Posts

RC RUKWA APIGA MARUFUKU KUPAKIA MIZIGO KATIKA MWALO WA KIRANDO

Image
SERIKALI mkuu mkoani   Rukwa imepiga marufuku   kuutumia mwalo uliopo katika   Kijiji cha Kirando ziwa Tanganyika kwa ajili ya kupakia na kushia mizigo kwani mwalo huo umetengwa kwa ajili ya shughuli za kuuzia samaki. Mkuu wa mkoa huo Joachim Wangabo alisema hayo akiwa katika ziara ya kikai wilayani Nkasi na kukuta katika mwalo wa Kirando unatumika kama bandari ambapo malori yalikuwa yakipakua na kupakia mizigo kwa lengo la kusafisirisha  kuipeleka kwenye visiwa vilivyopo ziwa Tanganyika. Alisema kuwa wananchi wasipotoshe lengo la kutebnwa kwa  mwalo huo ambayo ni kwaajili ya kuuza na kununua samaki wavuliwao kwenye ziwa Tanganyika na si  kwaajili ya magari kupakilia mizigo. Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa sehemu iliyotengwa ikitumika kama bandari haiko vizuri basi waone namna ya kuboresha ili sehemu hiyo ilirudi kama ilivyokuwa na sio kuikimbia na kuiacha kama ilivyo jwani kukimbia tatizo sio suluhisho bali kupambana na changamoto zilizopo na kubore...

DC MKOANI RUKWA APIGA MARUFUKU WAGONJWA WA KIPINDU PINDU KUPELEKWA KWA WAGANGA WA JADI

Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa Dk.Halfan Haule amewataka wakazi wa bonde ziwa Rukwa,kuacha tabia ya kuwapeleka wagonjwa wa kipindupindu kwa waganga wa kienyeji badala yake wawapeleke vituo vinavyotoa huduma za afya ili kupata tiba za kitaalamu. Mkuu huyo wa wilaya alisema hayo wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Mtowisa wilayani Sumbawanga mkoani humo. Alisema tabia ya baadhi ya wananchi kuendekeza imani za kushirikina na kuwapeleka wagonjwa wa kipindupindu kwa waganga wa kienyeji kunahatarisha maisha ya wagonjwa hao na wakati mwingine kusababisha vifo. Alisema jamii ya watu wa bonde la ziwa Rukwa ambako ugonjwa huo umeenea ipo haja sasa kubadilika na kuachana na tabia hiyo kwani ugonjwa huo unatokana na uchafu na si  kulogwa hivyo wanapaswa  kuwapeleka wagonjwa  katika zahanati,vituo vya afya na hospitali ili wapate tiba sahihi ambazo zitaokoa maisha yao. Aidha Dk.Haule alipiga marufuku tabia ya kaya moja kutumia choo kimoja badala yake alitaka...

WAFANYABIASHARA WILAYANI MPANDA WASITISHA MGOMO WA SIKU MBILI

Image
Mamia ya wafanyabiasahara katika masoko ya Mpanda Mkoani Katavi leo wameanza kufanya biashara kama kawaida kufuatia kuwepo kwa mgomo huo kwa muda wa siku mbili. Wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema wamefanya mazungumzo na uongonzi wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Katavi ili kufikia mwafaka wa mgomo uliosababishwa na kupandishwa kwa bei ya Pango kutoka sh 15,000 kwa hapo awali na kufikia shilingi 60,000. Kwa upande wa Mwenyekiti wa Soko la Buzogwe ambalo ni kitovu cha mvutano huo Bw.Ramadhani Karata  amedai amekuwa  mafichoni  kwa muda kutokana na kuandamwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za yeye kuwa chanzo. Mgomo wa wafanyabiashara hasa katika soko kuu la Wilaya ya Mpanda na Soko la Buzogwe ulianza juzi ambapo Mkuu wa Wilaya alikuwa amesisitiza kuwa mfanyabiashara asiyetaka kulipa tozo hizo arudishe chumba cha biashara. Hata hivyo mwafaka kamili kuhusu kiasi ambacho kinatakiwa kulipwa na wafanyabiashara kinatarajiwa kutolewa baada ya wiki moja hiyo ikiwa ni...

RAIS AMUAPISHA NAIBU WAZIRI WA MADINI,AMTENGUA KAMISHNA WA MADINI NA KUTEUA MWINGINE

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt. John Pombe Magufuli leo amemuapisha Mhe.Doto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini na kuiagiza Wizara hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Katiba na Sheria kuhakikisha kanuni za sheria mpya ya madini namba 7 ya mwaka 2017 inasainiwa ifikapo Ijumaa tarehe 12 Januari 2018. Mh.Rais Magufuli ametoa agizo hilo muda mfupi baada ya Mhe.Biteko kuapishwa Ikulu Jijini Dar es Salaam na ameelezea kutoridhishwa kwake na namna viongozi na watendaji wa Wizara ya Madini wanavyotekeleza majukumu yao polepole na bila kujali maslahi ya nchi. Amemuagiza Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi kushirikiana na Naibu Mawaziri, Katibu Mkuu na Wakurugenzi wanaohusika katika Wizara ya Madini kuhakikisha kanuni hizo zinasainiwa. Pamoja na maagizo hayo Mh.Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Kamishna wa Madini Mhandisi Benjamin Mchwampaka na amemteua Prof. Shukrani Elisha Manya kuwa Kamishna wa Madini na pia kukaimu nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Kam...

RAIS MAGUFULI AIPA SIKU 5 WIZARA YA KILIMO,WAZIRI MTEGONI

Image
Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Kilimo kuhakikisha mbolea inafikishwa katika mikoa yote ya uzalishaji wa chakula ukiwemo Mkoa wa Rukwa ifikapo Ijumaa Januari 12, 2018. Magufuli ameyasema hayo leo wakati akimwapisha Mhe. Dotto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini Ikulu jijini Dar es Salaam.  Amemuelekeza Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa kufuatilia jambo hilo na amebainisha kuwa endapo mbolea haitafikishwa katika maeneo hayo ifikapo Ijumaa wahusika waachie ngazi. Rais Magufuli amewataka watendaji wote wa Serikali kutekeleza majukumu yao ipasavyo na ameonya kuwa hatosita kumfukuza kazi mtendaji yeyote atakayeshindwa kutekeleza wajibu wake kwa maslahi ya Watanzania. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

MATOKEO YA DARASA LA NNE NA KIDATO CHA PILI YATANGAZWA

Image
Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mitihani ya upimaji wa darasa nne na kidato cha pili iliyofanyika Novemba 22 na 23 mwaka jana huku idadi kubwa ya wanafunzi wakifanya vyema katika mitihani hiyo. Akitangaza matokeo hayo leo,Katibu Mtendaji wa Necta,  Dk.Charles Msonde amesema jumla ya wanafunzi 1,086,156 waliofanya mtihani wa darasa la nne wamefaulu  kati ya 1,158,444 waliofanya upimaji huo. Amesema  wanafunzi hao wamefaulu kwa kupata alama zenye madaraja ya A,B,C na D wakati wanafunzi 72,288 sawa na asilimilia 6.24 wamepata alama za daraja E, ambao ni ufaulu usioridhisha. Kuhusu matokea ya upimaji wa kidato cha pili,Dk Msonde  amesema jumla ya wanafunzi 433,453 sawa na asilimia 82.32 kati ya 486,742 waliosajiliwa  kufanya mtihani huo wamepata ujuzi wa maarifa ya kuwawezesha kuendelea  na kidato cha tatu. Dk Msonde alisema wanafunzi wa kidato cha pili  51,807 sawa na asilimia 10.68 wameshindwa kupata alama za kuwaweze...

WAFANYABIASHARA WILAYANI MPANDA WAGOMA KUFUNGUA MADUKA,DC ATOA KAULI

Image
Na.Issack Gerald Mkuu wa wilaya ya mpanda Liliani Charles Matinga ameamuru masoko yote kufunguliwa  baada ya wafanyabiashara kufanya  mgomo kutokana na ongezeko la tozo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kodi. Amri hiyo ameitoa leo asubuhi wakati akiwa soko kuu  ambapo wafanyabiashara waliogoma  kufungua biashara zao huku akisema kwa anayeshindwa arudishe  chumba cha biashara. Amesema wamekaa na wafanyabiashara kwa ajili ya kupanga ongezeko hilo ambapo hapo awali halimashauri ilipanga laki moja na baada ya hapo  ikapungua hadi elfu sitini. Awali wafanya biashara hao wamesema walishindwa kumudu kodi iliyokuwepo ya shilingi 15000 ambapo wamesema serikali kuwatoza shilingi 60000 ni kuendelea kuwakandamiza. Masoko amabyo wafanyabiashara wamefunga biashara zao ni Soko kuu la Wilaya ya Mpanda na Soko la Buzogwe lenye zaidi ya wafanyabiashara zaidi ya 500 hii ikiwa ni kwa mjibu wa baadhi ya wafanyabiashara. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED