MKUU WA SHULE MKOANI RUKWA AMEJIUA KWA KUKATA KOROMEO LAKE
NKASI-RUKWA
MKUU wa shule ya Sekondari ya Mtenga wilayani Nkasi mkoani Rukwa
Leonard Mwipugi (29) amejiua kwa kujichoma kisu kwenye koromeo kutokana na wivu
wa kimapenzi.
Akizungumzia tukio hilo mratibu wa elimu kata ya Mtenga Hebron
Mwafungo alisema mwalimu huyo amekutwa akiwa amekufa baada ya kujichinja
nyumbani kwake majira ya saa 6 siku ya ijumaa.
Alisema mwalimu huyo jana alikwenda kazini kwake shule ya
sekondari Mtenga na baada ya majira ya saa 5 asubuhi alirejea nyumbani na
hakumkuta mkewe nyumbani na baada ya muda walipata taarifa kuwa
mwalimu huyo amekutwa amekufa baada ya kujichinja koromeo chumbani kwake
Aidha alisema mwalimu huyo alikua akiishi na mdogo wake wakike
nyumbani hapo na alipofika alimtuma mdogo wake huyo mbali na nyumbani
kwake na baada ya kurudi aliona damu zimetapakaa sebuleni na baada ya
kuchungulia chumbali alikuta kaka yake amefariki dunia kwa kujichinja ndipo
alipotoa taarifa uongozi wa kijiji hicho.
Alisema baada ya kumuhoji mdogo wa marehemu huyo alisema kuwa
kaka yake siku za nyuma alikua na mgogoro na mkewe akimtuhumu kuwa
si muaminifu katika ndoa yao lakini walizungumza na kuumaliza mgogoro
huo.
Siku chache baadaye mke wa marehemu huyo aliondoka nyumbani na
kwenda mjini Namanyere bila kumuaga mume wake huenda jambo hilo lilimkasilisha
kaka yake na kufikia uamuzi wa kujichinja.
Diwani wa kata ya Mtenga Pankrasi Maliyatabu amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa baada ya tukio hilo walitoa taarifa polisi
ambao walifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka katika
chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya wilaya ya Nkasi.
Kamanda wa polisi mkoani Rukwa George Kyando alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo nakuongeza kuwa bado uchunguzi wa polisi unafanyika
kufuatia tukio hilo.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au
ukurasa P5Tanzania Limited
Comments