AFISA ELIMU KATAVI:TUNATATHIMINI MATOKEO DARASA LA SABA 2017 TUJUE TULIPOJIKWAA TUCHUKUE HATUA
Na.Issack
Gerald-Katavi
MKOA
wa Katavi umesema wanajitathimini ili kubaini sababu zilizosababisha kushuka
kiwango cha ufaulu katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba kwa mwaka 2017.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Afisa Elimu mkoani katavi Mwl.Ernest Hinju wakati ambapo amesema
wanafanya tathimini hiyo kwa kushirikisha wadau wa elimu kuzuia kutofanya
vibaya katika mitihani ijayo.
Kiwango
cha ufaulu wa darasa la saba kwa mwaka huu katika Mkoa wa Katavi kimeshuka
tofauti na mwaka jana ambapo katika matokeo ya mwaka jana kati ya mikoa 26 ya
Tanzania bara,Mkoa wa Katavi ulishika nafasi ya 2 kwa asilimia 86.80 na mwaka huu imeshuka kwa
kushika nafasi ya 9 kwa asilimia 90.01.
Mwl
Hinju akizungumzia matokeo ngazi ya Halmshauri,amesema ufaulu katika Manispaa
ya Mpanda umeshuka kutoka asiliamia 96 hadi 60,Nsimbo kutoka asilimia 84 hadi 71,Mpimbwe
ikishuka na kufikia asilimia 79%,Mpanda Vijijini ikishuka kutoka asilimia 66
hadi 83.
Hata
hivyo Halmashauri ya Wilaya ya Mlele kitaifa kwa mwaka 2017 imepanda hadi
nafasi ya 6 kutoka nafasi ya 40 kwa mwaka 2016 ambapo Mlele ndiyo ambayo
imeshika nafasi ya kwanza kimkoa.
Hata
hivyo Mwl Hinju amesema wanachunguza kama kuna uzembe uliofanywa na watendaji kwa
kila Halmshauri kuanzia walimu wakuu mpka maafisa elimu ili hatua zaidi
zichukuliwe.
Nao
baadhi ya wadau wa elimu Mkoani Katavi wamesema matokeo hayo huenda yametokana
na kuwepo kwa ushirikiano kati ya wazazi na walimu katika kufuatilia maendeleo
ya mtoto awapo shuleni.
Kwa
miaka mitatu Mfululizo kuanzia mwaka 2014,Mkoa wa Katavi ulikuwa ukishika
nafasi ya 1-3 huku Manispaa ya Mpanda ikishika nafasi ya 1 kwa kipindi
hichohicho.
Comments