Posts

ASILIMIA 90 YA WACHIMBAJI MADINI MKOANI KATAVI WANACHIMBA MADINI BILA UTAFITI

Na.Issack Gerald-Katavi Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Magharibi Mhandisi Juma Haruna Sementa,amesema asilimia 90 ya wachimbaji wa madini Mkoani Katavi,wanashindwa kufikia malengo katika uchimbaji madini kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutofanya utafiti kabla ya kuchimba. Mhandisi Sementa amesema hayo wakati akizungumzia kuhusu baadhi maeneo ya uchimbaji kutelekezwa ikiwemo maeneo ya Kapalamsenga. Ametaja sababu nyingine inayokwamisha uchimbaji endelevu wa madini mkoani Katavi kuwa ni ukosefu wa mtaji wa fedha za kuendeshea mitambo. Katika hatua nyingine Kamishna Sementa amesema ujenzi wa kituo cha mfano cha kuchenjua madini kilichokuwa kimepangwa kukamilika ujenzi wake mwezi Septemba mwaka huu katika machimbo ya Kapanda,bado haujatekelezwa kutokana na uhaba wa fedha. Hata hivyo ametaja shughuli za uchimbaji madini bila utafiti ndiyo chanzo kinachopelekea uharibifu wa mazingira. Baadhi ya maeneo yanayotajwa kuwa na madini hususani dhahabu Mkoani Katavi ni pamo...

WATAKAOKAIDI KUONDOKA KATIKA HIFADHI ZA MISITU WILAYANI MPANDA KUONDOLEWA KWA NGUVU

Na.Issack Gerald-Mpanda Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga amepiga marufu kufanya shughuli za kilimo katika misitu iliyo hifadhiwa akisema kuwa wanaokaidi na kuendelea kuvamia maeneo ya hifadhi wataondolewa kwa nguvu. Bi.Matinga ametoa marufuku hiyo leo wakati akieleza za kuwepo kwa tetesi za baadhi ya wananchi walioondolewa katika maeneo ya hifadhi kutaka kuendesha  shughuli za kilimo. Aidha amesema serikali haitakubali kuangamiza uoto wa asili kutokana na watu wanaovamia misitu kwa kisingizio cha kukosa maeneo ya makazi huku sheria za kupata ardhi kwa matumizi ya kibinadamu zikiwa wazi. Miongoni mwa maeneo yaliyokumbuwa na operesheni ya wananchi  kuondolewa kinguvu  kwa madai ya kuvamia misitu ni Kijiji cha Mgolokani  kata ya Stalike,Kijiji cha Nsanda kilichopo kata ya Katumba na maeneo mengine.                          ...

MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO MTEGONI SUALA LA UKUSANYAJI MAPATO

Image
Uongozi wa Halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi umetakiwa kujitathimini kutokana na kushindwa kufikia malengo ya makusanyo ya mapato ya ndani. Pangani Smith-Mkurugenzi Nsimbo Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa TAMISEMI Joseph Kakunda    mara baada ya kupokea ripoti ya mkoa wa Katavi kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga. Aidha amefafanua kuwa serikali haitashindwa kuchukua hatua kwa watendaji wakuu wa halmashauri hiyo endapo hakutakuwa na mabadiliko ya haraka. Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo anatajwa kuwa matatani ikiwa ukusanyaji mapato utaendelea kuwa katika kiwango cha chini ambapo hatua huenda ikachukuliwa kwake kwa kushindwa kufikia malengo. Kwa mujibu wa Ripoti hiyo halmashauri hiyo ilikusanya mapato yake kwa 63% kinyume na agizo la Serikali ambayo inaagiza kufutwa kwa  halmashauri yoyote itakayo shindwa kufikia kiwango cha 80% kwa makusanyo yake. Mwandishi:Alinanuswe Edward,Mhariri-Issack G...

TFS WAMETOA ONYO KWA WAVAMIZI WA HIFADHI ZA MISITU MKOANI KATAVI

Image
Wakazi mkoani katavi wametakiwa kuacha tabia ya kuvamia misitu na kufanya shughuli katika hifadhi zinazoharibu uoto wa asili. Kauli hiyo imetolewa na Samwel Matula ambaye meneja wa misitu (TFS) kanda maalum ya mkoa wa Katavi ambapo amesema hakuna ruhusa ya watu kufanya shughuli kama kilimo au kuweka makazi katika hifadhi zilizopo katika maeneo mbalimbali. Hata hivyo meneja misitu wilaya ya mpanda Mustafa Abedi amewataka wote walioondolewa katika maeneo ya misitu kufuatia operesheni iliyofanyika mwezi wa saba mwaka huu ,kutorudi katika maeneo hayo na sheria kali zitachukuliwa kwa atakayekiuka agizo hilo. Mwezi Julai mwaka huu,operesheni ya kuwaondoa watu katika maeneo ya misitu kama vile msitu wa msaginya ,na misitu north east mpanda ilifanyika kwa lengo la kulinda misitu iliyopo Katavi kwa manufaa ya wananchi wote. Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

MASOKO YA USIKU MKOANI KIGOMA,HOFU USALAMA IMETANDA

Imeelezwa kuwa Masoko ya usiku katika baadhi ya kata za wilaya ya Buhigwe mkoani kigoma,yanapalekea matatizo kwa wakazi wa wilaya hiyo,yakiwemo matatizo ya kiusalama kutokana na wilaya hiyo kuwa mpakani mwa nchi jirani ya Burundi. Diwani wa kata ya Mkatanga ambaye ni makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe,Bw.Hamiss Lukanka  amesema soko hasa lililoko katika kata ya Mkatanga linapelekea hata watoto wa shule kutokupata muda wa kujisomea kutokana kutumia muda wao mwingi hasa wa usiku kuzurula sokoni humo. Amesema mpaka sasa wana mpango wa kuratibu na kusimamia soko hilo liwe linaanza muda wa asubuhi kwa siku maalum,ili kuondokana na changamoto zinazotokana na masoko ya usiku na kutoa nafasi kwa wakazi wa vijiji jirani kuleta bidhaa zao katika soko hilo. Katika upande mwingine Bw.Lukanka amewataka wananchi wa wilaya ya Buhigwe kufanya kazi kwa kushilikiana Bila kujali utofauti wa vyama wilayani humo,lengo kubwa  likiwa ni kuleta maendeleo ya wilaya yao. Ch...

TIMU YA CCBRT SASA NI MKOANI KIGOMA

Image
  Kampeni ya uhamasishaji wa matibabu ya ugonjwa wa   fistula inayoendeshwa na CCBRT inayofanyika Tanzania nzima,hivi sasa timu ya uhamasishaji matibabu ya ugonjwa huo mkoani Kigoma. Akiongea na timu hiyo mkuu wa mkoa wa Kigoma Bregedia mstaafu Emanueli Maganga ameeleza kufurahishwa kwake na juhudi zinazofanywa na CCBRT na kubariki ujio wa timu hiyo kwani utasaidia katika kueneza elimu juu ya ugonjwa huo kwa wakazi wa kigoma. Kwa upande wake meneja wa mradi wa fistula kutoka hospitali ya CCBRT iliyoko Msasani jijini Dar es salaam Bwana Clement Ndahana amesema kuwa kwa kila mwaka zaidi ya akina mama 3000 nchini hupata ugonjwa wa fistula lakini akina mama 1400 ndio ambao hupata matibabu ya ugonjwa huo. Mara baada ya salamu mkoani humo timu hiyo ya uhamasishaji imeelekea wilayani uvinza kijiji cha Kalia kilichopo mwambao wa ziwa Tanganyika ambako wataanza  na uhamasishaji wa matibabu ya ugonjwa wa fistula mkoni humo. Chanzo:Isaac Isaac,Mhariri-Issack Gerald Haba...

VYOMBO VYA USAFIRI KUFANYIWA UKAGUZI

Image
Wamiliki na madereva wa vyombo vya moto Mkoani Katavi wametakiwa kuhakikisha vyombo vyao vya usafiri vinafanyiwa ukaguzi. Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa kamati ya usalama Barabarani Mkoani Katavi Nassoro Alphi ambapo amesema zoezi hilo linafanyika nchi nzima na litadumu kwa kipindi cha mwaka mmoja. Amesema kuwa kwa mkoa wa katavi wameanza na magari ya abiria pamoja na Malori na ofisi ya Mkuu wa kitengo cha usalama barabarani imetoa wiki tatu ya ukaguzi wa hiari nje ya hapo zoezi la kukamata litaanza. Amesema lengo la kufanya ukaguzi huo ni kuhakikisha magari yote yanakuwa katika hali ya ubora na ambaye gari lake halitakaguliwa hata patiwa stika. Habari zaidi ni  www.p5tanzania.blogspot.com  au ukurasa P5Tanzania Limited