TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KATAVI TANZANIA
Na.Issack Gerald-Katavi
WILAYA ya Mpanda Mkoani Katavi imekumbwa na
tetemeko dogo la ardhi ambalo halijajulikana ukubwa wake.
Tetemeko hilo ambalo athari zake hazijajulikana
limetokea leo saa 3:05 asubuhi na kuzua taharuki kwa wakazi wa wilaya ya Mpanda
kutokana na mtikisiko wa nyumba zao ambapo baadhi ya wakazi wamesema walikuwa
ndani.
Baadhi ya maeneo ambayo mpaka sasa yameripotiwa
kuguswa na tetemeko hilo ni mpanda mjini na baadhi ya kata zilizopo vijijini kama Kakese,Katumba na Mwamkulu.
Mwezi Mei
mwaka huu kulitokea matetemeko kadhaa ambapo kwa mjibu wa wataalamu wa jiolojia
hapa nchiniwalisema ni kutokana na mikoa ya Rukwa,Kigoma na Katavi kupitiwa na
bonde la ufa lililopo katika ziwa Tanganyika.
Hata
hivypo huenda maeneo mengi ya Mkoa wa Katavi yakawa yameguswa na tetemeko hilo
ambapo mpaka sasa hakuna madhara yaliyoripotiwa.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au
ukurasa P5Tanzania Limited
Comments