Posts

MVUA YA LEO MKOANI KATAVI IMELETA MADHARA

Na.Issack Gerald Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Katavi zimesababisha madhara katika makazi ya wakazi wa Mtaa wa Misunkumilo uliopo Manispaa ya Mpanda ukiwemo uharibifu wa miundombinu. Baadhi ya wananchi ambao makazi yao yameharibiwa ikiwemo kufa kwa mifugo kutokana na maji kukosa mwelekeo hali inayosababishwa na kutokuwepo kwa mitaro ya maji wameiomba serikali ichukue hatua. Kwa upande wa Mwenyekiti wa mtaa huo BW Katabi Jona ameutaka uongozi wa Manispaa kuichukulia hatua Kandarasi iliyo husika na ujenzi wa barabara za mtaa huo bila kuweka mitaro. Haya yana jili ikiwa ni siku moja tu tangu mamlaka ya hali ya hewa nchini TMA kutoa tahadhari juu ya uwepo wa Mvua kubwa. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

WAZIRI JAFO AMTUMBUA MKURUGENZI MKOANI RUKWA

Na.Issack Gerald Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI Mh.Suleiman Jafo,amemsimamisha kazi mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa Bw.Julius Kaondo. Waziri Jafo katika kikao na Waandishi wa habari,amesema amemsimamisha Bw.Kaondo kutokana na tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa pamoja na kushindwa kusimamia mradi wa maji. Kufuatia hatua hiyo,Waziri Jafo ametoa agizo k wa wakurugenzi watendaji na watumishi wa umma kutojihusisha na vitendo vya rushwa na amewataka wasimamie wajibu wao kama inavyotakiwa katika kutekeleza majukumu anayotakiwa kuyatekeleza kwa mjibu wa miongozo ya nchi. Jafo amesema amechukua hatua hiyo kwa kuzingatia vifungu vya sheria za nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mwezi uliopita Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Bukoba na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba walifukuzwa kazi na Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli kwa kushindwa kujibu maswali yake akitaka kujua kiwango cha fed...

WATU WENYE ULEMAVU MKOANI KATAVI BADO WANAKABILIWA NA KITISHO CHA HAKI ZAO KUTOPATIWA KIPAUMBELE

Na.Issack Gerald Imebainika watu wenye ulemavu Mkoani Katavi bado wanakabiliwa na kitisho cha haki zao za msingi kutopati wa kipaumbele na hivyo kuchochea unyanyapaa kuendelea kuwa mkubwa dhidi ya makundi hayo. Hayo yamebainishwa leo katika kikao cha kupokea taarifa mbalimbali kutoka kwa wadau wa kupinga ukatiri dhidi ya watu wenye ulemavu na kujadili namna matatizo ya watu wenye ulemavu yanashghulikiwa. Kwa upande wa mratibu wa mradi wa elimu jumuishi Mikoa ya Rukwa na Katavi Bi.Veronica Mavanza pamoja na mratibu wa mradi huo Mkoani Katavi Raphael Fortunatus,wameahidi kuzifanyia kazi changamoto zinazowakumba watu wenye ulemavu katika Mkoa ya Rukwa na Katavi. Mkurugenzi wa Shirika la International Aid Service(IAS) kutoka nchini Denmark Bw.Torben Madsen mara baada ya kikao cha leo,amesema shirika hilo litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kutatua changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu hasa katika sekta ya elimu. Makundi ya Mtandao wa wazazi wenye ulem...

RAIS MAGUFULI ATANGAZA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 8157 IMO FAMILIA YA BABU SEYA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli ametangaza msamaha kwa wafungwa 8,157 huku wanaotakiwa kutolewa siku ya leo wakiwa ni 1,828. Papii Kocha na Nguza Viking Rais ametoa msamaha huo leo wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya Uhuru wa Tanganyika Mjini Dodoma Leo. Rais Magufuli amesema amezingatia ibara ya 45 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayompatia rais mamlaka ya kutoa msamaha kwa wafungwa . Miongoni mwa waliotangaziwa kusamehewa ni pamoja na Nguza Viking anayefahamika pia kwa jina la Babu Seya na mwanae Papii Kocha waachiwe huru kuanzia leo. Wakati huo huo wafungwa 61 waliotakiwa kunyongwa hadi kufa wamesamehewa. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

MKOA WA RUKWA UMESHAULIWA KUONGEZA VITUO VYA HUDMA ZA AFYA

MKOA wa Rukwa umeshauriwa Kuongeza vituo vya kutolea huduma za afya ili kupunguza mlundikano wa wagonjwa unaoendelea kuongezeka siku hadi siku kutokana na ongezeko la watu. Naibu waziri wa ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Josephat Kandege alitoa ushauri huo hivi karibuni alipokuwa akizungumza na uongozi wa mkoa huo wakati akihitimisha ziara yake ya kikazi. Alisema kuwa hivi sasa mkoa huo unaidadi kubwa ya watu hali iliyosababisha kuwepo idadi kubwa ya wagonjwa katika maeneo ya kutolea huduma za afya hivyo nilazima mkakati wakujenga zahanati, vituo vya afya na hospitali uanze mara moja ilikuendana na idadi ya wakazi wa mkoa huo.  Waziri Kandege alisema kuwa fursa nyingine iliyopo ni kuyatumia majengo yanayo achwa na makampuni ya kigeni ya ujenzi wa barabara mkoani humo kwani yakibadilishwa na kuboreshwa yanaweza kufaa kutumika kutolea huduma za afya.  Alisema kuwa zipo baadhi ya wilaya hazina hospitali ni vizuri sasa zikajipanga kujenga ili kuwafikis...

UHABA WA WATUMISHI VITUO VYA AFYA UVINZA NA NGURUKA MKOANI KIGOMA.

VITUO vya afya Uvinza na Nguruka vilivyopo wilayani Uvinza Mkoa wa Kigoma vinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya upungufu wa watumishi katika kada zote na hivyo kuathiri ufanisi wakazi ambao unaweza kusababisha vifo kwa wagonjwa wanaohitaji huduma katika vituo hivyo. Zena Shaban na Mapinduzi Hamisi ni baadhi ya wananchi katika wilaya ya uvinza ambapo wameiamba mpanda redio kero wanazo kumbana nazo na mapendekezo yao kwa serikali. Stanford Chamgeni ambaye ni mganga mfawidhi wa kituo cha afya Nguruka amesema wanakumbana na kazi kubwa wakati wa kutoa huduma kwa wagonjwa ambapo kwa siku hutoa huduma kwa wagonjwa 80 hadi 100 huku mganga wa Kituo cha afya Uvinza Albert Msingwa akielezea upungufu wa majengo katika kituo chake. Naye Mganga mkuu wa Wilaya hiyo Albert Mumwi amekiri mapungufu hayo na kuelezea kuwa kufikikia sasa tayari wauguzi 10 wamepatiwa ajila na tayari wamepangiwa vituo vya kazi. Tatizo hilo la upungufu wa watumishi limetajwa kuwa kero ya muda mrefu kati...

MKOANI KATAVI AHUKUMIWA JELA MIAKA 20 BAADA YA KUKAMATWA NA NYAMA YA KIBOKO KILO 110

Mahakama ya Wilaya ya Mpanda imemuhukumu Omary Maganga (45) kutumikia jela kifungo cha miaka 20 baada ya kupatikana na hatia ya kukamatwa na nyama ya kiboko zaidi ya kilo 110. Hukumu hiyo Imetolewa leo Ijumaa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda,Chiganga Tengwa baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashitaka uliokuwa ukiongozwa na mwa nasheria wa Serikali, Flaviani Shio. Awali,katika kesi hiyo mwendesha mashitaka huyo alidai mahakamani hapo kuwa mshitakiwa Maganga alitenda kosa hilo Oktoba 10 mwaka 2016 nyakati za saa 10 jioni. Alidai kuwa siku ya tukio mshitakiwa alikamatwa akiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi huku akiwa na nyama ya kiboko yenye uzito wa kilo 118 ambayo thamani yake Sh 3.2 milioni. Mwanasheria huyo wa Serikali ameiambia mahakama kuwa mshitakiwa huyo alikamatwa na askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi baada ya kuwa wamepata taarifa kutoka kwa raia wema za kuwa mshitakiwa amekuwa akifanya ujangili kwen...