MKUU WA JESHI TANZANIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA ZAHANATI YA JESHI LA POLISI MKOANI KATAVI
Na.Issack Gerald
Mkuu wa jeshi la polisi
nchini IGP Simon,ameweka jiwe la msingi ujenzi wa zahanati ya Jeshi la Polisi
Mkoani Katavi.
Katika
taarifa ya Mkuu wa Polisi Wilayani Mpanda Maria Kwayi,amesema mpaka sasa zaidi ya shilingi milioni 7
zimekwishatumika katika ujenzi ambapo inahitajika zaidi ya shilingi milioni 29
ili jengo likamilike huku changamoto ikiwa ni upungufu wa vifaa vya ujenzi.
Kwa upande wake IGP sirro
mara baada ya kupokea taarifa hiyo amesema jeshi la polisi litaongeza takribani
milioni kumi na Tano ili kuunga juhudi za ujenzi wa zahanati hiyo.
Wakati huo huo IGP siro
aliyehitimisha ziara yake jana Mkoani Katavi amesema,wafanyabiashara Mkoani
Katavi,Jeshi la Polisi Mkao makuu na serikali kuu wataangazia hatua za haraka
ili zipatikane nyumba kwa ajili ya polisi ili kutatua uhaba wa nyumba za polisi
Mkoani Katavi.
IGP Simon Sirro alikuwa na ziara ya kikazi siku mbili juzi na
jana Mkoani katavi akitokea Mkoani Kigoma kabla ya kuelekea Mkoani Rukwa.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments