Posts

CHANGAMOTO SKIMU YA UMWAGILIAJI RUKWA, MKUU WA MKOA ATOA AGIZO KALI KWA WAFUGAJI WA MIFUGO

Image
Na.Issack Gerald MRADI wa skimu ya umwagiliaji ya Ng'ongo wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa,unazidi kupungua uwezo wa kuzalisha mazao siku hadi siku kutokana na ukosefu wa maji pamoja na wafugaji wanaofuchungia mifugo katika eneo hilo. Akizungungumza jana mbele ya mkuu wa mkoa wa Rukwa,mwenyekiti wa mradi wa scheme ya umwagiliaji ya Ng'ongo Justine Amon alisema kwa kipindi cha mwaka 2015 /2016 wakulima walilima hekta 128 na kufanikiwa kuzalisha tani 460.8 za mahindi. Alisema katika msimu wa mwaka 2016/2017 katika hekta hizo 128 uzalidhaji umeshuka hadi kufikia tani 358.4 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo haribifu wa mazingira pamoja na wafugaji kuchungia ndani ya eneo la uzalishaji.   Amon alisema eneo linalofaa kwa umwagiliaji ni hekta 630 lakini zinazolimwa ni hizo 128 tu kwa kuwa ujenzi wa mfereji wenye urefu wa mita 3,000 haujakamilika kwa muda mrefu sasa. Mpaka sasa mfereji uliokalimilika unaurefu wa mita 1,725 ambao ndiyo unatumika katika umwagiliaji wa h...

WANANCHI WILAYANI SUMBAWANGA MKOANI RUKWA KULIPWA FIDIA KABLA YA UPANUZI UWANJA WA NDEGE

Image
Na.Issack Gerald WIZARA ya ujenzi,uchukuzi na mawasiliano imewahakikishia kuwalipa fidia wananchi wanaozunguka uwanja wa ndege Sumbawanga Mkoani Rukwa kabla ya kuanza upanuzi na ujenzi. Uwanja wa ndege wa Sumbawanga kabla ya kuharibika Kauli hiyo imetolewa na naibu waziri wa wizara hiyo Mh .Elias John Kwandikwa wakati akijibu swali la mbunge viti maalumu mkoani Rukwa Bupe Mwakang’ata aliyetaka kujua lini upanuzi na ujenzi wa uwanja wa ndege Sumbawanga utakamilika pamoja na kuwalipa fidia wananchi hao. Amesema wananchi wa Sumbawanga waendelee kuvumilia kwani muda wowote watalipwa fidia na kuongeza kuwa sheria itazingatiwa ikiwa wananchi hawatalipwa fidia zao kwa wakati ili walipwe fidia ya ziada. Aidha waziri Kwandikwa amesema mwezi Oktoba Mwaka 2016 serikali ilisaini mkataba na Kampuni ya SMPC kutoka Australia ili kusimamia ujenzi wa uwanja huo. Wakati huohuo mwezi Juni mwaka huu,serikali ilitiliana saini mkataba na kampuni ya Sino Shine Over Seas Construction And In...

JAMII MKOANI KATAVI IMETAKIWA KUSHIRIKI KUWAFICHUA WATOTO WENYE ULEMAVU WALIOFICHWA MAJUMBANI ILI WAPATE HAKI YAO YA ELIMU

Image
Na.Issack Gerald-Katavi JAMII Mkoani Katavi imeaswa kushirikiana ipasavyo na kamati ya kulea baraza la watoto wenye ulemavu iliyopo Wilayani Mpanda Mkoani Katavi kwa kuwafichua watoto waliofichwa majumbani ili wapatiwe haki ya elimu. Wanafunzi wenye ulemavu na wasio na ulemavui katika shule ya msingi Azimio Manispaa ya Mpanda wakiwa katika picha ya pamoja(PICHA NA.Issack Gerald) Aliyevaa koti kutoka kushoto ni mratibu wa Mradi wa elimu Jumuishi Mkoani Katavi,wa pili Issack Gerald mwandishi Mpanda Radio fm pia mjumbe na katibu wa kamati hiyo,waliobaki ni baadhi ya watoto wenye ulemavu (PICHA NA.Issack Gerald) Wito huo umetolewa leo na Meneja wa Mradi wa elimu jumuishi Tanzania Alani Kamunde wa shirika la International Aid Services,kupitia kikao cha kupokea,kujadili,kutathimini na kupanga mikakati ya namna ya kuyapatia ufumbuzi matatizo yanayowakbili watoto wenye ulemavu Mkoani Katavi. Kwa upande wake mratibu wa mradi wa elimu Jumuishi mikoa ya Rukwa na Katavi Bi.Veronic...

WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI IMEWATAKA WAVUVI WAKACHUKUE INJINI BOTI WAVUE SAMAKI KWA TIJA

Image
Na.Issack Gerald SERIKALI imetoa wito kwa wabunge wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania waliopo mwambao wa bahari na maziwa kuhamasisha vikundi vya wavuvi waliopo katika maeneo yao kupitia Halmashauri zao kujitokeza na kuchukua ruzuku ya boti injini 24 zilizobaki kwa ajili ya kuendesha shughuli za uvuvi zenye tija. Kauli hiyo imetolewa leo bungeni Dodoma na naibu waziri wa mifugo na uvuvi Mh. Abdallah Hamis Ulega wakati akijibu swali la Mbunge wa Mpanda Vijijini Mh.Moshi Suleiman Kakoso aliyetakakujua  ni lini serkal;I itawapatia vitendea kazi wavuvi wadogowadogo. Pamoja na mambo mengine Mh. Abdallah Hamis Ulega akijibu swali hilo amesema kwa mwaka wa fedha Mwaka wa fedha 2015/2016 serikali ya awamu ya tano ilitenga shilingi 400 zilizonunua boti injini 73 ambapo kati ya hizo injini 49 zilishachujkuliwa na vikundi vya uvuvi  nchini kwa mtindo wa ruzuku kupitia Halmashauri zao ambapo serikali inachangia 40 na vikundi 60%. Naye Mbunge viti maalumu Mkoani Katavi Anna Lup...

KWA MARA YA KWANZA HAPA NCHINI SIMBA ATIBIWA KWA KUFANYIWA UPASUAJI

Image
  Na Geofrey Stephen Ngoro Ngoro Taasisi ya wanyama pori TAWRI kupitia mtaalam wake wa wanyama pori Dkt.Ernest Mjingo amefanikiwa kuokoa maisha ya simba wenye matatizo ya ugonjwa ngiri kwa simba huyo mtoto. Simba Dkt.Ernest Mjingo amesema kwa mara ya kwanza wamefanya upasuaji na kufanikiwa kwa asilimia mia moja na kwamba simba huyo ataishi bila maradhi mara baada ya kupona na kurudi katika hali yake ya mwanzo. Hii ni mara ya kwanza kwa simba hapa nchini kufanyiwa upasuaji na kuimarika tofauti na wanyama wengine kupata maradhi na kufa kwa kukosa matibabu ya kitaaluma Msemaji wa wa ifadhi ya mamlaka ya ngoro ngoro worlter mairo amesema wanashukuru kuona simba huyo kupata matibabu na badae kuendelea kutangaza utalii wa ndani kwa kuongeza pato la taifa kupitia secta ya utalii Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

ASKARI WA WANYAMA PORI MKOANI ARUSHA WAMEINGIA MGOGORO NA WAFUGAJI

Image
Na Geofrey Stephen-Arusha. Wakazi wa kata za Ololosokwan,Soitsambu wilayani Ngorongoro mkoani Arusha,wamewashutumu baadhi ya askari wa mamlaka ya hifadhi ya Serengeti(Senapa) kukamata mifugo yao katika ardhi za vijiji na kisha kuipeleka ndani ya hifadhi. Moja ya alama inayotambulisha Mkoa wa Arusha Mwenyekiti wa kijiji cha Kirtalo,Yohana Toroge amesema,jumla ya ng’ombe wake 1000 walikamatwa   Novemba 4 mwaka huu  wakati wakielekea kunywa maji kisimamani na kisha kupelekwa ndani ya maeneo ya hifadhi. Aidha Wakazi hao walitoa kilio chao mbele ya waandishi wa habari katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Olosokwan uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kimila. Mkuu wa mamlaka ya hifadhi ya Serengeti (Senapa), William Mwakilema alijibu shutuma hizo na kusema wakazi hao wanatunga uongo kwa kuwa hakuna askari wake  anayekamata mifugo ndani ya ardhi za vijiji na kuwalipisha faini kubwa. Wenyekiti wa halmashauri ya Ngorongo...

SHIRIKA LA WORLD VISION KUKABIDHI VIFAA TIBA KWA VITUO VYA AFYA 111 MKOANI

Image
Na.Isaac Isaac-Kigoma Jumla ya vituo vya afya 111 vintarajiwa kunufaika kwa kupatiwa vifaa tiba pamoja na ujenzi wa wodi na vyumba vya upasuaji katika wilaya tatu (3) za mkoa wa Kigoma. Kigoma Ujiji Hatua hiyo ni kupitia mradi wa uboreshaji wa huduma ya mama na mtoto unaofadhiliwa na shirika la World Vision lengo likiwa ni kutoa hamasa kwa wajawazito  kujifungulia katika vituo vya afya. Kauli hiyo imetolewa na meneja mradi Monica Dedu kutoka katika shirika la world Vision wakati wa semina elekezi kwa viongozi wa madhehebu ya kidini pamoja na madiwani  katika Manispaa ya Kigoma ujiji ili kutia moyo na kuhamasisha  jamii kuona umuhimu wa kutumia huduma za afya. Naye Mganga mkuu wa mkoa Kigoma Poul Chaote amesema asilimia 65 ya akina mama wajawazito ndio wanaofika katika vituo vya afya kwa ajili ya kujifungua huku wengine wakijifungulia majumbani jambo linalohatarisha afya zao lakini pia usalam wa maisha ya watoto Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa kidini w...