WATU WENYE ULEMAVU MKOANI KATAVI BADO WANAKABILIWA NA KITISHO CHA HAKI ZAO KUTOPATIWA KIPAUMBELE
Na.Issack Gerald
Imebainika watu wenye ulemavu
Mkoani Katavi bado wanakabiliwa na kitisho cha haki zao za msingi kutopati wa
kipaumbele na hivyo kuchochea unyanyapaa kuendelea kuwa mkubwa dhidi ya makundi
hayo.
Hayo yamebainishwa leo katika
kikao cha kupokea taarifa mbalimbali kutoka kwa wadau wa kupinga ukatiri dhidi
ya watu wenye ulemavu na kujadili namna matatizo ya watu wenye ulemavu
yanashghulikiwa.
Kwa upande wa mratibu wa mradi wa
elimu jumuishi Mikoa ya Rukwa na Katavi Bi.Veronica Mavanza pamoja na mratibu
wa mradi huo Mkoani Katavi Raphael Fortunatus,wameahidi kuzifanyia kazi
changamoto zinazowakumba watu wenye ulemavu katika Mkoa ya Rukwa na Katavi.
Mkurugenzi wa Shirika la
International Aid Service(IAS) kutoka nchini Denmark Bw.Torben Madsen mara
baada ya kikao cha leo,amesema shirika hilo litaendelea kushirikiana na
serikali ya Tanzania katika kutatua changamoto zinazowakabili watu wenye
ulemavu hasa katika sekta ya elimu.
Makundi ya Mtandao wa wazazi
wenye ulemavu Wilayani Mpanda,Vyama vya watu wenye ulemavu na viongozi wa dini
wameshirikishwa katika kikao hichio.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments