WANANCHI:UGAWAJI VIWANJA UPENDELEO MTUPU
Na.Issack Gerald-Katavi
Baadhi
ya Wakazi wa Mtaa wa Msasani Kata ya
Mpanda Hotel Mkoani Katavi wameendelea
kushikilia msimamo wao wakutokuwa na imani na utaratibu wa ugawaji wa viwanja katika
eneo la Kampuni.
Wakizunguzumza
wamesema majina ambayo yametajwa kwa ajili ya kuhamia maeneo yaliyopangwa yanatoa
taswira ya upendeleo.
Hata
hivyo kwa upande wake Afisa mtendaji Alex Msabaha anayesimamia mitaa hiyo amesema
mchakato wa makazi mapya umefanyika na
kukamilika kwa amani na kwamba muda wowote kuanzia sasa wakazi hao watapewa
maeneo kwa utaratibu uliowekwa.
Mkutano
huo ambao umefanyika jana ni utekelezaji wa agizo la Halmashauri ya Manispaa iliyoagiza
kufanyika mkutano wa hadhara ili kuwashirikisha wananchi mchakato mzima ikiwemo
majina ya wanaotakiwa kupata viwanja kama awamu ya kwanza.
Katika
Mpango huo wa ugawaji viwanja vilivyop[o mtaa wa Kampuni kata ya Misunkumilo,mtaa
wa msasani utapata viwanja 75 na Mtaa wa Tambukareli viwanja 75 ambapo viwanja
hivyo vimenunuliwa na mbunge kwa ajili ya wahanga wa bomoabomoa inayotarajiwa
kufanyika mwezi Januari mwakani.
Zaidi
ya wakazi 200 katika eneo hilo wanapaswa kuyahama makazi yao kutokana na kuwa
katika hifadhi ya reli ambapo iliamuliwa kuwa wawe wameondoka ifikapo januari
2018.
Comments