimaye imezana Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Meli ya mafuta iliyokuwa ikiteketea moto imezama baharini . Kwa mjibu wa vyombo vya habari vya China,Sanchi na meli nyingine ya mizigo ziligongana kilomita 260 nje ya Shanghai Januari 6 mwaka huu ambapo baadaye ilianza kusombwa kusini mashariki kwenda Japan. Maafisa wa Iran sasa wanasema  Image caption Meli hiyo ilikuwa imebeba tani 136,000 za mafuta lakini maafisa wanasema kuwa hakuna hatari kubw a.  wahudumu wote 32, wakiwemo raia 30 wa Iran na wawili raia wa Bangladesh wote walifariki. Meli hiyo ilikuwa imebeba tani 136,000 za mafuta lakini maafisa wanasema kuwa hakuna hatari kubwa ambapo Meli zingine 13 na kikosi kutoka Iran wamekuwa wakishiriki katika jitihada za kuokoa licha ya kuwepo hali mbaya ya hewa. Siku ya Jumamosi wafanyakazi walikuwa wameingia kwenye meli hiyo ambapo walipata miili ya wahudumu wawili ...

WAKAZI WILAYANI MPANDA SERIKALI IWAJIBIKE KUTENGA MAENEO YA WAFUGAJI NA WAKULIMA

Baadhi ya wakazi wa kata ya Magamba Manispa ya Mpanda mkoani Katavi wameitaka serikali kutenga maeneo ya wafugaji na wakulima ili kuepusha migogoro ya ardhi inayojitokeza mara kwa mara Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema wakulima na wafugaji wanapoendesha shughuli zao katika eneo moja huchangia mifarakano isiyo ya lazima na kushauri wafugaji kutengewa eneo tofauti na wakulima ili kuondoa mwingiliano Kwa upande wake Bi.Anna Thomas ambaye ni mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Magamba amekiri kuwepo kwa migogoro ya mara kwa mara baina ya wakulima na wafugaji na kuongeza kuwa inachangangiwa na wafugaji kuwa na mifugo mengi kwenye eneo dogo Philemone Tesha Afisa kilimo wa kata ya magamba amesema serikali ina mpango wa kutenga maeneo ya kuchungia yatakayokuwa tofauti na mashamba japo hakubainisha wazi mpango huo ni lini utaanza kutekelezwa. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

MWENYEKITI WA BAVICHA TAIFA ZIARANI KATAVI ATOA NENO

Image
Mwenyekiti wa Taifa   balaza la wanawake la Chama cha Democrasia na Maendeleo Chadema   Ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kawe Halima Mdee amezitaka taasisi za ndani ya chama hicho kuwajibika vyema katika kukijenga chama hicho. Akizungumza na wanawake wa chama hicho pamoja na vijana katika shule ya sekondari ya Mtakatifu Maria  manispaa ya Mpanda  amesema  Taasisi hizo kwa kushilikiana na vijana vinamchango mkubwa katika kukijenga chama hicho Hapa nchini Kwa upande wake mbunge wa viti maalumu wa chama hicho katika Mkoa wa Katavi Rhoda Kunchela amesema kunavikundi mbalimbali vya akina ambavyo vimeanza kunufaika. Ziara hiyo ya mwenyekiti wa Bawacha Taifa inalengo la  kukagua uhai wa jumuia hiyo na chama kwa ujumla katika mikoa ya Rukwa Tabora na  Katavi  ugeni huo umeambatana na katibu mkuu wa balaza la wanawake la chama hicho Taifa Grace Tendega. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

DK.SHEIN ATUNUKU NISHANI ZILIZOTUKUKA 43

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Ali Mohammed Shein ametunuku nishani zilizotukuka 43 kwa viongozi na watumishi wa umma ikiwa ni maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar. Dkt.Shein ametoa nishani hizo kwa mutu ambae aliasisi,alishiriki na kutukuza pamoja na kuyaenzi Mapinduzi ya Zanzibar yaliyotokea mwaka 1964. Pamoja na hayo Dk. Shein amewataka wananchi wa Zanzibar kuendelea kudumisha amani na utulivu uliopo ili kuwa chachu ya kuendelea kuwa kivutio kikubwa kwa uwekezaji miradi mikubwa ya maendeleo visiwani . Katika maadhimisho hayo mbali ya nishani hizo serikali ya Zanzibar huzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni ishara ya ukombozi wa fikra na maendeleo ya kiuchumi ya taifa hilo. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED