WAKULIMA WA TUMBAKU MKOANI KATAVI WAILAUMU SERIKALI KUSHINDWA KUTEKELEZA KAULI YAKE
Na.Issack Gerald
Wakulima wa zao la tumbaku wa
chama cha msingi cha ushirika Mpanda Kati Mkoani Katavi wameilaumu serikali
kushindwa kutekeleza agizo lake la kuhakikisha tumbaku iliyo kosa soko
inanunuliwa.
Wakulima
hao kwa nyakati tofauti wamesema mpaka sasa hawajui hatima ya ununuzi wa
tumbaku yao huku wengine wakisema wameathirika kiuchumi na maisha kwa ujumla.
Hivi
karibuni,mwenyekiti chama cha msingi cha Ushirika Mpanda Kati Bw.Sosipeter
Salvatory ,alisema kuna kiasi cha kilo elfu ishirini na mbili ambazo hazijanunuliwa
kati ya kiasi chote cha tumbaku iliyozalishwa katika msimu wa mwaka mwaka
2016/2017.
Mnamo
Novemba 17 mwaka huu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akiahirisha vikao vya
Bunge mjini Dodoma alieleza kuwepo kwa kampuni itakayo nunua Tumbaku iliyosalia
pamoja na Mbaazi.
Habari zaidi ni
P5TANZANIA LIMITED
Comments