RAIS MAGUFULI ATANGAZA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 8157 IMO FAMILIA YA BABU SEYA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli ametangaza msamaha kwa wafungwa 8,157 huku wanaotakiwa kutolewa siku ya leo wakiwa ni 1,828.
Papii Kocha na Nguza Viking |
Rais ametoa msamaha huo leo wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya Uhuru wa Tanganyika Mjini Dodoma Leo.
Rais Magufuli amesema amezingatia ibara ya 45 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayompatia rais mamlaka ya kutoa msamaha kwa wafungwa.
Miongoni mwa waliotangaziwa kusamehewa ni pamoja na Nguza Viking anayefahamika pia kwa jina la Babu Seya na mwanae Papii Kocha waachiwe huru kuanzia leo.
Wakati huo huo wafungwa 61 waliotakiwa kunyongwa hadi kufa wamesamehewa.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments