Posts

RAIS MGABE AMETUMBULIWA

Image
Rais Robert Mgabe Shirika la afya duniani WHO limefuta uteuzi wa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe,kama balozi wa nia njema wa WHO. Awali alikuwa ameisifu Zimbabwe kwa kujitolea kuboresha afya ya umma Lakini wakosoaji walisema mifumo ya afya nchini Zimbabwe iliporomoka nchini humo chi ya utawala wa Mugabe wa miaka 30. Wafanyakazi mara nyingi hukosa kulipwa na madawa wakati mwingine hukosekana huku Mugabe mwenyewe mwenye umri miaka 93 akiwa anasafiri nje ya nchi kupata matibabu. Bw.Tedros alisema ameongea na serikali ya Zimbabwe na kuamua kumvua Mugabe wadhifa huo ni kwa manufaa ya WHO. Alisema anasalia kujitolea kufanya kazi na nchi zote na viongozi wake kujenga huduma bora za afya. Uteuzi wa Bw.Mugabe ulipatwa na shutuma kali kutoka nchi za Serikali ya Uingereza,waziri mkuu wa Canada na mashirika mengine kadha pamoja na watumiaji wa mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na kukosoa uteuzi huo. Kufuatia kukosolewa kutoka kwa mashirika ya haki za binadamu na kushangazwa kwa ...

MKUU WA SHULE MKOANI RUKWA AMEJIUA KWA KUKATA KOROMEO LAKE

Image
NKASI-RUKWA MKUU wa shule ya Sekondari ya Mtenga wilayani Nkasi mkoani Rukwa Leonard Mwipugi (29) amejiua kwa kujichoma kisu kwenye koromeo kutokana na wivu wa kimapenzi. 

TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KATAVI TANZANIA

Na.Issack Gerald-Katavi WILAYA ya Mpanda Mkoani Katavi imekumbwa na tetemeko dogo la ardhi ambalo halijajulikana ukubwa wake.

SHIRIKA LA WATERLEED WAMETOA MSAADA WA GARI 1 NA PIKIPIKI 26 KATIKA MKOA WA KATAVI

Image
Na.Issack Gerald-Katavi Shirika la Waterleeds  Program  Tanzani  WRP-T limetoa msaada wa  gari moja kwa  Manispaa ya  Mpanda na pikipiki 26 kwa Halmashauri za mkoa wa  Katavi zenye thamani ya  zaidi ya shilingi milioni 268.

RAIS MGABE AMETEULIWA NA UN KUWA BALOZI MWEMA WA AFYA

Image
Shirika la afya duniani WHO limemteuwa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kama 'balozi mwema ' katika kusaidia kukabiliana na magonjwa yaliyosahaulika . Akifafanua uamuzi wa uteuzi huo,Mkurugenzi mkuu mpya wa W.H.O.Dr Tedros Adha-nom Ghebre-yesus,alisifu namna Zimbabwe inavyozingatia afya ya umma. Lakini wakosoaji wamesema katika kipindi cha miaka thelathini na saba ya utawala wa rais Mugabe,huduma za afya zimekuwa mbaya ambapo wahudumu wa afya wamekuwa hawalipwi mara kwa mara na kumekuwa na ukosefu mkubwa wa dawa muhimu . Dr.Tedros ni raia wa Ethiopia ambaye ni Mwafrika wa kwanza kuongoza shirika la W.H.O. na alichaguliwa kwa ajili ya kukabiliana na kile kilichoaminiwa kuwa ni kugeuzwa kwa shirika hilo kuwa la kisiasa.

AJALI YA NDEGE CHINI KENYA

Ndege moja aina ya helikopta imeanguka katika ziwa Nakuru nchini Kenya muda mfupi baada ya kuondoka katika hoteli moja mjini humo.

WALIOUAWA KWA BOMU SOMALIA IMEFIKIA 358

Image
Mlipuko wa bomu Somalia uliowauawa zaidi ya watu 350 Serikali ya Somalia imesema idadi ya watu waliokufa katika shambulio kubwa la bomu la ndani ya Lori katika mji mkuu Mogadishu Jumamosi iliyopita imeongezeka na kufikia hadi watu 358. Lori lililipuka katika barabara ya makutano yenye shughuli nyingi na kuharibu hoteli,ofisi za serikali na migahawa . Hata hivyo haijabainika ikiwa eneo hilo la makutano ndilo lililolengwa au dereva wa Lori alilipua vilipuzi kwa sababu tayari watu walikuwa wameanza kushuku lori lake . Maafisa wamelilaumu kundi la wanamgambo wa al-Shabaab kwa shambulio hilo,lakini kundi hilo bado halijasema kuwa lilihusika na mlipuko huo Mlipuko huo uliwajeruhi watu zaidi ya mia mbili