Posts

TMA IMETAJA MIKOA ITAKAYOPATA MVUA KUBWA SIKUKUU ZA KRISMASI NA MWISHO WA MWAKA

Image
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),imesema wakati wa kuelekea sikukuu za Krismasi na mwisho wa mwaka,mvua kubwa zinatarajiwa kunyesha katika mikoa ya Mbeya,Songwe,rukwa na Kigoma. Meneja wa kituo Kikuu cha Utabiri wa Hali ya Hewa wa TMA,Samuel Mbuya,amesema mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo ya ukanda wa Pwani ni zile za kumalizika kwa msimu wa vuli. Mbuya alieleza Mikoa hiyo minne iliyotajwa ndiyo inayotarajiwa kuwa na mvua wakati wa sikukuu na ifikapo mwisho wa mwezi huu huku mvua zinazoendelea kunyesha katika mikoa mbalimbali ikiwamo Dar es Salaam zitakuwa zimefikia ukingoni. Aidha amesema TMA inatarajia mvua zitaendelea kunyesha katika mikoa ya Kigoma,tabora,Katavi,Rukwa, Songwe,Mbeya,Ruvuma,Lindi,Dodoma na Singida. Mvua katika mikoa hiyo zilianza kunyesha Novemba na zinatarajiwakumalizika mwezi Aprili mwakani. Wakati huo huo Mbuya amewataka wananchi kuendelea kufuatilia taarifa zinazotolewa na TMA mara kwa mara ili kupata mwelekeo wa hali ya hewa pamoja na k...

JELA MIAKA 30 KWA KUUA TEMBO MKOANI KATAVI

Image
MAHAKAMA ya wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imemuhukumu Jackison  Eijuel (52) mkazi wa kata ya Katumba kutumikia kifungo cha  miaka 30 jela na kulipa faini ya shilingi milioni 99 baada ya kupatikana na  hatia ya kumiliki na meno manne ya tembo pamoja na vipande vinne vya meno hayo. Hukumu  hiyo  ilitolewa juzi  na  hakimu   mkazi  mfawidhi wa  mahakama hiyo Chiganga  Tengwa baada ya  kuridhika  na  ushahidi uliotolewa   Mahakamani  hapo  ambapo mshitakiwa  hakuwa na shahidi yoyote kwa upande wake. Akisoma hukumu  hiyo hakimu Twengwa alisema  mahakama imebaini mtuhumiwa alitenda kosa hilo  kinyume  na  kifungu  cha  sheria  namba 235  cha mwenendo  wa  mashitaka. Alisema  baada ya  kusikiliza  ut...

MKUU WA JESHI TANZANIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA ZAHANATI YA JESHI LA POLISI MKOANI KATAVI

Image
Na.Issack Gerald Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon,ameweka jiwe la msingi ujenzi wa zahanati ya Jeshi la Polisi Mkoani Katavi. Katika taarifa ya Mkuu wa Polisi Wilayani Mpanda Maria Kwayi,amesema mpaka sasa zaidi ya shilingi milioni 7 zimekwishatumika katika ujenzi ambapo inahitajika zaidi ya shilingi milioni 29 ili jengo likamilike huku changamoto ikiwa ni upungufu wa vifaa vya ujenzi. Kwa upande wake IGP sirro mara baada ya kupokea taarifa hiyo amesema jeshi la polisi litaongeza takribani milioni kumi na Tano ili kuunga juhudi za ujenzi wa zahanati hiyo. Wakati huo huo IGP siro aliyehitimisha ziara yake jana Mkoani Katavi amesema,wafanyabiashara Mkoani Katavi,Jeshi la Polisi Mkao makuu na serikali kuu wataangazia hatua za haraka ili zipatikane nyumba kwa ajili ya polisi ili kutatua uhaba wa nyumba za polisi Mkoani Katavi. IGP Simon Sirro alikuwa na ziara ya kikazi siku mbili juzi na jana Mkoani katavi akitokea Mkoani Kigoma kabla ya kuelekea Mkoani Rukwa. Haba...

IGP SIRRO AWAOMBA VIONGOZI WA DINI MKOANI RUKWA KUHUBIRI AMANI ILI UHARIFU UPUNGUE

Image
Na.Issack Gerald Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon amewaomba viongozi wa dini mkoani Rukwa Kuongeza bidii katika kuhubiri amani ili mauaji yanayotokayo na imani za kishirikina na mapenzi yapungue mkoani humo.  IGP Sirro ametoa kauli hiyo wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua mikakati ya jeshi hilo katika kukabiliana na mauaji mkoani humo. Amesema jeshi la polisi linajitahidi kukabiliana na mauaji yote yanayotokea nchini lakini katika Mkoa wa Rukwa takwimu zinaonesha kuwa mauaji yanayotokana na ushirikina pamoja na  wivu wa mapenzi yanaongoza mkoani humo. Kamanda Sirro amesema viongozi wa dini wana jukumu kubwa kuhakikisha wanahubiri amani ili mauaji hayo yapungue kwani juhudi hizo zinapaswa kuwa za pamoja kwa kuwa nao wana nafasi kubwa la kuwalea wananchi kiroho. Wakati huo huo IGP Sirro ameahidi kuwa Jeshi hilo kupitia bajeti zake litajenga kituo kipya cha polisi cha Sumbawanga mjini kwa kuwa kilichopo ni kichakavu na majengo yanayot...

WAKULIMA WA TUMBAKU MKOANI KATAVI WAILAUMU SERIKALI KUSHINDWA KUTEKELEZA KAULI YAKE

Image
Na.Issack Gerald Wakulima wa zao la tumbaku wa chama cha msingi cha ushirika Mpanda Kati Mkoani Katavi wameilaumu serikali kushindwa kutekeleza agizo lake la kuhakikisha tumbaku iliyo kosa soko inanunuliwa. Wakulima hao  kwa nyakati tofauti wamesema mpaka sasa hawajui hatima ya ununuzi wa tumbaku yao huku wengine wakisema wameathirika kiuchumi na maisha kwa ujumla. Hivi karibuni,mwenyekiti chama cha msingi cha Ushirika Mpanda Kati Bw.Sosipeter Salvatory ,alisema kuna kiasi cha kilo  elfu ishirini na mbili ambazo hazijanunuliwa kati ya kiasi chote cha tumbaku iliyozalishwa katika msimu wa mwaka  mwaka 2016/2017. Mnamo Novemba 17 mwaka huu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akiahirisha vikao vya Bunge mjini Dodoma alieleza kuwepo kwa kampuni itakayo nunua Tumbaku iliyosalia pamoja na Mbaazi.   Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

IGP SIRO AKIWA MKOANI KATAVI AMESISITIZA KUCHUKUA HATUA KALI ZA KISHERIA KWA WAHARIFU NCHINI

Image
Na.Issack Gerald Mkuu wa Polisi nchini IGP Simon Sirro akiwa ziarani Mkoani Katavi,amesema Jeshi la polisi litaendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa watu wote wanaojihusisha na uharifu mbalimbali ikiwemo Mauaji ya watu kwa imani za kishirikina. IGP Sirro ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kupokea ripoti ya mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga kuhusu hali ya ulinzi,amani na usalama mkoani Katavi. Aidha Siro amesema uharifu Mkoani Katavi umepungua kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na uharifu uliokuwepo katika miaka michache iliyopita. Wakati huo huo Kamanda Sirro ambaye aliwasili jana Mkoani Katavi kwa zaiara ya kikazi ya siku mbili,ameweka jiwe la msingi ujenzi wa zahanati ya jeshi la polisi Mjini Mpanda. Katika hatua nyingine IGP akiwa ameambatana na maafisa wa polisi kutoka makao makuu ya polisi nchini pamoja na waliopo Mkoani Katavi,amekagua na kuangalia maonesho mbalimbali ya namna jeshi la Polisi Mkoani...

SERIKALI IMEAGIZA KUSITISHA UVUVI ZIWA RUKWA

Image
Na.Issack Gerald SERIKALI mkoani  Rukwa imeagiza kulifunga ziwa Rukwa kwa muda usiojulikana kutokana na shughuli za uvuvi kuchangia kasi ya ugonjwa wa kipindupindu katika ziwa hilo. Mkuu wa mkoa huo Joachim Wangabo alitoa agizo hilo wakati akizingumza na wavuvi kwa lengo la kuwaeleza sababu za kulifunga ziwa hilo na kuzuia kabisa uvuvi kutoendelea. Alisema baada ya kukaa na wataalamu wa afya wamekubaliana kusitisha shughuli za uvuvi kwani zimekuwa chanzo kikubwa cha kuenea ugonjwa huo.  Alisema athari inayopatikana katika kambi hizo za uvuvi zitawaathiri walaji wa samaki wanaotokana ziwa hilo hasa waliopo Sumbawanga mjini kwani wanategemea samaki hapo Kama kutoweo na kuwataka walio waliopiga kambi katika ziwa hilo kwa ajili ya uvuvi waondoke mara moja kwani hawataruhusiwa kuingia ziwani kuendelea kuvua samaki.  Wakati huo huo aliagiza kufunguliwa maeneo maalumu kwa ajili ya kuwatibia wagonjwa  watakaopatikana kwani wasipofanya hivyo mlipuko wa ugonjwa huo...