Posts

WAZEE MKOANI KATAVI WAOMBA SERIKALI IWATENGENEZEE MAZINGIRA RAFIKI KATIKA MASUALA YA MATIBABU-Septemba 29,2017

Na.Issack Gerald-Katavi UMOJA wa wazee Mkoani Katavi kimeiomba serikali kuendelea kutengeneza mazingira yatakayomwezesha mzee kupatiwa huduma za matibabu bila usumbufu.

VIBOKO MKOANI KATAVI WASABABISHA NDOA KUVUNJIKA PIA UHARIBIFU WA MAZAO SHAMBANI-Septemba 29,2017

Image
Mfano wa picha ya viboko vinavyopatikana mto sitalike mkoani katavi Na.Issack Gerald-Katavi WAKAZI wa kijiji cha Milala Kata ya Misunkumilo katika Manispaa ya Mpanda,wameilalamikia serikali kutochukua hatua dhidi ya viboko waliopo bwawa la Milala vinavyoharibu mazao shambani na kutishia uhai wa binadamu mara kwa mara.

WAKAZI KATA YA MPANDA HOTEL WAELEZEA KUFURAHISHWA NA HATUA YA KUTATUA TATIZO LA MAJI-Septemba 29,2017

Na.Issack Gerald-Katavi BAADHI ya wakazi wa kata ya Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda wameelezea kufurahishwa na hatua ya uchimbaji mitaro ya kupitisha mabomba kwa ajili ya kuleta huduma ya maji katika katika kata hiyo.

HALMASHAURI ZOTE MKOANI KATAVI ZATAKIWA KUANDAA VITAMBULISHO VYA WAZEE-Septemba 28,2017

Na.Issack Gerald-Katavi Halmashauri  zote Mkoani Katavi zimetakiwa kuandaa vitambulisho kwa wazee wote waliokidhi vigezo vya kupatiwa matibabu bure.

WANAFUNZI 417 WAKATISHA ELIMU WILAYANI MLELE-Septemba 27,2017

Na.Issack Gerald-Mlele Katavi ZAIDI ya wanafunzi 417 wa sekondari katika halmashauri ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi wamekatisha masomo yao kwa kipindi cha kati ya mwaka 2014 na 2016 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mimba na utoro Hali hiyo imebainishwa na Afisa elimu idara ya Sekondari Bw.Sylivanus Raphael Kunambi ambapo amesema kuwepo changamoto ya wanafunzi kuikatisha masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo utoro na mimba. Kunambi amesema kwa mwaka 2014 wanafunzi 108 sawa na asilimia 17.4 ya wanafunzi wote waliokuwa wamesajiliwa katika mwaka huo hawakuhitimu huku mwaka 2015 idadi ya wanafunzi ambao hawakumaliza masomo yao ikiongezeka na kufikia 160 sawa na asilimia 22.9  wakati huo kwa mwaka 2016 wanafunzi 149 sawa na asilimia 20 ya wanafunzi wote waliokuwa wamesajiliwa wakishindwa kuhitimu elimu ya sekonadri.. Aidha ametaja sababu nyingine inayosababisha wanafunzi kutohitimu elimu ya Sekondari ni pamoja na jamii ya wafugaji wanaohama hama katika wilaya ya Mlele hal...

NDUGU 6 MKOANI RUKWA WAHUKUMIWA KUNYONGWA-Septemba 27,2017

Image
Na.Issack Gerald-Sumbawanga Rukwa NDUGU sita wa familia moja wamehukumiwa kifo kwa kunyongwa baada ya kuthibitika Kuwa walimuua ndugu yao wakimtuhumu Kuwa ni mchawi.

MBUNGE JIMBO LA NSIMBO ATUHUMIWA KUJIHUSISHA NA RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA UVCCM WILAYANI MPANDA KATAVI -Septemba 27,2017

Image
Mbunge Jimbo la Nsimbo Richard Mbogo MBUNGE wa jimbo la Nsimbo wa jimbo la Nsimbo Richard Philipo Mbogo ametuhumiwa kuwa miongoni mwa watu waliohusika katika kutoa rushwa ya fedha kwa kila mjumbe aliyeshiriki katika uchaguzi wa viongozi wa Jumuiya ya Vijana ya chama cha Mapinduzi CCM Wilayani Mpanda.