Na.Issack Gerald-Nsimbo Katavi Mtu mmoja anayefahamika kwa jina la James Modest mkazi wa Kijiji cha Mnyaki A kata ya Katumba Wilayani Mpanda amenusurika kuuwawa baada ya watu wanaosadikiwa kuwa majambazi kuvamia nyumbani kwake usiku wa kuamkia leo. Kwa mjibu wa James Modest ambaye ni Mhanga wa tukio hilo amesema ameporwa fedha taslimu shilingi 730,000 vifaa vya sola za umeme vyenye thamani ya shilingi 70,000. Aidha amesema ndani waliingia watu watatu na kuanza kumshambulia kwa vitu vizito ambapo walichukua kiasi hicho cha fedha na kumuamru awakabidhi simu ya Smartphone yenye thamani ya 220,000 pamoja,simu ndogo yenye thamani ya shilingi 40000. Shuhuda wa tukio hilo Yadunia Modest ambaye pia ni kaka wa aliyejeruhiwa na kuporwa mali zake,amesema mdogo wake amekatwakatwa kwa mapanga na kujeruhiwa puani na kichwani hali ambayo imemsababishia maumivu makali. Mwenyekiti wa kijiji cha Mnyaki A Bw.Kisele Meshack amethibitisha tukio hilo na kusema kuwa tukipo hilo limetok...