MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO MTEGONI SUALA LA UKUSANYAJI MAPATO

Uongozi wa Halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi umetakiwa kujitathimini kutokana na kushindwa kufikia malengo ya makusanyo ya mapato ya ndani.

Pangani Smith-Mkurugenzi Nsimbo

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa TAMISEMI Joseph Kakunda    mara baada ya kupokea ripoti ya mkoa wa Katavi kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga.

Aidha amefafanua kuwa serikali haitashindwa kuchukua hatua kwa watendaji wakuu wa halmashauri hiyo endapo hakutakuwa na mabadiliko ya haraka.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo anatajwa kuwa matatani ikiwa ukusanyaji mapato utaendelea kuwa katika kiwango cha chini ambapo hatua huenda ikachukuliwa kwake kwa kushindwa kufikia malengo.

Kwa mujibu wa Ripoti hiyo halmashauri hiyo ilikusanya mapato yake kwa 63% kinyume na agizo la Serikali ambayo inaagiza kufutwa kwa  halmashauri yoyote itakayo shindwa kufikia kiwango cha 80% kwa makusanyo yake.

Mwandishi:Alinanuswe Edward,Mhariri-Issack Gerald
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA