MVUA YA LEO MKOANI KATAVI IMELETA MADHARA
Na.Issack Gerald
Mvua
zinazoendelea kunyesha mkoani Katavi zimesababisha madhara katika makazi ya
wakazi wa Mtaa wa Misunkumilo uliopo Manispaa ya Mpanda ukiwemo uharibifu wa miundombinu.
Baadhi
ya wananchi ambao makazi yao yameharibiwa ikiwemo kufa kwa mifugo kutokana na
maji kukosa mwelekeo hali inayosababishwa na kutokuwepo kwa mitaro ya maji
wameiomba serikali ichukue hatua.
Kwa
upande wa Mwenyekiti wa mtaa huo BW Katabi Jona ameutaka uongozi wa Manispaa
kuichukulia hatua Kandarasi iliyo husika na ujenzi wa barabara za mtaa huo bila
kuweka mitaro.
Haya
yana jili ikiwa ni siku moja tu tangu mamlaka ya hali ya hewa nchini TMA kutoa
tahadhari juu ya uwepo wa Mvua kubwa.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments