Posts

RAIS MUGABE AMEMTUMBUA JIPU MAKAMU WAKE WA RAIS

Image
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amemfuta kazi Makamu wake wa Rais Emmerson Mnangagwa. Emmerson Mnangagwa Kwa mjibu wa Waziri wa Habari wa Zimbabwe Simon Kahaya Moyo,Bw.Mnangagwa (75) ameachishwa kazi kwa madai kuwa alionyesha tabia za kukosa uzalendo na uaminifu hasa kwa Rais. Kufutwa kwake ni ishara kuwa mke wa rais Robert Muabe, Bi.Grace,atafuata nyayo za mumeme za kuwa rais wa Zimbabwe Siku ya Jumapili Bi.Grace Mugabe alitoa wito wa kutaka mumewe amfute kazi Mnangagwa. Bw.Mnangagwa ambaye ni mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi,amekuwa kwenye mstari wa mbele kumrithi Rais Mugabe. Kufutwa kwake kunakuja baada ya Rais Robert Mugabe(93)kutishia kumuachisha kazi Bw Mnangagwa, hatua ambayo imezua uvumi kuwa anataka mke wake kuchukua hatamu za kuliongoza taifa hilo. Akihutubia mkutano wa wanachama wa makanisa ya asili mji Harare siku ya Jumapili,Bi Mugabe alisema Bw Mugabe alimtaka Mnangagwa na wafuasi wake kumuonyesha uzalendo au afutwe kazi. Chama cha Zanu-PF kinataraj...

WATOTO 2 WAMEPOTEA KATIKA MAZINGIRA TATANISHI MKOANI KATAVI

Na.Issack Gerald WATOTO wawili wakazi wa kitongoji cha Mnyaki B Rama na Vitisho wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 9 na 11 Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi,wamepotea katika mazingira ya kutatanisha. Mwenyekiti wa kitongoji cha Mnyaki B Bw.Alex Gezaho,amethibitisha kupotea kwa watoto hao Jumamosi iliyopita ambapo amesema,walikuwa wakiwinda ndege pori kwa manati. Kwa mjibu wa baadhi ya wakazi wa kitongoji cha Mnyaki B,watoto hao ambao ni wanafunzi wa shule ya Msingi Mnyaki mmoja akisoma darasa la pili na mwingine darasa la tatu ni miongoni mwa watoto watatu waliokuwa wakiwinda ndege siku ya juzi walipopotea. Watoto hao wawili wametajwa kuwa walikuwa wakiishi kwa mama mmoja anayeishi katika kitongoji cha Mnyaki B ambaye naye ametambulika kwa jina la mama Mwereza.                        Mwenyekiti wa kitongoji cha Mnyaki B amesema,tukio kama hilo ...

WATOZA USHURU PUNGUFU TA TANI 1 KUKIONA CHA MOTO,SERIKALI KUANZA KULIPA MISHAHARA YA WATUMISHI WA UMMA MWEZI HUU

Image
Na.Issack Gerald Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Magufuli ameviagiza vyombo vya ulinzi na Usalama nchini kuwakamata watumishi na watoza ushuru wote nchini watakamtomtoza ushuru mwananchi anayesafrisha mzigo usiozidi tani moja. Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo wakati akihutubia wananchi mjini Bukoba Mkoani Kagera ambapo alikuwa na shughuli ya kuweka jiwe la msingi upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba. Katika hatua nyingine,Rais Magufuli amesema kuanzia mwezi huu serikali itaanza kulipa stahiki zote za wafanyakazi wa umma wanazoidai serikali ikiwemo malimbikizo ya mishahara ambapo zaidi ya shilingi bilioni 159 zimetengwa kwa ajili hiyo. Rais magufuli amefanya ziara mkoani Kagera kama mwendelezo wa ziara zake za kikazi katika maeneo mbalimbali hapa nchini ambapo wiki iliyopita alifanya ziara katika mikoa ya Mwanza na Geita na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo. Kwa mjibu wa rais Magufuli,keshokutwa atakwenda Nchini Uganda kwa ajili ya kwenda kuweka jiwe...

DC MATINGA:MALIASILI WATAJENGA SHULE MBADALA WA NSANDA

Image
Na.Issack Gerald-Mpanda Sehemu ya majengo ya iliyokuwa shule ya Msingi Nsanda Mkuu wa wilaya ya Mpanda bi Liliani Matinga amewataka wananchi kuwa wavumilivu wakati wizara ya maliasili ikishughulikia kujenga shule ambayo itakuwa mbadala wa iliyokuwepo katika maeneo ya hifadhi walipoondolewa wananchi. Moja ya majengo ya vyoo vya iliyokuwa shule ya Msingi Nsanda Kauli hiyo imetolewa jana na Matinga ambapo amesema shule ya Msingi Nsanda ilijengwa kimakosa katika kijiji ambacho kilikuwa hakijasajiliwa hivyo wizara ya maliasili itayachukua majengo hayo na kujenga shule nyingine katika kijiji kilichosajiliwa. Ameeleza kuwa taratibu zote zimeshafanyika na tayari wizara ya maliasili imeshakubali kujenga na hivyo wanasubiri utekelezaji kuanza. Matinga amewaasa wananchi kuwa makini na wawekezaji wanao ingia katika maeneo yao ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima.                    ...

ASILIMIA 90 YA WACHIMBAJI MADINI MKOANI KATAVI WANACHIMBA MADINI BILA UTAFITI

Na.Issack Gerald-Katavi Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Magharibi Mhandisi Juma Haruna Sementa,amesema asilimia 90 ya wachimbaji wa madini Mkoani Katavi,wanashindwa kufikia malengo katika uchimbaji madini kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutofanya utafiti kabla ya kuchimba. Mhandisi Sementa amesema hayo wakati akizungumzia kuhusu baadhi maeneo ya uchimbaji kutelekezwa ikiwemo maeneo ya Kapalamsenga. Ametaja sababu nyingine inayokwamisha uchimbaji endelevu wa madini mkoani Katavi kuwa ni ukosefu wa mtaji wa fedha za kuendeshea mitambo. Katika hatua nyingine Kamishna Sementa amesema ujenzi wa kituo cha mfano cha kuchenjua madini kilichokuwa kimepangwa kukamilika ujenzi wake mwezi Septemba mwaka huu katika machimbo ya Kapanda,bado haujatekelezwa kutokana na uhaba wa fedha. Hata hivyo ametaja shughuli za uchimbaji madini bila utafiti ndiyo chanzo kinachopelekea uharibifu wa mazingira. Baadhi ya maeneo yanayotajwa kuwa na madini hususani dhahabu Mkoani Katavi ni pamo...

WATAKAOKAIDI KUONDOKA KATIKA HIFADHI ZA MISITU WILAYANI MPANDA KUONDOLEWA KWA NGUVU

Na.Issack Gerald-Mpanda Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga amepiga marufu kufanya shughuli za kilimo katika misitu iliyo hifadhiwa akisema kuwa wanaokaidi na kuendelea kuvamia maeneo ya hifadhi wataondolewa kwa nguvu. Bi.Matinga ametoa marufuku hiyo leo wakati akieleza za kuwepo kwa tetesi za baadhi ya wananchi walioondolewa katika maeneo ya hifadhi kutaka kuendesha  shughuli za kilimo. Aidha amesema serikali haitakubali kuangamiza uoto wa asili kutokana na watu wanaovamia misitu kwa kisingizio cha kukosa maeneo ya makazi huku sheria za kupata ardhi kwa matumizi ya kibinadamu zikiwa wazi. Miongoni mwa maeneo yaliyokumbuwa na operesheni ya wananchi  kuondolewa kinguvu  kwa madai ya kuvamia misitu ni Kijiji cha Mgolokani  kata ya Stalike,Kijiji cha Nsanda kilichopo kata ya Katumba na maeneo mengine.                          ...

MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO MTEGONI SUALA LA UKUSANYAJI MAPATO

Image
Uongozi wa Halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi umetakiwa kujitathimini kutokana na kushindwa kufikia malengo ya makusanyo ya mapato ya ndani. Pangani Smith-Mkurugenzi Nsimbo Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa TAMISEMI Joseph Kakunda    mara baada ya kupokea ripoti ya mkoa wa Katavi kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga. Aidha amefafanua kuwa serikali haitashindwa kuchukua hatua kwa watendaji wakuu wa halmashauri hiyo endapo hakutakuwa na mabadiliko ya haraka. Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo anatajwa kuwa matatani ikiwa ukusanyaji mapato utaendelea kuwa katika kiwango cha chini ambapo hatua huenda ikachukuliwa kwake kwa kushindwa kufikia malengo. Kwa mujibu wa Ripoti hiyo halmashauri hiyo ilikusanya mapato yake kwa 63% kinyume na agizo la Serikali ambayo inaagiza kufutwa kwa  halmashauri yoyote itakayo shindwa kufikia kiwango cha 80% kwa makusanyo yake. Mwandishi:Alinanuswe Edward,Mhariri-Issack G...