WAZIRI JAFO AMTUMBUA MKURUGENZI MKOANI RUKWA
Na.Issack Gerald
Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI Mh.Suleiman Jafo,amemsimamisha kazi mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa Bw.Julius Kaondo.
Waziri Jafo katika kikao na Waandishi wa habari,amesema amemsimamisha Bw.Kaondo kutokana na tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa pamoja na kushindwa kusimamia mradi wa maji.
Kufuatia hatua hiyo,Waziri Jafo ametoa agizo kwa wakurugenzi watendaji na watumishi wa umma kutojihusisha na vitendo vya rushwa na amewataka wasimamie wajibu wao kama inavyotakiwa katika kutekeleza majukumu anayotakiwa kuyatekeleza kwa mjibu wa miongozo ya nchi.
Jafo amesema amechukua hatua hiyo kwa kuzingatia vifungu vya sheria za nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwezi uliopita Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Bukoba na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba walifukuzwa kazi na Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli kwa kushindwa kujibu maswali yake akitaka kujua kiwango cha fedha kilichopokelewa na halmashauri hizo kwa ajili ya ujenzi wa barabara za ndani ya halmashauri zao.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments