Posts

UHABA WA VYUMBA VYA MADARSA MKOANI KIGOMA WANAFUNZI ZAIDI YA 2000 WAKOSA KUJIUNGA NA SEKONDARI.

Image
Upungufu wa vyumba   vya madarasa wilayani Uvinza Mkoani Kigoma imekuwa sababu ya zaidi ya wanafunzi 2000 kukosa nafasi ya kujiunga na masomoa ya sekondari kwa mwaka 2018. Kutokana na hali hiyo,imewalazimu wakazi wa kijiji cha Nyanganga wilayani humo kuamua kuanza ujenzi wa shule ya sekondari ili wanafunzi waliochaguliwa waanze masomo. Wilaya hiyo ina upungufu wa vyumba vya madaras 73 ambapo hata hivyo wanafunzi wengi wanalzamika kusafiri umbali wa karibu masaa 3 kutoka nyumbani kufuata shule katika vijiji vya jirani na wengine kulazimika kuhama nyumbani kuishi karibu na shule hizo. Kama sehemu ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto hiyo, Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na watoto Dk.Fustine amechangia mifuko 20 ya saruji na kuwataka wananchi kushirikiana katika miradi mbambali ya maendeleo yao. Nao Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Bw.MwanamvuaMlindo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Weja Ngolo wametoa pamoja na kusema kuwa wameweka m...

RAIS MAGUFULI AMEMTEUA ALIYEKUWA KATIBU MKUU IKULU BW.ALPHAYO KIDATA KUWA BALOZI

Image
Rais John Magufuli ameteua mabalozi wapya wawili ambao ni Alphayo Kidata na Meja Jenerali Mstaafu,Simoni Mumwi. Alphayo Kidata Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu,Gerson Msigwa imesema Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi John Kijazi amesema uteuzi wa Kidata umeanza jana Jumatano Januari 10. Kabla ya uteuzi huo Kidata alikuwa Katibu Mkuu,Ikulu. Taarifa hiyo imeeleza kuwa mabalozi hao wateule watapangiwa vituo vyao vya kazi na kuapishwa baada ya taratibu kukamilika. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

SUALA LA AIRTEL MIKONONI MWA RAIS,WAZIRI WA AFYA NA SHERIA NAO WATEKELEZA MAAGIZO YA RAIS

Image
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Philip Isdor Mpango leo amewasilisha taarifa ya kamati aliyoiunda kuchunguza umiliki wa kampuni ya simu Airtel kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli aliyeagiza kufanyika kwa uchunguzi huo Desemba 20 mwaka jana. Dkt.Philipo Mpango Baada ya kuwasilisha taarifa hiyo,Dkt.Mpango amesema Serikali imejiridhisha kuwa ubinafsishaji wa Shirika la Simu Tanzania ( TTCL ) kwenda Celtel,baadaye kuhamishiwa Zain na sasa Airtel ulifanyika kwa ukiukwaji mkubwa wa sheria,kanuni na taratibu. Kufuatia ukiukwaji huo Dkt.Mpango amesema Serikali inayomiliki asilimia 40 ya hisa za kampuni ya Airtel imeamua kufanya mazungumzo na kampuni ya Airtel inayomiliki asilimia 60 ya hisa ili nchi iweze kupata haki yake. Dkt.Ummy Mwalimu Wakati huo huo, Mhe.Rais Magufuli amepokea taarifa ya utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa Novemba 25 mwaka jana wakati wa ufunguzi wa Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirik...

NAIBU WAZIRI AWAKABIDHI SILAHA MADEREVA BODABODA MKOANI KATAVI TAYARI KUPAMBANA NA MIMBA ZA UTOTONI

Image
Na.Issack Gerald Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Dk.Faustine Ndugulile,amewataka waendesha pikipiki Mkoani Katavi kushirikiana na serikali ili kutokomeza mimba za utotoni. Dk.Ndugulile ametoa agizo hilo leo wakati akitunuku vyeti kwa waendsha pikipiki 100 wa Manispaa ya Mpanda waliohitimu mafunzo ya kidhibiti Mimba za utotoni huku akiwataka pia watendaji wa wizara mpaka wilaya kote nchini kutatua shida zinazowakabili madereva hao. Wakati huo huo Dk.Ndugulile amekabidhi baiskeli tano kwa wasimamizi wa mashauri ya watoto Manispaa ya Mpanda baiskeli ambazo zimetolewa na shirika la JSI la Marekani ili baiskeli hizo zitumike kuwafikia watoto waishio katika mazingira hatarishi. Kwa upande wake Mwenyekiti wa waendesha pikpiki Mkoani Katavi Mh.Asalile Mwakabafu amesema wao watahakikisha wanashiriki kudhibiti mimba za utotoni huku akisisitiza serikali kusimamia watendaji wake wasioshughulikia matatizo ya waendesha pikipiki Mkoani Katavi. Kwa upan...

RC RUKWA APIGA MARUFUKU KUPAKIA MIZIGO KATIKA MWALO WA KIRANDO

Image
SERIKALI mkuu mkoani   Rukwa imepiga marufuku   kuutumia mwalo uliopo katika   Kijiji cha Kirando ziwa Tanganyika kwa ajili ya kupakia na kushia mizigo kwani mwalo huo umetengwa kwa ajili ya shughuli za kuuzia samaki. Mkuu wa mkoa huo Joachim Wangabo alisema hayo akiwa katika ziara ya kikai wilayani Nkasi na kukuta katika mwalo wa Kirando unatumika kama bandari ambapo malori yalikuwa yakipakua na kupakia mizigo kwa lengo la kusafisirisha  kuipeleka kwenye visiwa vilivyopo ziwa Tanganyika. Alisema kuwa wananchi wasipotoshe lengo la kutebnwa kwa  mwalo huo ambayo ni kwaajili ya kuuza na kununua samaki wavuliwao kwenye ziwa Tanganyika na si  kwaajili ya magari kupakilia mizigo. Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa sehemu iliyotengwa ikitumika kama bandari haiko vizuri basi waone namna ya kuboresha ili sehemu hiyo ilirudi kama ilivyokuwa na sio kuikimbia na kuiacha kama ilivyo jwani kukimbia tatizo sio suluhisho bali kupambana na changamoto zilizopo na kubore...

DC MKOANI RUKWA APIGA MARUFUKU WAGONJWA WA KIPINDU PINDU KUPELEKWA KWA WAGANGA WA JADI

Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa Dk.Halfan Haule amewataka wakazi wa bonde ziwa Rukwa,kuacha tabia ya kuwapeleka wagonjwa wa kipindupindu kwa waganga wa kienyeji badala yake wawapeleke vituo vinavyotoa huduma za afya ili kupata tiba za kitaalamu. Mkuu huyo wa wilaya alisema hayo wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Mtowisa wilayani Sumbawanga mkoani humo. Alisema tabia ya baadhi ya wananchi kuendekeza imani za kushirikina na kuwapeleka wagonjwa wa kipindupindu kwa waganga wa kienyeji kunahatarisha maisha ya wagonjwa hao na wakati mwingine kusababisha vifo. Alisema jamii ya watu wa bonde la ziwa Rukwa ambako ugonjwa huo umeenea ipo haja sasa kubadilika na kuachana na tabia hiyo kwani ugonjwa huo unatokana na uchafu na si  kulogwa hivyo wanapaswa  kuwapeleka wagonjwa  katika zahanati,vituo vya afya na hospitali ili wapate tiba sahihi ambazo zitaokoa maisha yao. Aidha Dk.Haule alipiga marufuku tabia ya kaya moja kutumia choo kimoja badala yake alitaka...

WAFANYABIASHARA WILAYANI MPANDA WASITISHA MGOMO WA SIKU MBILI

Image
Mamia ya wafanyabiasahara katika masoko ya Mpanda Mkoani Katavi leo wameanza kufanya biashara kama kawaida kufuatia kuwepo kwa mgomo huo kwa muda wa siku mbili. Wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema wamefanya mazungumzo na uongonzi wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Katavi ili kufikia mwafaka wa mgomo uliosababishwa na kupandishwa kwa bei ya Pango kutoka sh 15,000 kwa hapo awali na kufikia shilingi 60,000. Kwa upande wa Mwenyekiti wa Soko la Buzogwe ambalo ni kitovu cha mvutano huo Bw.Ramadhani Karata  amedai amekuwa  mafichoni  kwa muda kutokana na kuandamwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za yeye kuwa chanzo. Mgomo wa wafanyabiashara hasa katika soko kuu la Wilaya ya Mpanda na Soko la Buzogwe ulianza juzi ambapo Mkuu wa Wilaya alikuwa amesisitiza kuwa mfanyabiashara asiyetaka kulipa tozo hizo arudishe chumba cha biashara. Hata hivyo mwafaka kamili kuhusu kiasi ambacho kinatakiwa kulipwa na wafanyabiashara kinatarajiwa kutolewa baada ya wiki moja hiyo ikiwa ni...