IGP SIRRO AWAOMBA VIONGOZI WA DINI MKOANI RUKWA KUHUBIRI AMANI ILI UHARIFU UPUNGUE
Na.Issack Gerald
Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon amewaomba viongozi wa
dini mkoani Rukwa Kuongeza bidii katika kuhubiri amani ili mauaji yanayotokayo
na imani za kishirikina na mapenzi yapungue mkoani humo.
IGP Sirro ametoa kauli hiyo wakati akijibu maswali ya waandishi
wa habari waliotaka kujua mikakati ya jeshi hilo katika kukabiliana na mauaji
mkoani humo.
Amesema jeshi la polisi linajitahidi kukabiliana na mauaji yote
yanayotokea nchini lakini katika Mkoa wa Rukwa takwimu zinaonesha kuwa mauaji
yanayotokana na ushirikina pamoja na wivu wa mapenzi yanaongoza mkoani
humo.
Kamanda Sirro amesema viongozi wa dini wana jukumu kubwa kuhakikisha
wanahubiri amani ili mauaji hayo yapungue kwani juhudi hizo zinapaswa kuwa za
pamoja kwa kuwa nao wana nafasi kubwa la kuwalea wananchi kiroho.
Wakati huo huo IGP Sirro ameahidi kuwa Jeshi hilo kupitia bajeti
zake litajenga kituo kipya cha polisi cha Sumbawanga mjini kwa kuwa kilichopo
ni kichakavu na majengo yanayotumika yalirithiwa kutoka kwa wakoloni.
Pamoja na kuahidi ujenzi wa kituo hicho,pia ameahidi kuupatia
mkoa wa Rukwa gari moja jipya aina ya Lori litakalosaidia kutumika katika
matumizi mbalimbali ya polisi mkoani humo kwa kuwa kuna upungufu wa vitendea
kazi.
Hata hivyo amewataka wananchi mkoani humo Kushirikiana na jeshi
la polisi na kubadirika kuacha kubweteka kwani hivi sasa maisha yamekuwa
tofauti na matukio mbalimbali yamekuwa yakiongezeka ni jukumu lao kujijali na
kujiepusha kutofanya uhalifu.
Kwa upande wake Mwenyekiti kamati ya wa ulinzi na usalama mkoani
Rukwa Joachim Wangabo ambaye pia ni mkuu wa mkoa huo amemwambia IGP kuwa
atajitahidi kuwashirikisha wafanyabiashara mkoani humo ili wajenge nyumba za
kuishi polisi kwa kuwa hawawezi kusubiri mpaka serikali ifanye kazi hiyo.
Habari zaidi ni
P5TANZANIA LIMITED
Comments