Posts

WAISLAMU KATAVI WATAKIWA KUWA WAMOJA NA WENYE MOYO WA HURUMA-Septemba 1,2017

Image
WAISLAMU mkoani Katavi wametakiwa kuwa wamoja na wenye mshikamano katika hali mbalimbali ya maisha ya kila siku wanayopitia bila kujali itikadi ya chama,rangi,dini,kabila wala taifa analotoka kwa kuwa wote ni binadamu ambao wameumba na mwenyezi mungu.

SITA WAHUKUMIWA MIAKA 20 JERA KWA JARIBIO LA KUUA,YUMO MWENYE UALBINO ALIYEKATWA MKONO-Septemba 1,2017

Image
MAHAKAMA Kuu  ya Tanzania Kanda ya Sumbawanga  imewahukumu  washtakiwa  sita   kati ya kumi kifungo cha miaka 20 jela baada  ya  kuwatia hatiani kwa makosa mawili ya kula njama ya kuua na jaribio la kumuua mtoto mwenye  ulemavu wa  ngozi ‘albino” Mwigulu Matonange (13) kwa kumkata mkono wake wa kushoto .

MKOANI KATAVI SIMBA AVAMIA KIJIJI MTOTO ANUSURIKA KUTAFUNWA-Agosti 31,2017

Image
MTOTO mmoja mwenye Umri wa miaka 13 Mkazi wa Isinde kata ya Mtapenda,Halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi,amenusurika kufa baada ya kushambuliwa na Simba akiwa nyumbani kwao. Inaelezwa kuwa smba huyo alivamia kijijini hapo majira ya saa kumi usiku wa jana mpaka alipoanza kumshambulia mtoto huyo anayejulikana kwa jina la Nyutuliangila Madirisha.

POLISI,JAJI MKUU WATOA ONYO MGOMO WA MAWAKILI HAPA NCHINI-Agosti 28,2017

Image
Kaimu  Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma na Jeshi la Polisi nchini,wamelionya Baraza la Uongozi la Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS),kutoingilia vyombo vya uchunguzi na upelelezi,vinavyochunguza tukio la mlipuko,uliotokea kwenye ofisi za Kampuni ya Mawakili ya IMMMA usiku wa kuamkia juzi jijini Dar es Salaam.

POLISI WAWEKA WAZI MAJIBU YA UCHUNGUZI OFISI ZA MAWAKILI IMMMA KULIPULIWA-Agosti 28,2017

Image
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, leo limesema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa watu wasiojulikana utambulisho wao na idadi yao walifika katika ofisi za Mawakili wa IMMMA Advocates wakiwa katika magari mawili na kujifanya ni maaskari na kuwarubuni walinzi na kuondoka nao katika gari mojawapo kabla ya kulipua jengo hilo.

RAIS MAGUFULI AWATAKA TAKUKURU KUTOKUWA NA KIGUGUMIZI DHIDI YA WAHUSIKA VITENDO VYA WA RUSHWA-Agosti 28,2017

Image
Rais Magufuli akiwa ndani ya Ofisi ya Takukulu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewataka viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU ) kutokuwa na kigugumizi cha kuchukua hatua pale wanapokuwa na ushahidi dhidi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya rushwa.

OFISI ZA WANASHERIA AKIWEMO MTOTO WA RAIS FATUMA KARUME NA LAURENCE MASHA ZATEKETEA KWA MOTO USIKU WA KUAMKIA LEO-Agosti 26,2017

Image
Sehenu ya majengo ya Ofisi Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,Lucas Mkondya amethibitisha kushambuliwa ofisi za wanasheria za IMMMA saa 8 usiku wa kuamkia leo.