RAIS MGABE AMETUMBULIWA
Rais Robert Mgabe |
Awali
alikuwa ameisifu Zimbabwe kwa kujitolea kuboresha afya ya umma Lakini wakosoaji
walisema mifumo ya afya nchini Zimbabwe iliporomoka nchini humo chi ya utawala
wa Mugabe wa miaka 30.
Wafanyakazi mara nyingi
hukosa kulipwa na madawa wakati mwingine hukosekana huku Mugabe mwenyewe mwenye
umri miaka 93 akiwa anasafiri nje ya nchi kupata matibabu.
Bw.Tedros alisema ameongea
na serikali ya Zimbabwe na kuamua kumvua Mugabe wadhifa huo ni kwa manufaa ya
WHO.
Alisema
anasalia kujitolea kufanya kazi na nchi zote na viongozi wake kujenga huduma
bora za afya.
Uteuzi wa
Bw.Mugabe ulipatwa na shutuma kali kutoka nchi za Serikali ya Uingereza,waziri
mkuu wa Canada na mashirika mengine kadha pamoja na watumiaji wa mitandao ya
kijamii ikiwa ni pamoja na kukosoa uteuzi huo.
Kufuatia kukosolewa kutoka
kwa mashirika ya haki za binadamu na kushangazwa kwa mataifa mengi wanachama,WHO
haikuwa na lingine ila kufuata mpango wake wa kumvua Robert Mugabe wadhifa wa
balozi wa nia njema.
Comments