DC MATINGA:MALIASILI WATAJENGA SHULE MBADALA WA NSANDA
Na.Issack Gerald-Mpanda
Sehemu ya majengo ya iliyokuwa shule ya Msingi Nsanda |
Mkuu
wa wilaya ya Mpanda bi Liliani Matinga amewataka wananchi kuwa wavumilivu
wakati wizara ya maliasili ikishughulikia kujenga shule ambayo itakuwa mbadala
wa iliyokuwepo katika maeneo ya hifadhi walipoondolewa wananchi.
Moja ya majengo ya vyoo vya iliyokuwa shule ya Msingi Nsanda |
Kauli
hiyo imetolewa jana na Matinga ambapo amesema shule ya Msingi Nsanda ilijengwa
kimakosa katika kijiji ambacho kilikuwa hakijasajiliwa hivyo wizara ya
maliasili itayachukua majengo hayo na kujenga shule nyingine katika kijiji
kilichosajiliwa.
Ameeleza
kuwa taratibu zote zimeshafanyika na tayari wizara ya maliasili imeshakubali
kujenga na hivyo wanasubiri utekelezaji kuanza.
Matinga
amewaasa wananchi kuwa makini na wawekezaji wanao ingia katika maeneo yao ili
kuepusha migogoro isiyo ya lazima.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments