UTATA WAIBUKA UGAWAJI VIWANJA WAHANGA WA BOMOABOMOA MKOANI KATAVI
Na.Issack Gerald-Katavi
WAKAZI wa Mitaa ya Msasani na Tambukareli
Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wameeleza kutoridhishwa na mwenendo wa ugawaji
viwanja katika mtaa wa kampuni kata ya Misunkumilo wanakotakiwa kuhamia.
Wakizungumza kwa masikitiko ya
kutoelewa hatima ya wanakotakiwa kujenga makazi yao wamesema,wamesikitishwa na kauli
ya Mstahiki Meya Manispaa ya Mpanda Willium Mbogo kwamba wanaotakiwa kupewa
viwanja kwa sasa ni wazee, wajane na
wasiojiweza huku wengine wakiachwa bila kujua hatima yao kwa sasa.
Miongoni mwa wakazi wa msasani na
Tambukareli ambao wamezungumzia utata wa ugawaji viwanja ni pamoja na Joyce
Kledo Myomba,Tito Emmanuel,Magiroya Mkautani,Juliana Paul Mgawe,Aurelia ambapo
pia wamedai kuwa ikiwa watapelekwa wazee na watu wasiojiweza katika eneo hilo
pekee yao ni kudumaza maendeleo suala ambalo limeungwa mkono na baadhi ya wazee
wakisema inatakiwa iwe mchanganyiko ili washiriki kwa pamoja kuleta maendeleo.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa
Manispaa ya Mpanda Willium Mbogo amekanusha eneo la kampuni kupewa wazee,wajane
na wagonjwa peke yao ambapo amesema mgao huo utafanyika kwa wahanga wote
isipokuwa kipaumbele kimetolewa kwa wasiokuwa na uwezo wakiwemo wazee.
Aidha amesema mgao huo wa viwanja unaofanyika
kwa kuzingatia agizo la mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastian Kapufi ambaye
ndiye aliyenunua viwanja kwa ajili ya wananchi hao,ni ugawaji wa viwanja bure
Wakati huo huo Serikali za mitaa ya
Msasani na Tambukareli wameagizwa kufanya mikutano ya hadhara kuanzia kesho ili
kuwashirikisha wananchi juu wa wananchi wa awamu ya kwanza wanaotakiwa kupewa
viwanja ambapo kila mtaa umepewa viwanja 75.
Sakata la baadhi ya wakazi kutakiwa
kuondoka katika eneo ya hifadhi ya reli lilianza kuibuka mwezi juni mwaka huu
ambapo kutokana na ukosefu wa maeneo wanakotakiwa kujenga makazi mapya ili
kupisha eneo la reli kulisababisha wakazi hao kuongezewa miezi 6 na kutakiwa
kuondoka kabla ya mwezi Januari kupisha bomoa bomoa.
Kaya zaidi ya 200 za mitaa ya Msasani
na Tambukareli zinatakiwa kuondoka baada ya kuathiriwa na agizo la Shirika la
reli Tanzania TRL.
Comments