Posts

WANANCHI:UGAWAJI VIWANJA UPENDELEO MTUPU

Na.Issack Gerald-Katavi Baadhi ya Wakazi wa  Mtaa wa Msasani Kata ya Mpanda Hotel  Mkoani Katavi wameendelea kushikilia msimamo wao wakutokuwa na imani na utaratibu wa ugawaji wa viwanja katika eneo la Kampuni. Wakizunguzumza wamesema majina ambayo yametajwa kwa ajili ya kuhamia maeneo yaliyopangwa yanatoa taswira ya upendeleo. Hata hivyo kwa upande wake Afisa mtendaji Alex Msabaha anayesimamia mitaa hiyo amesema mchakato wa  makazi mapya umefanyika na kukamilika kwa amani na kwamba muda wowote kuanzia sasa wakazi hao watapewa maeneo kwa utaratibu uliowekwa. Mkutano huo ambao umefanyika jana ni utekelezaji wa agizo la Halmashauri ya Manispaa iliyoagiza kufanyika mkutano wa hadhara ili kuwashirikisha wananchi mchakato mzima ikiwemo majina ya wanaotakiwa kupata viwanja kama awamu ya kwanza.   Katika Mpango huo wa ugawaji viwanja vilivyop[o mtaa wa Kampuni kata ya Misunkumilo,mtaa wa msasani utapata viwanja 75 na Mtaa wa Tambukareli viwanja 75 ambapo viwanj...

RAIS MAGUFULI AMEPOKEA HATI 3 ZA MABALOZI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo amepokea hati za utambulisho za Mabalozi watatu waliopangiwa kuziwakilisha nchi za Oman,Uholanzi na China hapa nchini. Rais dkt John Pombe Magufuli Waliowasilisha hati zao kwa Mhe.Rais Magufuli,Ikulu Jijini Dar es Salaam ni Mhe.Ali Abdullah Al Mahruqi – Balozi wa Oman hapa nchini,Mhe. Jeroen Verheul – Balozi wa Uholanzi hapa nchini na Mhe.Wang Ke – Balozi wa China hapa nchini. Mhe.Rais Magufuli amewapongeza Mabalozi hao kwa kuteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini na amewahakikishia kuwa Serikali yake itafanya kazi nao kwa ukaribu ili kuendeleza na kukuza zaidi ushirikiano kati ya nchi hizo na Tanzania hususani katika uchumi. Mhe. Rais Magufuli amemuambia Balozi Jeroen Verheul wa Uholanzi kuwa Tanzania inayo gesi nyingi na itafurahi kupokea wawekezaji kutoka Uholanzi ikizingatiwa kuwa nchi hiyo ina uzoefu na teknolojia kubwa katika sekta hiyo. Kwa upande wa Balozi wa China hapa nchini Mhe. Wang ...

WAKULIMA WA KAHAWA KUTOKA KIGOMA KWENDA IKULU YA RAIS KUFIKISHA KILIO CHA MADAI YAO

Image
Chama cha ushirika cha wakulima wa kahawa  (AMKOS) wilayani Buhigwe mkoani Kigoma,kimechagua wawakilishi watatu,kwa ajili ya kuwawakilisha wakulima hao kwa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli. Wawakilishi hao watamfikishia Mh.Rais madai yao wanayodai kwa viongozi waliopita  wa chama hicho,ambapo ni muda wa miaka miwili sasa. Wamefikia maamzi hayo katika mkutano wa wanachama uliofanyika wilayani humo,kwa lengo la kujadili kuhusu madai yao wanayodai kwa viongozi waliopita wa chama hicho. Mwenyekiti wa chama hicho,Bw.Issa Madamu amesema, wakulima hao wanadai jumla ya sh.mil.27 kwa viongozi hao waliopita tangu 2015. Bw.Madamu amesema juhudi za kudai pesa hiyo,zimeenda hadi ngazi ya mkoa lakini bado hawajapata mafanikio na kwamba ndio maana wamechukua maamzi hayo ya kwenda kwa Rais ili wapatiwe ufumbuzi wa madai yao. Aidha wakulima hao wameiomba serikali ya mkoa wa Kigoma kuwahimiza viongozi wa ngazi za chini kushughulikia matatizo ya wananchi...

WANANCHI MKOANI TABORA WAMETAKA KITUO CHA POLISI KIFUNGULIWE

Wananchi wa kata ya Loya wilaya ya uyui mkoani tabora wameomba kufunguliwa kituo cha polisi katani humo kwa lengo la kukabiliana na matukio ya uharifu. Kata hiyo pamoja na kata nyingine nne hazina kituo cha polisi hali inayowalaizimu kutembea umbali wa zaidi ya kilometa 150 kufuata huduma za kipolisi katika kata ya Kigwa. Wakizungumza katika mkutano wa hadhara mbele ya kamanda wa polisi mkoa wa tabora ACP Wilbrod Mutafungwa wananchi hao wamesem kwa sasa wanakabiliwa na matukio mbalimbali ya uharifu ikiwemo wizi lakini imekuwa vigumu kudhibiti uharifu katika maeneo hayo kwa kuwa hakuna kituo cha polisi. Kamanda Mutafungwa baada ya kukagua jengo la kituo cha polisi katani hapo,ametoa muda wa wiki mbili kwa viongozi wa kata na wilaya kukamilisha ukarabati wa jengo la kituo cha polisi ili kifunguliwe na kuanza kuwahudumia wananchi. Wananchi wa kata ya Loya na kata jirani wanaamini kufunguliwa kwa Kituo hicho cha polisi kitakuwa mkombozi wa matukio mbalimbali ya uharifu. H...

WANANCHI WILAYANI TANGANYIKA WAMETAKIWA KUWASILISHA MALALAMIKO YA MIGOGORO YA ARDHI BADALA YA KUJENGA KIHOLELA

Na.Issack Gerald-Tanganyika Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imetoa wito kwa wakazi wa Halmashauri hiyo kuwasilisha malalamiko yao kuhusu migogoro ya ardhi badala ya kuamua kujenga kiholela katika maeneo yasiyoruhusiwa. Wito huo umetolewa na Mkuu wa idara ya ardhi na maliasili katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Bi.Josephine Beda Lupia wakati akizungumzia kuhusu mikakati iliyowekwa kudhibiti wakazi wanaojenga makazi holela katika maeneo yasiyo rasmi. Aidha Bi.Lupia amesema katika kuweka matumizi bora ya ardhi,halmashuari kwa kushirikiana na baraza la madiwani katika halmshauri hiyo,walipitsha kutengwa zaidi ya  hekta 46,000 kwa ajili ya sekta ya kilimo,uwekezaji na ufugaji. Katika hatua nyingine Bi.Lupia amesema katika mpango bora wa ardhi,walizingatia pia haki za makundi maalumu yasiyokuwa na uwezo kwa kulipia fedha taslimu na badala yake wakapewa nafasi ya kulipa kwa awamu ambapo jumla malipo yalikuwa hadi shilingi laki moja kwa kiwanja. Maeneo yaliyoku...

KAULI YA KAMANDA WA POLISI TABORA HII ITAZAA MATUNDA?AU NI DANGANYA TOTO?

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Tabora ACP Wilbrod Mutafungwa amewataka wananchi waliokimbia hivi karibuni kwenye kijiji cha Mwamabondo kurejea katika makazi yao. Wakazi hao walikimbia kufuati msako mkali uliofanywa na jeshi la polisi  baada ya wananchi hao kufanya jaribio la  kutaka kuwaua wanawake wanne waliowapiga na kuchomwa moto sehemu za siri kutokana na imani za kishirikina. Aidha Kamanda Wa Polisi Mkoani Tabora Amelazimika Kusafiri Umbali Mrefu Wa Zaidi Ya Kilometa 150 Kwa Ajili ya Kuzungumza na baadhi ya wananchi  waliobakia Kijijini Hapo. Wakati akizungumza na wananchi hao miongoni mwa mambo yaliyojitokeza Katika Mkutano huo ni pamoja na kuelezwa kuwa Mahudhurio ya wanafunzi wa shule ya msingi kijijni  hapo yameshuka kwa asilimia 30 kutokana na wazazi wa wanafunzi hao kukimbia kutakimbia makazi yao. Miongoni mwa Wanawake wanne walionusurika kifo wamelipongeza jeshi la polisi kwa kuokoa maisha yao. Mwanzoni mwa mwezi wa tisa mwaka...

CWT MKOANI KATAVI KIMEZUNGUMZIA SHULE ZA SERIKALI KUFANYA VIBAYA MTIHANI WA DARASA LA SABA MWAKA 2017.

Na.Issack Gerald-Katavi CHAMA cha walimu Tanzania CWT mkoani Katavi kimesema wanafunzi wengi wa shule za serikali wanashindwa kufaulu vizuri kwa kiwango cha juu kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mlundikano wa wanafunzi wengi darasani kwa wakati mmoja. Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu wa CWT Mkoani Katavi Hamisi Ismail ambapo amesema shule za binafsi zinafanya vizuri katika kufaulisha wanafunzi kutokana na kuwa na idadai ndogo ya wanafunzi darasani idadi ambayo ni rahisi mwalimu kuimudu anapokuwa anafundisha suala ambalo limekuwa gumu upande wa shule za serikali. Katika hatua nyingine amesema uwepo wa vitabu vingi vyenye mitaala inayotofautiana husababisha wanafunzi kuelewa mambo tofauti akisema kuwa ni vema serikali ikawa na kitabu kimoja kitakachotumika nchi nzima. Wakati huo huo Mwalimu Hamisi Ismail amesema chama cha walimu CWT mbali na kuwepo kwa ajili ya kutetea haki na maslahi ya walimu,pia kinahakikisha walimu wanawajibika katika kufundisha wanafunzi ipasav...